Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,828
- 13,585
Mwenyekiti wa Chadema Taifa na mwenyekiti wa TCD, Freeman Mbowe siku ya leo ameongoza uzinduzi wa ripoti ya tathmini ya hali ya demokrasia nchini kwa mwaka mmoja uliopita, iliyoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).
Tukio hilo limefanyika Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo Septemba 19, 2024 na litahitimishwa kesho Septemba 20, 2024.
Freeman Mbowe aliambatana na Makamu mwenyekiti Bara Tundu Lissu, Katibu Mkuu wa Chama, John Mnyika na viongozi wengine waandamizi wa CHADEMA.
Soma pia: Waziri Stergomena Tax ashiriki hafla ya uzinduzi wa boti ya doria katika bahari na maziwa
Katika mkutano huo Mbowe alizungumzia kuhusu sakata la utekaji linaloendelea nchini kwa kudokeza kuwa inasikitisha kuona baadhi ya viongozi wa chama hicho wakipotea kwenye mazingira ya kukutanisha.
Mbowe aliongeza kwa kusema kuwa kipindi Rais Samia anaingia madarakani, vyama vya upinzani vilianza kuona mwanga wa kurudi wa Demokrasia nchini lakini baadae mambo yalionekana kuwa tofauti.
Katika kipindi kifupi ambacho tulishaanza kuona matunda ya Demokrasia katika taifa letu kwamba kwa kiwango kikubwa uhuru wa kufanya siasa ikiwemo mikutano ya hadhara, yalifanyika nchi nzia kwa amani sana kwa ushirikiano mkubwa kati ya vyama vya siasa na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. Lakini ghafla ile stability tuliyokuwa tunaipata katika taifa haijawa endelevu.
Aidha uzinduzi wa ripoti hiyo ulihudhuriwa na balozi wa Marekani nchini Tanzania, Michael Battle pamoja na viongozi wengine kwenye balozi mbalimbali.
Aidha Waziri mkuu mstaafu, Joseph Sinde Warioba ambaye kwa upande wake alikemea ukabila pamoja na uoga wa kukosoa serikali ambao kwa sasa unawakabili viongozi na wananchi wengi Tanzania huku akivitaka vyama vya siasa hasa CHADEMA na CCM kukaa pamoja kusuluhisha mgogoro uliopo.
Mpaka jana nilikuwa najitahidi bado muda mfupi tuingie kwenye uchaguzi wa seikali za mitaa. Tafadhali viongozi wote tukubaliane. Tutakapoenda kwenye uchaguzi ule tuwe tumekubaliana. Tukienda na mapambano haya inaweza ikaleta misingi ya mapambano kote nchini.
Balozi wa Marekani Nchini Tanzania, Michael A. Battle amesisitiza kuwa Nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali na kusisitiza haitarudi nyuma katika uwazi wa masuala ya Demokrasia na Haki za Binadamu
Amesema hayo kwenye Mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kinachowakutanisha Wadau kujadili na kufanya tathmini ya hali ya Demokrasia nchini, leo Septemba 19, 2024