Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 4,545
- 7,745
Klabu ya Vipers SC ya nchini Uganda imemzawadia Mtoto Jamal Ssenyondwa aliyetokwa na Machozi katika uwanja wa Nakivubo wakati Vipers ilipopigwa goli la pili na klabu ya Express United na kufanya Mechi kuwa 2-1 katika dakika ya 90+3 kisha akaonekana kushangilia kwa furaha baada ya Vipers kurudisha goli hilo katika dakika ya 90+4 na kupata sare muhimu ya 2-2.
Jamal alialikwa kwenye chumba cha kubadilisha nguo cha Vipers, akapewa Jezi , pamoja na tiketi za Msimu wote za daraja ya VVIP.
Ila kubwa zaidi ni kutoa ahadi ya kusomeshwa bure na klabu hiyo katika moja ya shule zinakuza vipaji Afrika Mashariki shule ya St. Mary's Kitende ya huko Uganda.
Vipers wamepata shabiki damu damu wa milele.