Jana ilinipa shida sana kuelewa CCM walikuwa wanatafuta uwakilishi gani!!??Bunge ni chombo kikubwa katika nchi na ni sehemu ambayo hutumika kanuni na busara katika kuamua mambo yake. Mabunge mengi duniani hutumika kama nyenzo ya kutuliza hali pale inapochafuka hata pale muhimili mmoja unapochafua hali. Tumeshuhuidia busara ikitumika kwa kuielekeza serikali kutekeleza baadhi ya mambo ili tu kuondowa sintofahamu kwenye jamii ama baina ya serikali na wafanyakazi ama serikali na kundi fulani katika jamii.
Hili la mgogoro wa CUF bunge limetumika kufanya ushabiki sana na kukoleza moto. Wanajuwa kuna MGOGORO pale na kesi iko mahakamani hili wanalijuwa. Busara ingetumika kuhusu nafasi ya mgombea wa EALA kutoka CUF basi walau wangeiacha nafasi wazi mpaka mgogoro uamuliwe mahakamani.
Ilichokifanya Bunge letu la JMT kupitia Job ndugai na Kashilila ni kutaka kulidhalilisha Bunge letu mbele ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na tuonekane watanzania kuwa ni mbumbumbu. Hapana.
Tokea Mwanzo dalili zilishaonekana kuwakamia upinzani na kufanya siasa zisizo tija. Tunashindwa kujuwa wakati gani maslahi ya Taifa yatangulizwe mbele na wakati gani tufanye siasa. Ikiwa hapa Bunge linafanya zile siasa za kukomoana kwa wapinzani , wamesahau kuwa vyama hivi vina wanasheria weledi na yumkini suala litafika mahakama ya EAC. Itategemea maamuzi ya kisheria lakini naona tunaweeza kuadhirika kama taifa.
CUF inajulikana ilishamfukuza uanachama Habib Mnyaa tena kwa katiba ya CUF mamlaka hayo yako katika tawi lake huko mkanyageni Pemba. Na wala si CUF Taifa. Ikumbukwe pia kuwa Mnyaa alikuwa mwanaCHAMA WA KAWAIDA TU HAKUWA KIONGOZI AMBAYE TUNGESEMA YUKO KWENYE MGOGORO ULE ULIOPO WA KIUONGOZI. Hivi hili bunge letu hili wanalijuwa?
Kukimbilia kuwatambuwa eti wagombea wote wa CUF bila kusubiri kujuwa hatma ya maamuzi ya Mahakama ni kupoteza rasilimali na muda bure. Ikitokea kesi ya msingi ya mgogoro wa CUF ikaamua vyenginevyo dhidi ya Lipumba na genge lake bunge letu litasemaje kuhusu utoto huu waliofanya wa kukosa busara tena za kawaida?
Hawakumbuki kuwa ni juzi tu Mahakama imemzuiya Msajili kuwapa ruzuku CUF mpaka kesi ya msingi itakapoamuliwa iweje leo bunge lije likoleze mgogoro na kushindwa kutumia busara?
Tunawatakia kila la heri wateuliwa.
Kishada.
Nilifikiri kilichokuwa kikitafutwa ni uwakilishi wa Tanzania ndani ya bunge la Afrika Mashariki,kwa nilichokiona ilikuwa kukomoana kati ya CCM na upinzania.
Honestry kama wabunge wa CCM wataendelea na upuuzi huu,hakuna hata haja ya kuwa na uwakilishi majimboni,ni upotevu wa pesa za walala hoi!!
Kwa nini tuhangaike na uvyama kwenye uwakilishi wa nchi? Busara,hekima na utaifa vinakosekana mpaka kwa spika wa bunge!!??
Inasikitisha, inatia hasira mpaka inafikia hatua unachukia nchi sababu ya kuwa tunahangaishwa na uvyama mpaka sehemu ambayo ni just kuangalia utaifa na kuweka kando upuuzi wa vyama.
Na itachukua miaka mingi sana kwa nchi yetu kwenda mbele mpaka hapo adui MKUBWA na nambari wani kuja kupotea ambaye ni UJINGA...kwa nilivyoona elimu yetu itaendelea kuwa ya chini ili wajinga tuendelee kuwa wengi na wenye dola yao waendelee kuishikilia. Kwa taifa lenye wananchi wenye uelewa sarakasi ya jana ilitosha kabisa kuwaadabisha watu.
Kwa nini????