Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,031
- 25,765
- Thread starter
- #41
Economics ni simple logic mkuu.Hapa ni price ndiyo inayopanda,pako clear kabisa,economics Iko tofauti na wengi tunavyofikiri,Ina lugha yake, demand ni ability and willingness..then how scarcity affects that!?...mwigulu aliposema uchumi waachiwe wachumi kujadili,tuliosoma uchumi tulimuelewa
Kama kuna watu kumi na kilo kumi za sukari, kuna kila uwezekano kila mtu akapata kilo moja kwa shilingi elfu moja.
Sokomoko ni pale scarcity ya sukari inatokea, kuna kilo mbili sokoni.
Katika wale watu kumi basi ni yule mwenye uwezo wa kuinunua kilo hizo mbili zote kwa shs elfu tano kwa kilo ndiye ataipata sukari, muuzaji shida yake faida.
Hiyo ni gaph ya diminished quantity na higher prices.
Vile vile, kama kuna watu walewale kumi, na sukari iko kilo hamsini ghalani hadi inakaribia kuharibika, mtu ataiuza hata shs mia tano ili isiharibike.
Vile vile, kama kuna sukari, iwe na tatizo,mathalani imeingia mafuta ya taa na watu hawaitaki, hiyo sukari hata uigawe bure, zero price, hakuna demand hapo ,hakuna anayeitaka.
Hivyo basi, scenarios zipo nyingi tu kuelezea masuala ya scarcity, demand, supply na price.
Katika varables zote hizo ukiingiza kitu elekezi , matokeo yake unaweza shindwa ku control matokeo yake.