SoC03 Kuboreshwe uwajibikaji wa kitaasisi katika kupambana na rushwa

Stories of Change - 2023 Competition

Tonytz

Senior Member
Jul 18, 2022
159
1,142

IMG_20230706_153320_251.jpg

picha: mtandaoni@JamiiForums
UTANGULIZI.
Rushwa kwa maana iliyo nyepesi ni kitendo cha kutumia nafasi za kimadaraka na kiofisi au hadhi za kiofisi kutumia rasilimali za umma kujipatia manufaa binafsi. Rushwa inajumuisha kutoa na kupokea hongo. Kwa miongo mingi sasa rushwa imekuwa chanzo kikubwa cha kukwamisha maendeleo ya nchi nyingi barani Afrika, Tanzania ikiwemo. Uchu au tamaa ya madaraka, ukosefu wa maadili ya kazi, kukosekana kwa uzalendo miongoni mwa watendaji waliopewa dhamana, kucheleweshwa kwa maamuzi ndani ya mahakama, michakato isiyo ya lazima na ubinafsi ni miongoni mwa mambo yanayochochea ukuaji wa rushwa nchini kwetu. Baadhi ya vyanzo vya rushwa ni pamoja na uhitaji wa taarifa za siri, upendeleo kwenye huduma fulani na kuhitaji madaraka.

Ni wazi kuwa nchi yoyote ili kufikia maendeleo chanya ni lazima ithamini na kuwa na matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo. Ila kwa sehemu fulani rasilimali hizi hutumiwa na watendaji waliopewa dhamana na kuaminiwa na wananchi kwa kujipatia manufaa yao binafsi pasipo kujali mustakabali wa Taifa na raia wake. Japokuwa serikali imekuwa ikichukua hatua na jitihada kadhaa ili kukomesha rushwa, bado rushwa imekithiri katika taasisi mbalimbali za umma na zisizo za umma (binafsi). Rushwa imekithiri sana kwenye baadhi ya taasisi hasa katika kufanya maamuzi na utekelezaji wa miradi. Rushwa inazuia uwajibikaji na uwazi juu ya matumizi sahihi ya rasilimali za nchi yetu. Zaidi, rushwa huathiri sana maendeleo ya nchi kutokana na kutokuwepo na ukweli na uwazi juu ya matumizi sahihi ya rasilimali za nchi na maamuzi kinzani yanayochochewa na rushwa.

Rushwa hupelekea uvunjifu wa haki na sheria, usafirishaji wa rasilimali kihalamu, kupunguza hali ya uwekezaji nchini,kuzuia usawa katika rasilimali, kuvunja taratibu zinazoelekeza matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo, uvunjifu wa haki za binadamu na kuathiri mipango, na miradi ya kiutekelezaji kwa kuandaa mikakati finyu na baadhi ya viongozi wadhalimu.

Kukosekana kwa uwajibikaji wa kitaasisi katika kupambana na rushwa ni miongoni mwa mambo yanayochochea ukuaji wa rushwa nchini. Hii inajidhihirisha wazi kutokana na kaguzi mbalimbali zilizofanywa wa wakaguzi wakuu wa hesabu za serikali (CAG) katika vipindi tofauti tofauti.
IMG_20230706_153106_791.jpg

Chanzo cha picha:mtandao@JamiiForums

NJIA ZITAKAZOWEZESHA KULETA MABORESHO YA KIUWAJIBIKAJI KITAASISI NA KUPAMBANA NA RUSHWA NDANI YA TAASISI.

Kwa kuwa tunaona vitendo vya rushwa vimekithiri zaidi katika taasisi zetu hapa nchini, ambapo huchochewa na kutokuwa na uwajibikaji uliotukuka, ni jambo la msingi kuboresha uwajibikaji wa kitaasisi ili kukomesha vitendo vya rushwa ndani ya taasisi na jamii kwa ujumla. Hapa nitaeleza hatua kadhaa zitakazoweza kuongeza uwajibikaji wa kitaasisi katika kupambana na rushwa ili kuongeza wigo mpana wa kufikia maendeleo endelevu;

Kwanza, kukuza na kuendeleza utamaduni wa ushiriki hai wa raia katika michakato ya kufanya maamuzi ndani ya taasisi. Kwa mfano kushirikisha vyombo vya habari, asasi za kiraia na wadau katika kufatilia na kuripoti vitendo vya rushwa. Uchunguzi shirikishi huo unaweza kuongeza uwajibikaji katika taasisi ili kupambana vitendo vya rushwa.

Pili, kufanyika kwa ukaguzi wa ndani kwa taasisi mara kwa mara na kuchukua hatua stahiki kwa wanaojihusisha na vitendo vya rushwa mara wanapobainika. Hapa ni pamoja na kuwachukulia hatua za haraka wanaobainishwa kwenye ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali. Kwa kuimarisha udhibiti huo kwa njia ya ukaguzi wa mara kwa mara kutaongeza uwajibikaji katika kupambana na rushwa ili kuongeza wigo wa maendeleo endelevu hapa mchini.

Tatu, kuanzishwa kwa kamati hai za kimaadili ndani ya taasisi zote. Kamati hizi zinaweza kusaidia kurekebisha tabia na kuongeza uzalendo miongoni mwa watendaji ndani ya taasisi.

Nne, kutoa mafunzo ya mara kwa mara na program za kuwajengea uwezo maafisa wa umma. Ni muhimu kuwepo na mafunzo endelevu kwa watendaji katika taasisi ili kuongeza uwajibikaji katika kupambana na rushwa. Mafunzo hayo yajikite Zaidi kufundisha maadili na njia stahiki za kuzuia rushwa na kuchunguza rushwa. Kuimarishwa kwa ujuzi huo kunajenga taasisi na jamii yenye kuwajibika.

