Kosa la Rais Samia ambalo watanzania wengi hawalitaki ni hili

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,641
52,458
Habari Wakuu!

Kwanza ijue nchi yako, waelewe Watu wako. Ifahamu jamii yako.

Sisi ni jamii ambayo mtu ukifanikiwa utaitwa ni Freemasonry,
Tupo kwenye jamii ambayo ukiwa na utajiri unaitwa Fisadi, Jizi au muuza madawa ya kulevya.
Tupo kwenye jamii ambayo ukimiliki vimiradi kadhaa au biashara za hapa na pale unaitwa unatumia Uchawi wa ngende. Ielewe jamii yako na watu wake.

Fanya vyovyote utakavyofanya, TOA jasho lako utakalotoa lakini elewa kuwa siku utakayofanikiwa watanzania wengi watakuweka kwenye mojawapo ya makundi hayo hapo juu.

Kwa kweli Taikon Master tangu nimezaliwa mpaka umri nilionao sijawahi kumuona Tajiri au mtu aliyefanikiwa hapa nchini ambaye Watu wanasema amepata Pesa kihalali. Hiyo sijawahi kusikia. Itakuwa mara yangu ya Kwanza na ambayo nitaiandika kwenye kumbukumbu zangu na pengine kuandika kitabu cha huyo mtu ambaye Watu watamsema amepata Mafanikio yake Kwa halali.

Leo sitaki kuwasumbua Sana,
Mama Samia kosa alilofanya ni Kutumia Ile Kanuni ya kila MTU ale urefu wa kamba yake. Kauli ambayo watanzania hawatakuja kuitaka Kwa sababu watanzania ni jamii ya kijamaa. Watu ambao wanataka kula kamba Kwa kushirikiana.

Watanzania wanavutiwa zaidi na viongozi ambao wanataka kuwafanya Watu wote kuwa Sawa ndani ya jamii. Yaani matajiri na Maskini wote wawe Sawa. Wavivu na wachapakazi wawe Sawa. Wenye bahati na wasio na bahati wawe sawasawa. Hilo Kwa Samia halipo, hiyo sio falsafa yake. Hapo ndipo anapopishana na upendo wa watanzania.

Samia anatumia Ile falsafa ya Yesu isemayo kila MTU abebe msalaba wake. Kila mtu ajikune pale mkono wake unapofikia.

Samia hawezi kumshusha wa juu ili afanane nawa Chini. Hiyo sio falsafa yake. WA Chini akitaka kwenda juu apambane kivyake vyake. Wakati vivyohivyo.

Wenye bahati wabaki wenye bahati Yao mpaka bahati Yao itakapokwisha. Wasio na bahati waendelee kuhenyeka mpaka bahati Yao utakapokuja yenyewe au Kwa wao kuitafuta.

Watanzania kama jamii hainaga Tabia ya ku- appreciate uwezo wa waliofanikiwa. Hata hapo kwenu wewe ukifanikiwa bado watakuona kama aidha umebahatisha, huna uwezo, au umetumia ndumba, au umebebwa bebwa.

Samia hiyo falsafa yake hawezi kutoboa kwenye mioyo ya Watanzania. Na sidhani kama yeye ni wale Watu wanaotafuta kupendwa au kulazimisha kukubalika.

Eeeh! Acha nipumzike tuu.

Ijumaa Kareem
 
Tatizo upigaji kwa wachache umeongezeka, huku maisha ya wengi yakiendelea kudidimia. Katika hili, ajiandae tu kusikia kelele kutoka kila kona ya nchi.

Kelele haziwezi kuzidi zile za jpm.
 
Kula usawa wa Kamba manake nini?

Kwani kabla yake watz walikuwa wanagawana vipato?

Au kula usawa wa kamba unaongelea ubadhirifu wa mali za ummma?

Nchi yeyote kaz ya serikal ni kuangalia watu wa chini, hivi Kuna faida gani ya kuendesha mgari wa mil 500 kwenye barabara zenye mashimo?

Au kuwa na big life alafu nchi yako haiwez kukutibu pneumonia?

Akili mtu wangu.
 
Kila MTU ale urefu wa kamba yake ni kauli ya kifasihi. Mtu yeyote anaweza kuifasiri anavyoweza au anavyotaka na asipelekwe wala kufanywa chochote
 
Wala si kauli ya kifasihi bali ni msemo wa mtaani wenye kumaanisha kuwa Kila mtu atafanya uhalifu Kwa kadri ya nafasi yake aliyo nayo kwenye jamii.

Huu si msemo mpya na wala usitafute kuupa tafsiri mpya.
 
Hiyo ni Fasihi.
Hizo kauli za mitaani ni sehemu ya Fasihi.
Ndio maana kuna rejesta na misimu.

