Nauliza hivi sababu najua jukwaa hili tutapata muafaka wa hili jambo tukiweka kwa pamoja mawazo yetu katika jambo hili ambalo hua lina mkanganyiko katika mahusiano mengi.
Lakini je nauliza mapenzi ya dhati lazima yapimwe kwa zinaa? Naomba nitumie neno hilo kali mana ndilo linavyoitwa hivo katika Biblia kwa wanaokutana kimwili kabla ya ndoa. Au ngoja tu nipunguze ukal wa neno..je sex ndo kipimo cha mapenzi ya kweli?
Unakuta watu wawili mmekubaliana kabisa ..mwanaume amekubaliana na mwanamke kwamba wasubiriane.hadi ndoa ndipo watakapofanya sex ama tendo la ndoa mana wapo ndoani sasa,
lakini katika kusubiriana huko mmoja kati ya wapenzi hao anatembea na mtu mwingine, anakua na mahusiano na mtu mwingine na haichukui mda wana sex, lakini yule mpenz wako anaekupenda kwa dhati aliekuvumilia na ambae mlikubaliana kwa dhati kwamba msubiriane mana hio sex mtaenda kuifanya kwa nafas mkiwa kwenye ndoa,
lakini wapi huyo unamuona sjui mshamba ama vipi ama hukumpenda ulikua unamtumia for your own selfish reasons ama sabab tu nyingine ambayo hazina mashiko, then huyo mwingine unamvulia nguo free kabisa mnafanya sex bila shida yoyote.
Badae matokeo yake mhusika ananogewa na mimba anashika anaamua kukuacha kabisa. Cases hizi zipo sana kwa wanawake na pia wanaume, na kwakwel inauma sana mana utafikiria kwamba through all that time alikufikiriaje ama alikuchukuliaje?
Kuna mdada mmoja mpenz wake alikua wamekubaliana kwamba April hii aje nyumban kujitambulisha, na situation ilikua kama hii nayoilezea kua walikubaliana wajitunze hadi ndoa ndio sex, lakin ghafla bin vuu jamaa kapita alipopita kampa.msichana mwingine mimba.
Mdada kachanganyikiwa na nyumban walikua wamejiandaa na ugeni mzito wa wakwe. Hamna kilichoendelea. Badae jamaa anasema alizidiwa, sasa najiuliza kama mtu uko na mpenz wako umezidiwa na unataka kwanini msiambizane tu, jamaa si angempa mimba tu mpenz wake?
Je kwani sex before marriage inakubalika kweli, na kwan ni kipimo cha upendo kweli? wanadai lazima upime sijui, kwamba mwenzangu yuko vipi, kwani amekua mchele? Na je vitabu vitakatifu vinasemaje?
Biblia inasema...Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe.
Sijui kwa wenzangu waislamu sijui katika kitabu chenu kitakatifu cha Quran kinasemaje kuhusu hili...mana lazima twende na maandiko sasa
Kama mfano mwingine mada flan imeletwa jukwaa hili, jamaa wamekubaliana na mpenz wake wa kike vizuri kwamba sex hadi ndoa, mwanamke akatambulishwa kwao, means mahusiano yalikua na muelekeo, kumbe mwanamke anafanya yake huku na kumvulia nguo mwanaume mwingine na mimba juu, na mipango ya ndoa iko katika hatua za mwisho, yule mpenz wake anaempenda kwa dhati akamuona mjinga, ndio jamaa anaambiwa akaanza kulia hadharani.
Msondo ngoma walisema ukiona mtu mzima analia mbele za watu ujue kuna jambo. Tujadiliane hili kua nini hasa kinatokea ?? Ni mapepo ama nini?.ama kulogwa..!! Hivi upendo ama mapenzi ya kweli kabla ya ndoa yanaweza kupimwa kwa zinaa kweli???