Kiwanda cha General Tyre cha Arusha kufunguliwa

Si ungi mkono kufufuliwa kwa General tyre kwa mfumo ulele uliyoifanya ife hii ni upotevu wa fedha za umma fedha hizo zingeweza kuwasaidia wa mama wanonaolala mzungu wa nne hospital ya Temeke wakati wa kujifungua.

============

Mjadala wenye tija na uchambuzi kuhusu kiwanda cha matairi cha General Tyres uliofanyika hapa JF na pengine kuchochea Serikali kukifufua kiwanda hicho upo kwenye uzi huu; General Tyres Tanzania ilivyohamishiwa Kenya na kuitwa YANA tyres! [/SIZE][/QUOTE]
 
Tatizo lililoko GT ni ushindani ulioko sasa hivi kwenye soko la tairi, ili kiwanda kiweze kujiendesha lazima uuze bidhaa bora na kwa bei ya ushindani hii ndiyo changamoto hata kampuni ya samir tyres ya Kenya ilikutananae hata baada ya moi kuzuia kwa muda tairi kutoka nje alivyo ingia kibaki mambo yakawa magumu tena,kwanza kipindi cha nyuma GT ilkua inapata mpira kutoka mashamba ya mpira nchini kwa bei nafuu leo mashamba yamebinafsishwa,hivyo itabidi uanze kuagiza mpira nje,halafu ushindane na hao wenye kukuuzia mpira kwenye soko la Tairi,wenye Viwanda karne ya 21 wamejipanga kuanzia upatikanaji wa malighafi kwa bei nafuu ili waweze kushika soko, ndiyo maana Dangote yuko mtwara mahali penye gesi na choka na malighafi mengine leo hii makampuni makubwa ya tyre zimejenga Viwanda vya matairi china na Vietnam siyo bure wanafuata malighafi,kwa hiyo Kama atafufua anaweza, lakini je litadumu muda gani?

Tatizo lingine ni kiwanda kiko Arusha wakati 70% ya soko liko Dar na mali ghafi yote 90% inapitia bandarini. Kiwanda kilijengwa Arusha ili kukidhi mahitaji ya Afrika mashariki lakini Kenya walipojenga Firestone ndipo mwanzo wa kifo cha GT ulipoanza. Kiwanda hakiwezi fufuka bila kuwa na mbia atayeleta vinu vyake. Itachukua muda mrefu sana kabla hakijaanza kufanya kazi. Hii yote ni siasa tu kujaribu kupata kura za watu wa Arusha.
 
CCM lazima waondoke kukifunga hicho kiwanda bila sababu za msingi kuliathiri familia nyingi sana, wafanyakazi walikufa kwa msongo wa mawazo, wengine walishindwa kusomesha watoto, wengine ndoa zilivunjika yte haya kwa sababu ya dhuluma waliyofanyiwa na serikali ya ccm, haya yaliyotekea hayarekebishiki majeraha ni makubwa sana hapa hamdangayi mtu. Mtaondoka tu.
 
General tyre kufufuliwa, JF nayo tupongezwe..

=============


============

Mjadala wenye tija na uchambuzi kuhusu kiwanda cha matairi cha General Tyres uliofanyika hapa JF na pengine kuchochea Serikali kukifufua kiwanda hicho upo kwenye uzi huu; General Tyres Tanzania ilivyohamishiwa Kenya na kuitwa YANA tyres!
hivi mkiwaza kitu kichwani kwako unahamka na uzushi halafu unataka watu wenye akili timamu wakubali uzushi?
1.yana tyres ilikuwa inaitwa Firestone na walikuwa na mashine bora kuliko hizo za general tyre,kwa hiyo hata bure wasingezichukua.

2.kufufua siyo tatizo ila tatizo ni uuzaji wa vitu unavyozalisha,kiwanda ni kama mwili wa binadamu usipokula mwili wako hautafanyakazi(malighafi) na usipofanyia kazi uliokula (uzalishaji)utakufa na usipotoa choo utakufa (uuzaji) pia,kwa hiyo kiwanda hicho hakiwezi kuendeshwa kibiashara kwa sababu mashine ni ya zamani sana na teknolojia imebadilika sana kutoka system ya Tube hadi tubeless.
3. malighafi aliyokuwa ikipatikana hapa(mpira) mashamba yale yalibinafsish wa, hivyo hicho kiwanda inabidi kifungwe machine za kisasa halafu malighafi uagize nje kisha ushindane na wale wasioagiza malighafi.
4.kwa hiyo kiwanda itafufuliwa lakini litadumu muda gani?
 
Sio kweli. Serikali ilishatoa shilingi bilioni kumi miaka mingi iliyopita za kulipa hilo madeni na kufufua kiwanda. Mbia (Continental/General Tyre) alikuwa anadai dollar 2.4 million na HSBC walikuwa wanadai 2 million dollars. Deni likalipwa pesa iliyobaki Mramba, Shelukindo na mafisadi wenzao huko CCM wakazitia ndani kiwanda kikatelekezwa.
Mzee Shelukindo anatajwa sana kwenye hili,kama ni kweli ivi anajisikiaje kuwa sehemu ya anguko la iki kiwanda watu zaidi ya 300 kukosa ajira za moja kwa moja achilia mbali ajira zisizo za moja kwa moja.
Hasara zingine kibao kama uagizaji wa matyre kwa kutumia forex,mapato kwa inchi etc dah inauma kwa kweli
 
Kuna sehemu nimesoma kwamba Serikali ya Tz imechukua hisa 24% zilizokuwa zinamilikiwa na mwekezaji na hivyo kuhodhi 100% kwani kabla ya hapo walikuwa na 76%.

Swali ni kwamba mbona nilisikia hiyo General Tyre ilishakufa siku nyingi? Utanunuaje hisa za kampuni iliyokufa?

Labda mimi sielewi naomba kuelimishwa kwa hilo.
 
Ndio uwekezaji huo, unauza kiwanda, wawekezaji wanakiuwa halafu unachukua marehemu wako
 
kuna sehemu nimesoma kwamba serikali ya tz imechukua hisa 24% zilizokuwa zinamilikiwa na mwekezaji na hivyo kuhodhi 100% kwani kabla ya hapo walikuwa na 76%.

Swali ni kwamba mbona nilisikia hiyo general tyre ilishakufa siku nyingi? Utanunuaje hisa za kampuni iliyokufa?

Labda mimi sielewi naomba kuelimishwa kwa hilo.
porojo......
 
general tyre east africa, inatukumbusha mbali sana......na viwanda vingine pia walete kauli tusikie
 
mashine nzuri na technolojia ilishahamishiwa kenya na sasa yanatengenezwa matairi yanaitwa yana tyres so hapo ni usanii
 
Back
Top Bottom