Misemo ya kifasihi maana zake zinatokana na MTU
 
Kula usawa wa Kamba manake nini?

Kwani kabla yake watz walikuwa wanagawana vipato?

Au kula usawa wa kamba unaongelea ubadhirifu wa mali za ummma?

Nchi yeyote kaz ya serikal ni kuangalia watu wa chini, hivi Kuna faida gani ya kuendesha mgari wa mil 500 kwenye barabara zenye mashimo?

Au kuwa na big life alafu nchi yako haiwez kukutibu pneumonia?

Akili mtu wangu.
Serikali ipo kwa ajili ya watu wote na sio masikini tu.
 
Habari Wakuu!

Kwanza ijue nchi yako, waelewe Watu wako. Ifahamu jamii yako.

Sisi ni jamii ambayo mtu ukifanikiwa utaitwa ni Freemasonry,
Tupo kwenye jamii ambayo ukiwa na utajiri unaitwa Fisadi, Jizi au muuza madawa ya kulevya.
Tupo kwenye jamii ambayo ukimiliki vimiradi kadhaa au biashara za hapa na pale unaitwa unatumia Uchawi wa ngende.
Ielewe jamii yako na watu wake.

Fanya vyovyote utakavyofanya, TOA jasho lako utakalotoa lakini elewa kuwa siku utakayofanikiwa watanzania wengi watakuweka kwenye mojawapo ya makundi hayo hapo juu.

Kwa kweli Taikon Master tangu nimezaliwa mpaka umri nilionao sijawahi kumuona Tajiri au mtu aliyefanikiwa hapa nchini ambaye Watu wanasema amepata Pesa kihalali. Hiyo sijawahi kusikia. Itakuwa mara yangu ya Kwanza na ambayo nitaiandika kwenye kumbukumbu zangu na pengine kuandika kitabu cha huyo mtu ambaye Watu watamsema amepata Mafanikio yake Kwa halali.

Leo sitaki kuwasumbua Sana,
Mama Samia kosa alilofanya ni Kutumia Ile Kanuni ya kila MTU ale urefu wa kamba yake. Kauli ambayo watanzania hawatakuja kuitaka Kwa sababu watanzania ni jamii ya kijamaa. Watu ambao wanataka kula kamba Kwa kushirikiana.

Watanzania wanavutiwa zaidi na viongozi ambao wanataka kuwafanya Watu wote kuwa Sawa ndani ya jamii. Yaani matajiri na Maskini wote wawe Sawa. Wavivu na wachapakazi wawe Sawa. Wenye bahati na wasio na bahati wawe sawasawa. Hilo Kwa Samia halipo, hiyo sio falsafa yake. Hapo ndipo anapopishana na upendo wa watanzania.

Samia anatumia Ile falsafa ya Yesu isemayo kila MTU abebe msalaba wake. Kila mtu ajikune pale mkono wake unapofikia.

Samia hawezi kumshusha wa juu ili afanane nawa Chini. Hiyo sio falsafa yake. WA Chini akitaka kwenda juu apambane kivyake vyake. Wakati vivyohivyo.

Wenye bahati wabaki wenye bahati Yao mpaka bahati Yao itakapokwisha. Wasio na bahati waendelee kuhenyeka mpaka bahati Yao utakapokuja yenyewe au Kwa wao kuitafuta.

Watanzania kama jamii hainaga Tabia ya ku- appreciate uwezo wa waliofanikiwa. Hata hapo kwenu wewe ukifanikiwa bado watakuona kama aidha umebahatisha, huna uwezo, au umetumia ndumba, au umebebwa bebwa.

Samia hiyo falsafa yake hawezi kutoboa kwenye mioyo ya Watanzania. Na sidhani kama yeye ni wale Watu wanaotafuta kupendwa au kulazimisha kukubalika.

Eeeh! Acha nipumzike tuu.

Ijumaa Kareem
Kumbe eeh
 
Sisi ni jamii ambayo mtu ukifanikiwa utaitwa ni Freemasonry,
Tupo kwenye jamii ambayo ukiwa na utajiri unaitwa Fisadi, Jizi au muuza madawa ya kulevya.
Tupo kwenye jamii ambayo ukimiliki vimiradi kadhaa au biashara za hapa na pale unaitwa unatumia Uchawi wa ngende.
Ielewe jamii yako na watu wake.
Kama unadhani kumiliki mali nyingi ni kazi rahisi basi inaonekana na wewe utakuwa maskini tu.

There is always behind bussness nyuma ya utajiri Mkubwa.

Sio utajiri wa kuuza duka na kuuza Nyanya kariakoo
 
Back
Top Bottom