Kituo cha Polisi Wilaya ya Butiama chajengwa kwa Tsh. Milioni 802, kukamilika Desemba 2023

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Butiama, Jumanne Sagini ameagiza kukamilika kwa wakati Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja B cha Wilaya ya Butiama Mkoani Mara, ifikapo mwezi Disemba 2023 kama ilivyoelekezwa.

Maagizo hayo ameyatoa leo Novemba 18, 2023 wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua uendelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo hicho kilichopo katika eneo la Mtuzu Kata ya Butiama Wilayani Butiama.
View attachment 2818004
Muonekano wa Jengo la Kituo cha Polisi Daraja B kinachojengwa katika eneo la Mtuzu Kata ya Butiama Wilayani Butiama Mkoani Mara Novemba 18, 2023.

View attachment 2818005
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini (Mb), akikagua uendelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja B kinachojengwa katika eneo la Mtuzu Kata ya Butiama Wilayani Butiama Mkoani Mara, leo Novemba 18, 2023.

"Nimefurahishwa na kasi ya Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Butiama, mradi huu unatekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wetu mpendwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, bila kuchoka mama huyu amemwaga fedha za kutosha hivyo basi nimtake mkandarasi kukamilisha mradi haraka bila vikwazo kwani Wananchi wana kiu kubwa ya kupata huduma karibu," alisema

Katika taarifa yake Meneja wa Mradi wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Butiama wa Kikosi cha Polisi Ujenzi, Mkandarasi SP Masiva Mfinanga alieeleza kuwa, mradi huo una thamani ya Shilingi 802,000,000 (Tsh. Milioni 802) ambapo ujenzi ulianza rasmi Mei 6, 2023 na unategemewa kukamilika mwishoni mwa mwezi Disemba 2023.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Butiama, Jumanne Sagini yupo Mkoani Mara kwa ziara yake ya kikazi ambapo atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi inayoendelea katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara hiyo.
Haleluiya
 
Taarifa zingine zimekaa kipotoshaji zaidi.

Kwamba jengo litakuwa Moja tuu?
 
Ujenzi haujakaa wa ramani ya kituo kuweza kujihami ikiwa watavamiwa na watenda maovu.

Ifike mahali vituo vya polisi viwe Standard nchi nzima kuanzia Central Polisi za Mkoa, wilaya na vituo vidogo, badala ya ujenzi holela usiozingatia kuwa viko ktk utayari wa kujihami kukitokea chochote wakisubiri msaada.
Hii Nchi Huwa Ina watu wajinga sana na wasiofikiri.

Ukiona hata majengo ya shule,zinakuja na Ramani lakini wakenzi Kila mtu anaweza anavyojiskia.

Hii tabia ni ya kipuuzi na ya kijinga , Serikali Huwa hamuoni haya?

Ndio Vituo vinajengwa kienyeji utadhani hakuna wasanifu.
 
Watakwambia wanaokoa pesa kwani pesa ya kumlipa msanifu ni ndefu sana.
 
Nimefurahishwa na kasi ya Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Butiama, mradi huu unatekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wetu mpendwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, bila kuchoka mama huyu amemwaga fedha za kutosha hivyo basi nimtake mkandarasi kukamilisha mradi haraka bila vikwazo kwani Wananchi wana kiu kubwa ya kupata huduma karibu," alisema
Mill 800+

Wamegawana hizo
 
Back
Top Bottom