Kuelekea chaguzi za 2024/2025, Viongozi wa Dini timizeni majukumu yenu

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
2,626
3,141
Mimi naamini kuwa, Nchi yetu imefika hapa ilipo kutokana na viongozi wetu wa Dini kujisahau kidogo kutimiza majukumu yao vizuri kwa waamini wao.

Viongozi wa Dini tumehubiri sana Amani, Utulivu na Upendo Makanisani na Misikitini tangu tupate uhuru mpaka sasa lakini hatujafanikiwa sana kwa sababu tulisahau kwamba hivyo vyote hupatikana tu ikiwa mihimili ya Serikali itasimama vizuri.

Kupitia DP World, tumejifunza mengi sana. Tumejua rangi ya kila Mhimili, Taasisi na hata watu binafsi.

Mbaya zaidi katika Historia ya Dunia,
Ndugu zetu Wabunge ambao kwa mujibu wa Katiba wanatakiwa kuisimamia, kuishauri, kuiagiza na kuiwajibisha Serikali, wao wanaitetea Serikali kwa zaidi ya 95%. Ndo maana karibu kila Mbunge akisimama kuchangia hoja Bungeni, muda wake zaidi ya 90% unatumika kumsifu, kumpongeza, kumshukuru na kumwimbia mapambao Rais badala ya kuelezea shida za Wananchi wake.

Enough is enough.
Kwa hiyo napendekeza Viongozi wa Dini tufanye yafuatayo:-

1. Tunapoongoza ibada Makanisani na Misikitini, muda mwingi utumike kuangalia mustakabali wa Nchi na Wananchi wake ambao ndo waamini wetu.

2. Waiteni Viongozi wa Serikali na kuwaambia kuwa, uchaguzi wa 2024/2025 unatakiwa kuwa HURU na wa HAKI.

3. Marekebisho makubwa ya Katiba yafanyike mara moja ili kuendana na uchaguzi huru na wa haki.

4. Katiba iseme wazi kuwa, Mbunge/Diwani ambaye atashindwa kuisimamia, kuiagiza, kuishauri na kuiwajibisha Serikali pale inapopotoka atachukuliwa hatua gani kali.

5. Viongozi wa Dini mnatakiwa kuwa ni sehemu ya mchakato mzima wa uchaguzi wa 2024/2025 kuanzia uteuzi wa wagombea wa Ngazi zote, kampeni, siku ya uchaguzi mpaka utoaji wa matokeo( Ninyi mtakuwa Waangalizi tu)

Baada ya uchaguzi mtatakiwa kuleta Report kamili kwa waamini wenu Makanisani na Misikitini na kutoa tamko rasmi kuhusu uchaguzi husika.

Kwa kufanya hivyo, viongozi wa Dini mtakuwa mmetimiza wajibu wenu vizuri.

Ahsante.
 
Viongozi wa dini ni wanafiq,baadhi yao wakati wa magu walifiata mkia wakati huu heti ndio wasemaji hoviooo majoo yao yananuka rushwa
 
Back
Top Bottom