Kiwango cha uzalishaji wa dhahabu kupitia barrick kimepungua!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
36,086
29,652
Vyombo vya taarifa duniani vinaeleza kuwa kampuni ya barrick imeathirika katika uzalishaji au uuzaji wa dhahabu duniani...na moja ya sababu inaweza kuwa ni mgogoro kati ya Tanzania na kampuni ya barrick/acacia.

Kwangu mimi hii inamaanisha[B/] umuhimu mkubwa wa migodi yetu katika kutoa dhahabu ingawa kipato tulichokuwa tunapata kilikuwa ni kiduchu mno.

Zuio la mchanga wa makanikia lina athari kubwa kwa kampuni hii ...ina maana kampuni ilikuwa ikinufaika haswa na madini yetu.

Zuio hili ni muhimu kwa kuwa hapo mwanzo tulikuwa hatupati kitu ilihali mchango wa uzalishaji wa dhahabu ulikuwa ni significant to Barrick and the world.

Way foward:
Barrick kuendelea kuhonor makubaluano ya awali ili iendelee kusimama kwenye soko la dhahabu duniani.

Barrick kuharakisha suluhisho la tatizo ili iweze kusimama tena kama muuzaji au mfanyabiashara mkuu wa dhahabu duniani.

Serikali ya Tanzania iendelee kusimamia kucha na ikiwezekana itoe ultmatum ya usuluhu wa issue ya makanikia.

Bado naiamini tume ya makanikia na tume ya majadiliano ingawa Mheshimiwa Rais anatakiwa kuendelea kuifuatilia kwa ukaribu wa kipekee ili isihongwe au kurubuniwa.

Watanzania wanatakiwa waendelee kuwapuuza vibaraka mfano wa Pasco ambao wanaweza kununuliwa muda wowote na wakaanzisha threads zisizo na mashiko zenye kuulizia mambo yaliyotolewa ufafanuzi!

This battle is hard but Tanzania and Magufuli will prevail as winners.

Barrick just makes 2017 production guidance | MINING.com
 
Tulidhani una hoja, kumbe umekuja kipropaganda kumjibu Paskali!! Tunamuomba Paskali aendelee kumwaga mambo makubwa hivi hivi, ikibidi aanzishe mada ya hii miaka 7 madarakani. Tupe updates ya vile viwanda 100 kila mkoa.
Vyerehani vimeshashuka vya kutosha...
 
Tulidhani una hoja, kumbe umekuja kipropaganda kumjibu Paskali!! Tunamuomba Paskali aendelee kumwaga mambo makubwa hivi hivi, ikibidi aanzishe mada ya hii miaka 7 madarakani. Tupe updates ya vile viwanda 100 kila mkoa.
mkuu usitake kuchanganya mada let us stay on the topic..tunaongelea dhahabu na sakata la madini nchini.

mengineyo tuyajadili sehemu husika
 
Vyombo vya taarifa duniani vinaeleza kuwa kampuni ya barrick imeathirika katika uzalishaji au uuzaji wa dhahabu duniani...na moja ya sababu inaweza kuwa ni mgogoro kati ya Tanzania na kampuni ya barrick/acacia.

Kwangu mimi hii inamaanisha[B/] umuhimu mkubwa wa migodi yetu katika kutoa dhahabu ingawa kipato tulichokuwa tunapata kilikuwa ni kiduchu mno.

Zuio la mchanga wa makanikia lina athari kubwa kwa kampuni hii ...ina maana kampuni ilikuwa ikinufaika haswa na madini yetu.

Zuio hili ni muhimu kwa kuwa hapo mwanzo tulikuwa hatupati kitu ilihali mchango wa uzalishaji wa dhahabu ulikuwa ni significant to Barrick and the world.

Way foward:
Barrick kuendelea kuhonor makubaluano ya awali ili iendelee kusimama kwenye soko la dhahabu duniani.

