Ciprofloxacin.
JF-Expert Member
- Apr 15, 2015
- 1,583
- 2,702
Kuna tofauti kubwa sana Kati ya maisha ya Marekani na Tanzania, wala usijipe moyo, wewe unakula vyakula ambavyo mara sana siyo chaguo lako, wakati Marekani 80% ya wananchi wanakula wanachokitaka ,wanavaa nguo original wewe unavaa feki, wengi wao wana ajira na akiba ya pesa sisi Tanzania hatuna, tangu umezaliwa hata chui hujawahi kumwona na chui wapo ktk hifadhi kibao ndani ya nchi yako lakini pesa ya utalii kwenda huna, yote inaishia kwenye matibabu na ada za Shule za watoto. wakati wamarekani kila mwaka wanajazana Tanzania mamia kwa mamia na kwenda kutalii, wana bima za uhakika za matibabu wewe Kama unayo basi haizidi sh laki mbili na haitoshi lolote Kama una ugonjwa mkubwa, Kwa hiyo tofauti ipo kubwa sana acha kujipa moyo.Marekani kuna kitu gani cha ajabu hasaa, ambacho kinifanye niiache nchi yangu niende huko...ninachokula mie ndicho wanakula wao,,nachovaa mie ndicho wanachovaa wao,,kitu gani ninapungukiwa, hali ya hewa tuliyonayo ni nzuri tunashukuru Mungu