Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

State Propaganda

JF-Expert Member
Apr 25, 2024
560
1,319
Wakati CHADEMA ikikomaa na NO REFORM, NO ELECTION, ACT WAZALENDO nao wamekuja na mpya kususia vikao vya umoja wa vyama vya siasa kwa madai kama ya CHADEMA.

CCM wao wako busy kubuni mbinu za kunasa makundi mengi ya wananchi waisapoti na kuipa kura nyingi uchaguzi mkuu. Wanabuni vikundi vya ajabuajabu kama wadudu wa Arusha, NETO, wanawake wa samia, vikundi vya walemavu, mama/baba lishe, wapaa samaki, washindilia vitunguu kwenye magunia, wajasiriamali wa aina zote, motivation speakers, ma MC, ma producer, wasanii wa fani zote, ma DJ, vikundi ni vingi na orodha ni ndefu, CCM imejipanga kwa kampeni kabambe, wanakuambia UTU NA KAZI, TUNASONGA MBELE.

Kiufupi CCM tayari wako mbele kwenye kampeni kabla muda rasmi haujaanza. Kwa hali hii hawa hata wakishinda ni halali yao kwa jinsi strategy ya kupata kura wanayoipata.
 
Ccm wakishinda ni halali yao, kwani kuna uchaguzi au maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura?
 
Wakati CHADEMA ikikomaa na NO REFORM, NO ELECTION, ACT WAZALENDO nao wamekuja na mpya kususia vikao vya umoja wa vyama vya siasa kwa madai kama ya CHADEMA.

CCM wao wako busy kubuni mbinu za kunasa makundi mengi ya wananchi waisapoti na kuipa kura nyingi uchaguzi mkuu. Wanabuni vikundi vya ajabuajabu kama wadudu wa Arusha, NETO, wanawake wa samia, vikundi vya walemavu, mama/baba lishe, wapaa samaki, washindilia vitunguu kwenye magunia, wajasiriamali wa aina zote, motivation speakers, ma MC, ma producer, wasanii wa fani zote, ma DJ, vikundi ni vingi na orodha ni ndefu, CCM imejipanga kwa kampeni kabambe, wanakuambia UTU NA KAZI, TUNASONGA MBELE.

Kiufupi CCM tayari wako mbele kwenye kampeni kabla muda rasmi haujaanza. Kwa hali hii hawa hata wakishinda ni halali yao kwa jinsi strategy ya kupata kura wanayoipata.
Unamaanisha kuwa kuna kipindi CCM walishashindwa? Na hapo wanashindana na chama gani?
Kama wananchi wanaona kuwa CCM kuendelea kushinda kwao ni neema na wanapata maendeleo watakayo basi ni jambo la kheri.

Uwezi kusema CCM watashinda kwasababu hawajawai kutaka kushindana.
 
Wahuni tu wezi wa kura hata za vitongoji.hakuna namna Tena ya kufanya uchaguzi katika nchii,ni upumbavi kabisa.
 
usisahau Kibaya[ccm]kinajitembeza na chema kinajiuza..pia sahivi msajili wa vyama kama vile hayupo sasa siku nao CHADEMA waanze kufanya haya wanaofanya Ccm utaona atakavyokurupuka kwa matamko na mabarua ya kutaka wajieleze bila kusahau vyombo vya dola hasa wale mapoti watatoa vitisho na marufuku za hapa na pale bila kusahau kamatakamata na kuwapa makesi yasiyo eleweka..mara inteljensia eti wapinzani wanaharibu amani ya nchi mara watafanya nchi isitawalike..sahivi ccm wanatamba kila kona vyombo vyote kimya sasa subiri CDM nao waanze amsha amsha utaona sarakasi za vyombo kutoka mashimoni wakitoa makaripio makali na vitisho vizito vya haja..basi inachekesha na kutia huzuni.!
 
Waache wafanye maana haya wanayopitia wapinzani wao hawayajui
 
Wenzao wanaanza kujiandaa, wao wao hawaeleweki no ELEKISHENI NO ELEKISHENI, subiri vijana wanaokuwa na expectation za kugombea wawakimbie
 
Back
Top Bottom