Kuelekea uchaguzi, vyama vya siasa viwe vitatu pekee

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
20,465
32,139
Salaam, Shalom.

Ili kudhibiti matumizi mabaya ya pesa kwenye uchaguzi, pia Ili kuhakikisha vyama vinagharimia ipasavyo wagombea wao, na Ili kuondoa ubaguzi Kwa wagombea wasio njema kiuchumi, nashauri yafuatayo;

1. Vyama vya siasa nchini viwe vitatu pekee.

2. Vyama vingine vifutwe au kuunganishwa.

3. Ruzuku itolewe Kwa vyama hivi vitatu pekee.

NB: Utitiri wa Vyama visivyoweza hata kuwa na ofisi isiyohamishika, kunaua DEMOKRASIA.

Karibuni 🙏
 
Kaka hakuna vyama hapo.

Chama gani hakijawahi kuwa na mkutano wa hadhara mahali popote nchini tangu kisajiliwe?
Wanasubiri CDM itangaze maandamano ndipo hujikusanya kupinga.

Ukiwauliza ofisi zao zilipo,

Wanakuonyesha laptop,

Kwamba ofisi ni popote!!
 
Kwanini tuhangaike na MAITI?.. vyama serious mbona vinajulikana..mapambano yawe zaidi kwenye
i.TUME HURU YA UCHAGUZI,
ii.WAGOMBEA BINAFSI
IiiKATiBA MPYA ILIYO BORA
 
Back
Top Bottom