Tano, wahenga walisema kuwa”kidole kimoja hakivunji chawa” na” umoja ni nguvu utengano ni dhaifu” methali hizi zimejikita katika kuhimiza ushirikiano katika utendaji na maamuzi. Kukuza ushirikiano wa kimataifa na kitaifa kutasaidia kubadilishana mbinu na maarifa ya kupambana na rushwa. Kushirikishwa katika mikataba ya kimataifa ya kupambana na rushwa na mipango kutasaidia kubadili mitazamo hasi na kuongeza uwajibikaji katika kupambana na rushwa ili kufikia maendeleo endelevu.

Sita, kuwepo na ulinzi wa mtoa taarifa. Jukumu la kupambana na rushwa ndani nan je ya taasisi ni jukumu la kila mmoja. Uwepo na ulinzi kwa watu wanaotoa taarifa juu ya vitendo vya rushwa kutaongeza uwajibikaji katika kupambana na rushwa. Kwa kuweka usiri, kutoa ulinzi wa kisheria, na kutoa motisha kwa kuripoti rushwa. Kuna Watanzania wengi ambao pengine wanaviona vitendo vya rushwa ndani ya taasisi au nje ya taasisi lakini kwa kuhofia mustakabali wao, huogopa kutoa taarifa. Hivyo kuundwe mbinu thabiti za kuwalinda watoa taarifa kwa kusudi la kuongeza uwajibikaji katika kupambana na rushwa.

Saba, kutekelezwa kwa hatua za kukuza uwazi na ukweli katika taasisi. Miongoni mwa mambo yanayokuza rushwa ndani na nje ya taasisi ni kukosekana kwa uwazi na ukweli juu ya maamuzi na utekelezaji. Kufichua bajeti za serikali, mikataba, kuwezesha ufikiaji rahisi wa habari kwa raia na waandishi wa habari na michakato ya ununuzi ni miongoni mwa hatua za kuziendeleza ili kujenga uwazi na ukweli katika utendaji kutasaidia kufichua vitendo vya rushwa na kuongeza uwajibikaji.

Nane, kuwalea mafisadi kwa kisa cha urafiki, undugu, au uhusiano wowote ule ni sumu kubwa katika kupambana na rushwa. Kama Taifa ifike wakati sasa kuimarisha mifumo ya kisheria iliyo Madhubuti katika kuwachukulia stahiki mafisadi wa nchi hii. Kucheleweshwa kwa maamuzi ya kimahakama juu ya mafisadi, hukuza rushwa. Kwa kuhakikisha mifumo huru ya mahakama katika kutoa hukumu juu ya mafisadi ni njia mojawapo ya kuongeza uwajibikaji katika kupambana na rushwa ili kuongeza wigo wa maendeleo endelevu.
IMG_20230706_152057_151.jpg

Picha: chanzo mtandao@JamiiForums

Kwa kuhitimisha ni kuwa, suala la kupambana na rushwa kunahitajika nguvu, maarifa na mitazamo mipana na yenye taswira tofauti. Kila mwanajamii ana wajibu katika kutoa taarifa juu ya vitendo vya rushwa katika jamii anamoishi ili kuongeza uwajibikaji wenye tija kwa watendaji wetu. Ripoti za wakaguzi wakuu wa hesabu za serikali juu ya mafisadi zitekelezwe haraka kwa kuwachukulia hatua stahiki waliohusika. Sambamba na hilo, kusiwepo na ucheleweshwaji wa maamuzi ya kimahakama kwa mafisadi ambao wamebainika wazi
 
View attachment 2680215
picha: mtandaoni

View attachment 2680218
Chanzo cha picha:mtandao.

View attachment 2680226
Picha: chanzo mtandao

Kwa kuhitimisha ni kuwa, suala la kupambana na rushwa kunahitajika nguvu, maarifa na mitazamo mipana na yenye taswira tofauti. Kila mwanajamii ana wajibu katika kutoa taarifa juu ya vitendo vya rushwa katika jamii anamoishi ili kuongeza uwajibikaji wenye tija kwa watendaji wetu. Ripoti za wakaguzi wakuu wa hesabu za serikali juu ya mafisadi zitekelezwe haraka kwa kuwachukulia hatua stahiki waliohusika. Sambamba na hilo, kusiwepo na ucheleweshwaji wa maamuzi ya kimahakama kwa mafisadi ambao wamebainika wazi
Taarifa tunatoa kuhusu maeneo ambayo watu wanachukua rushwa lakini hawazifanyii kazi. TAKUKURU kimebakia ni chombo kinachotumika na Serikali ku harass watu ambao hawawataki kwa sababu zao.

Halafu je ni nani anayewakagua TAKUKURU? Maana hata wao wenyewe ni wapokea RUSHWA wakubwa. Kuna wakati mtu unaona hata usiripoti kuhusu RUSHWA iliyoiona kwa kuwa unawaongezea wao kipato. Wakimkuta mtoa RUSHWA wanaishia kugawana na uchunguzi unafunikwa
 
Ni kweli,lakini tuzidi kupaza sauti.endapo kàma màoni haya yàtawafkia wengi na wahusika,basi uwajibikaji utaongezeka tu. Na hiyo takukuru kunà kujuana sana, kumkamatà mwarifu harafu unampa njia za kuepuka mikono yà Sheria ni hatari sana
 
Back
Top Bottom