eti Kubenea anajiandaa kutoa taarifa. inachekesha. nadhani angeanza kwanza kutoa taarifa ya ushahidi aliokuwa akisema ya kuwa Lowasa ni fisadi. mwandishi wa habari za kiuchunguzi enzi hizo kabla ajajivua gamba na kukumbatia ufisadi. pyuuuuu! ! nani anapoteza muda wake kumsikiliza kanjanja huyu.SAED Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema) amepanga kutoa taarifa itakayowagusa viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli na Jeshi la Polisi, anaandika Faki Sosi.
Kwenye taarifa hiyo pia ataeleza taarifa za kukamatwa kwake zilizothibitishwa na Simon Siro, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
Taarifa kwenye vyombo vya habari jana zilieleza kwamba, Kubenea ni miongoni mwa waliokamatwa na Jeshi la Polisi ambapo Kamanda Siro alidai kukamatwa kwake.
Taarifa kutoka ndani ya Chadema zinaeleza kuwa, anatarajia kutoa taarifa kwa umma wakati wowote kueleza kile kinachoitwa sakata la polisi, madiwani na wabunge wa Ukawa wakati wa vurugu za uchaguzi wa meya ulioghairisha Jumamosi wiki iliyopita.
Taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa juu wa Ukawa inaeleza kuwa, Kubenea anatarajia kutoa taarifa ili kutoa ufafanuzi wa ndani kuhusu tukio hilo.
“Kubenea atatoa taarifa muda wowote kuanzia sasa, kwa kuongea moja kwa moja na waandishi wa habari, ama kutoa taarifa kwa vyombo vya habari,” amesema
Source.
Kubenea aishiwa uvumilivu
tuliuliza Kubenea tuambie kiwango chako cha elimu, tuliishia kujibiwa kuwa alisema elimu ya hapa na pale. haijulikani alisoma wapi na mpaka darasa gani. !! hakuna rekodi katika mashule zinazoonyesha habari hii na yeye mwwnyewe hakumbuki alisoma wapi! !! HILI SASA NAAMINI NI JIPU UCHUNGU