Barrick kuharakisha suluhisho la tatizo ili iweze kusimama tena kama muuzaji au mfanyabiashara mkuu wa dhahabu duniani.

Serikali ya Tanzania iendelee kusimamia kucha na ikiwezekana itoe ultmatum ya usuluhu wa issue ya makanikia.

Bado naiamini tume ya makanikia na tume ya majadiliano ingawa Mheshimiwa Rais anatakiwa kuendelea kuifuatilia kwa ukaribu wa kipekee ili isihongwe au kurubuniwa.

Watanzania wanatakiwa waendelee kuwapuuza vibaraka mfano wa Pasco ambao wanaweza kununuliwa muda wowote na wakaanzisha threads zisizo na mashiko zenye kuulizia mambo yaliyotolewa ufafanuzi!

This battle is hard but Tanzania and Magufuli will prevail as winners.

Barrick just makes 2017 production guidance | MINING.com

Lakini zile dola milioni mia 300 tulizoambiwa tutalipwa zimeshalipwa ? Usisahau kuwa Noah zetu hatujazipata bado
 
mkuu usitake kuchanganya mada let us stay on the topic..tunaongelea dhahabu na sakata la madini nchini.

mengineyo tuyajadili sehemu husika

Ukituletea mada ya propaganda tutakujibu tunavyotaka na tutakurudisha kwenye mada zenye tija na sio hii propaganda mfu yako.
 
Lakini zile dola milioni mia 300 tulizoambiwa tutalipwa zimeshalipwa ? Usisahau kuwa Noah zetu hatujazipata bado
malipo ya fedha kulingana na mazungumzo yaliyofanyika yaliahidiwa na Barrick Team
...na tuliambiwa yatajadiliwa ...na jibu muhimu litatoka in 6 months of 2018...unapouliza leo unatarajia jibu gani?
 
Ukituletea mada ya propaganda tutakujibu tunavyotaka na tutakurudisha kwenye mada zenye tija na sio hii propaganda mfu yako.
napenda sana mtu aneyefuatilia mada kwa facts..sio propaganda!
 
Ungekuja na facts usingepaswa kumchafua Paskali kwa kumuita anaweza kuhongwa wakati wowote. Ile ni kumchafua kwakuwa jana kaleta mada iliyokukera wewe na unaojipendekeza kwao. Facts zako hazikupaswa kuchanganywa kwa kuchafua mtu. Matokeo yake tumeona sio facts bali ni uzandiki tu kama uzandiki mwingine. Jitahidi unapoleta facts usichanganye na siasa chafu ili mada yako iheshimike.
 
Mwenzio yupo kazini hapo LB7.
 
Ungekuja na facts usingepaswa kumchagua Paskali kwa kumuita anaweza kuhongwa wakati wowote. Ile ni kumchafua kwakuwa jana kaleta mada iliyokukera wewe na unaojipendekeza kwako. Facts zako hazikupaswa kuchanganywa kwa kuchafua mtu. Matokeo yake tumeona sio facts bali ni uzandiki tu kama uzandiki mwingine. Jitahidi unapoleta facts usichanganye na siasa chafu ili mada yako iheshimike.
Keep your concentration on facts! utaelimika na utaelewa.
mada ya pasco ni ya kijinga sana kwa kuwa iliulizia au kuelezea yaliyofafanuliwa na yaliyojiri.
Barrick walikubaliana na Serikali...kilichobaki ni baraka za kampuni kuhusu makubaluano hayo na kulingana na taarifa au majadirida mbalimbali suala hilo lilihitaji baraka za bodi ya barrick ambayo ingeketi na kuamua ndani ya miezi 6 ya mwaka huu.

Kwa nini uibuke leo na kushutumu kwamba mambo hayatokei wakati tuna muda hadi juni 2018?
Sitegemei kama mwanahabari na mfuatilliaji kama pasco ashindwe kujua facts za namna hii zaidi ya kupewa bahasha na kununuliwa...

ninamjibu kwa thread hii ili ajue tunafuatilia kwa undani ikiwa na pamoja na wale wote wanaonunuliwa!
 
