KITUO cha Mabasi ya Mikoani cha Temeke kuhamishiwa Mkuranga

Mnataka kututia umaskini bila sababu; mwenda kusini anayetoka kibamba itabidi ahamie mkuranga kwa muda ili awahi bus, si hasara hiyo?
 
mkuu hizo gari za songea ili zishushe temeke zinapitia morogoro-chalinze-mlandizi-kibaha kama kawaida? kama ndo hivyo ebu nieleze baadae zinapitia wapi kwenda huko mbagala? au ubungo-mandela road?
Temeke - mkuranga- ikwirir- somanga- lindi - mnazi mmoja- masasi- tunduru - songea
 
daladala za kutoa watu mkuranga kuleta Dar hazitaleta msongamano. tena basi la watu 60 likijaza daladala tatu si msongamano utaongezeka badala ya kupungua? nielewesheni.
hata mimi hapo nimeshindwa kuelewa kwa kweli......
 
Kama wadau wengine walivyosema, Mkuranga ni wilaya na inaanzia pale mpakani na kongowe. Kwa wanaoijua st Matthews secondary, pale ilipo ni mkuranga siyo dar.
Hivyo basi, kama stand itawekwa hapo mwanzoni (siyo lazima iwe kandokando ya barabara) nadhani itakua siyo mbaya sana kwa factor ya umbali. Lakini pia kiuhalisia hiyo stand haitakuwa ya Dar tena bali itakua ya Pwani.

Kuna wengine wanasema mbagala rangi tatu panatosha, ila ukweli ni kwamba pale ni padogo sana, city busses zipo nyingi halafu ni kubwa mfano Eicher, hivyo zikiingia chache tu stand inajaa.
Gari zote zinazotoka mbagala kwenda tandika na temeke hazina kituo ila zinabanana pale njiani. Mimi naona hiki ndo chanzo kikubwa cha msongamano.
 
Back
Top Bottom