Kuelekea 2025 Kuhusu Katiba mpya/ Sheria mpya za Uchaguzi, mimi nitakuwa mstari wa mbele

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mushkov

JF-Expert Member
Feb 16, 2024
244
527
Ndugu zangu Maaskofu, Masheikh, Mapadre, Wachungaji, Manabii, Mitume na Watanzania wote, suala la Katiba mpya na Sheria mpya za Uchaguzi linatuhusu sisi sote.

Katiba mpya na Sheria mpya za Uchaguzi si kwa ajili ya chama/ vyama vya siasa tu, bali ni kwa ajili ya Watanzania wote.

Katiba mbovu inaleta uchaguzi m bovu, Uchaguzi m bovu unaleta viongozi wabovu, viongozi wabovu wanaleta huduma za jamii mbovu au hawaleti kabisa, huduma za jamii mbovu husababisha maisha duni ya Watanzania.

Kwa muktadha huu, Katiba mpya na Sheria mpya za Uchaguzi vinatuhusu sote.

Nawaomba sana viongozi wa Dini tusikae nyuma ya pazia kana kwamba haituhusu, naomba tuwe mstari wa mbele katika hili.

Elimu ya Uraia kuhusu umuhimu wa Katiba bora itolewe maeneo yafuatayo:-

Makanisani, Misikitini, Kwenye kumbi za harusi na matukio mengine, vijiweni, kwenye mikusanyiko ya watu na hata kwa mtu mmoja mmoja.

Kila mtu Mtanzania awe na wajibu wa kutoa Elimu hii ya Uraia kuhusu umuhimu wa Katiba mpya.
 
Back
Top Bottom