Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,797
Watu wanaielewa dunia kwa kusoma, kusafiri, kuchangamana na jamii tofauti nk. Ukipata bahati ya kufanya hata kazi za ndani kwa watu wa aina hii unapata ahueni.
Kazi za ndani kwa houseboy au house girl atahakikisha kabla ya ajira una sehemu ya kuishi ambayo unamudu kuilipia. Inawezekana ikawa ni servants quater ndani ya uzio wa nyumba yake, lakini inajigetemea. Au anakupa mshahara unaotosha kulipa pango la nyumba na usafiri wa kila siku.
Atakupa mkataba wa kazi, inawezekana ikawa saa 08: 00 - 16:00 Jumatatu mpaka Ijumaa na uniforms utapewa. Pamoja na hayo unapata likizo yenye malipo ya mwezi mmoja kwa mwaka. Kwa mshahara unaopata unamudu kujikatia Bima ya Afya.
Kwa wengine kufanya kazi za ndani ni utumwa. Unalala saa saba usiku na kuamshwa saa 11 alfajiri. Unalazwa sebuleni na baba wa nyumba anaona ni halali kukubaka. Mshahara ni haki yako lakini mwisho wa mwezi hadithi zinaanza. Ukiugua unarudishwa kwenu utibiwe ni Polepole style.