Klabu ya West Ham yachukua mchezaji MAN UTD

Mributz

Senior Member
Aug 29, 2022
167
516
Klabu ya West Ham imekamilisha usajili wa beki wa kulia, Aaron Wan-Bissaka kutoka klabu ya Manchester United kwa mkataba hadi Juni 2029.

Aaron Wan-Bissaka mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na klabu ya Manchester United Juni mwaka 2019 akitokea klabu ya Crystal Palace.

Alicheza mechi yake ya kwanza ya akiwa na jezi ya United mnamo Agosti 2019, akisaidia kikosi cha aliyekuwa kocha wa kipindi hiko, Ole Gunnar Solskjaer kupata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Chelsea.

Katika klabu ya United nyota huyo amecheza jumla ya mechi 190 amefunga mabao mawili na kutoa asisti 13 na ameshinda makombe mawili, Kombe la FA 2024 na Kombe la Ligi 2023.

𝐇𝐄𝐑𝐄-𝐖𝐄-π†πŽ-west-ham-agree-deal-to-sign-aaron-wan-bissaka-v0-j2wxj0bj7uhd1.png
 
Jamaa kumpita ni kazi kidogo, mzuri sana kwenye tackling ila kushambulia si mzuri saana, haswa sector ya kumwaga maji.
 
Back
Top Bottom