Ukitaka kuchukiwa na mjinga mwambie ukwel....
Eddo hajui mpira! Unapowaponda wachezaji na kuwaita WAVULANA, maana yake ni dharau na udhalilishaji kwao. Ndiyo simba inamapungufu makubwa safu ya ushambuliaji,lakini kwangu ndiyo timu bora kwasasa Nchini. Hao Yanga kama si Nguvu ya marefa mwaka huu wasingechukua ubingwa. Alipaswa kuchambua kama mwandishi makini na si kejeli za jinsi hiyo. Hao wavulana tunawategemea sana kwenye timu yetu ya Taifa. Hakupaswa kuwakejeli as if yanga ni bora,wakati tunaona bila mabadiliko mechi za kwanza tu yanga ataaga mashindano.
Maestro ndo mchambuzi mbovu kabisa kuwahi kutokea tz.....Mleta mada jichunguze kauli yako ya kumponda Maestro. Huyo kacheza ligi kuu na timu ya Simba na amepitia kozi za ukocha. Wewe wapondee Edo Kumwembe na Hajji Manara hao hawajacheza mpira wa ushindani kwa kiwango cha juu.
Nlitaka kuongea lakini umemaliza kila kitu mkuu, ukweli Wabongo wengi hatupendi kukosolewa na kusahihishwaGame ya Ajax vs Man Utd pundits walikuwa wanaiita ni boys against Men. Na ni kweli ilikuwa wavulana dhidi ya wanaume.
Edo anaweza kuwa hajawahi kucheza hata chandimu, lakini kwa mtu ambaye hajui historia yake ukimwambia hivyo hawezi kukuamini kwasababu pamoja na kutokujua amekuwa akitoa soccer consultancy nzuri sana.
Tuwe wawazi, mimi ni mshabiki wa Simba damu damu, jamaa wanaomponda sana ni mashabiki wenzangu wa Simba kwa kuwa tu kazungumzia mapungufu ya timu yetu. Ulikuwa ni ushauri tena katumia lugha nzuri sana, ila kwa kuwa sisi mashabiki akili zetu zote katushikia Manara basi imekuwa tatizo. Kwani uongo kuwa kwenye timu yetu kuna vivulana? Maana kama wangekuwa wanaume tungekuwa tulishamaliza ligi kabla ya ligi yenyewe kuisha.
Tukubali kushaurika. Waungwana ni wale ambao hukubali mapungufu yao na kuyafanyia kazi ili kuleta mafanikio zaidi. Ni kweli kuwa tuna striker wazuri, ila hatuna wauaji pale mbele. Hatuna commanding midfielder, beki yetu ya kati iko vizuri lakini ni vizuri tukianza kutafuta mtu wa kumrith maana kiukweli ukiachilia umri wa kwenye passport yake ana umri wake wa ziada.
Tukubali kushaulika kama kweli tunataka kuwa contestant wa ukweli ndani na nje ya nchi.
Wewe Sio shafii dauda kweli?Maestro ndo mchambuzi mbovu kabisa kuwahi kutokea tz.....
kwani uongo!?Amekurupuka usingizini,