kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,870
- 7,752
Inaelekea wanaoongoza TANESCO kwa sasa mama anawabeba kwa mbeleko kama watoto wake wa kuwazaa.
Shirika la TANESCO ni mali ya Serikali kwa asilimia 100. Sasa anapokuja huyu Maharage na waziri wake Makamba kutuambia eti madeni ya Serikali yanageuzwa hisa ndio nini maana yake?
Si bora wangesema tu serikali imesamehe madeni yake TANESCO. Tulichotegemea ni huyu maharage kuboresha usimamizi wa shirika kwenye maeneo ya utendaji, mfano kuongeza uadilifu kwa kudhibiti ubadhirifu na upigaji ili mapato ya shirika yaongezeka na sio kupotea kwa wizi na kukosekana uaminifu.
Hili la kufutiwa madeni na serikali kisha kuendeleza ubadhirifu mbele ya umma kwa kufanya eti tafrija kubwa kusoma faida inayoonekana vitabuni kwa kufutiwa madeni sio jambo la kujivunia.
Pia hii dhana ya kugeuza madeni ya serikali TANESCO isije kua kigezo cha hawa wapigaji kwa kujidai maliberali kwenye uchumi kuanza kubinafsisha tanesco maana huu uongozi wa mama umezungukwa na wapigaji na wajanja wenye kutaka kupora mali za Tanzania kwa fujo wakijua huko mbele watanzania watachagua Rais mwingine mwenye mwelekeo wa kizalendo kama Magufuli.
Wapigaji wengine wanalenga kuja kudai mabilioni kama fidia wakijua watanzania kwa desturi hawakubali uhuni.