Keep your concentration on facts! utaelimika na utaelewa.
mada ya pasco ni ya kijinga sana kwa kuwa iliulizia au kuelezea yaliyofafanuliwa na yaliyojiri.
Barrick walikubaliana na Serikali...kilichobaki ni baraka za kampuni kuhusu makubaluano hayo na kulingana na taarifa au majadirida mbalimbali suala hilo lilihitaji baraka za bodi ya barrick ambayo ingeketi na kuamua ndani ya miezi 6 ya mwaka huu.

Kwa nini uibuke leo na kushutumu kwamba mambo hayatokei wakati tuna muda hadi juni 2018?
Sitegemei kama mwanahabari na mfuatilliaji kama pasco ashindwe kujua facts za namna hii zaidi ya kupewa bahasha na kununuliwa...

ninamjibu kwa thread hii ili ajue tunafuatilia kwa undani ikiwa na wale wote wanaonunuliwa!

Hapo kwenye nyekundu kama muda wa kulipwa ulikuwa ndani ya miezi sita, je toka kikao kilipoisha mpaka hiyo june bado itakuwa ni miezi sita? Halafu walisema ni mpaka miezi sita iliyojaa au ni ndani ya miezi sita? Unasema mada ya Pasco ni ya kijinga sana kwa sababu haiendani na utashi wako na waliokutuma. Sisi wengine tuliumelewa Pasco kwakuwa hakuja na hizi hadithi zako. Hili suala tunaona utata mwingi, na hata utekelezaji wake ni kuchanganya sana. Kuna watu walitajwa kwa majina kuhusu mikataba ile mibovu na rais akaagiza wakamatwe na uchunguzi dhidi yao uanze. Watu hao ni Chenge, Karamagi, Yona nk. Mpaka leo hawajamatwa wala kuchukuliwa hatua yoyote. Je hawa nao wanasubiri hiyo miezi sita hatua dhidi yao ianze? Kama hili la kuwawajibisha watu wetu limetushinda tutaamini vipi kwamba hao Barrick watalipa wakati wameonyesha kabisa watalipa kwa mapenzi yao? Ni kwanini zile 450Tr tulizoaminishwa hiyo kamati ya Kabudi ilishindwa kuidhibitisha?

Hukuna yoyote anayelipwa wala kununuliwa kwani hayo makampuni sio kwamba yameingia hapa nchini baada ya awamu hii kuingia madarakani bali wana miaka kibao. Kama kuna mahali Paskali alisaini mikataba na hao jamaa iweke hapa tuone. Na kama kuna nia njema kwanini hiyo mikataba mibovu haipelekwi bungeni tujue kilichomo humo ndani? Kama mnafanya jambo kwa maslahi ya umma iweje kuwe na kificho na uhasama kwa watu wanaohoji kama akina Paskali? Kuna tofauti gani na awamu zilizopita kwa kuficha hiyo mikataba?
 
...Kuna watu walitajwa kwa majina kuhusu mikataba ile mibovu na rais akaagiza wakamatwe na uchunguzi dhidi yao uanze. Watu hao ni Chenge, Karamagi, Yona nk. Mpaka leo hawajamatwa wala kuchukuliwa hatua yoyote...
Tusubiri mkombozi lowasa akiingia ikulu atukamatie majangiri haya.
 
Nani, kwa mtazamo wako, anayeweza kuwakamata?!

Mimi na wazalendo wa kweli ambao hatukuwahi kuwa katika serekali zilizoingia hiyo mikataba mibovu. Yeyote ambaye alikuwa madarakani wakati hiyo mikataba mibovu inaingiwa naye ni mchafu kama hao waliotajwa hivyo hana uwezo wa kuwafanya lolote zaidi ya kupiga kelele.
 
Back
Top Bottom