Kituo cha Afya Makuburi: Ulomi aliletwa hospitali na Askari

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
2,181
5,553
Salaam Wakuu,

Sakata la Ulomi linazidi kuleta taswira mpya kila siku, leo Kituo cha Afya Makuburi wanasema Ulomi aliletwa kituoni kwao na Askari, tushie lipi?

Someni wenyewe hapa chini sakata limeelezewa:

Kituo cha Afya cha Makuburi kilichopo Ubungo Jijini Dar es salaam kimesema Mfanyabiashara, Daisle Ulomi, alifikishwa kituoni hapo na Askari wa Kituo cha Polisi Makuburi ambao walimchukua eneo alipopatia ajali na kusema Ulomi alikuwa amevunjika mguu na mkono wa kushoto na pia alikuwa na majeraha kichwani huku pia ikihisiwa baadhi ya viungo vyake tumboni ikiwemo bandama na ini vilipasuka na kuvuja damu.

Akiongea kwenye mahojiano maalum na Mwandishi wa @AyoTV_, Bakari Chijumba kituoni hapo leo December 17,2024, Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dkt. Alphoncina Mbinda, amesema “Tulimpokea majeruhi (Ulomi) December 12,2024 mchana kama saa 7:30, aliletwa na Askari tukampokea tukamuhudumia, alivunjika mguu na mkono wa kushoto, aliumia kwenye paji la uso, puani, tukamuhudumia, jitihada zilifanyika lakini Mgonjwa akaanza kuwa mweupe dalili kuwa ameishiwa damu, tuliona ana dalili za kuwa amepata majeruhi ya viungo vya tumboni inawezekana organs tumboni bandama au ini zilipasuka ndio maana akazidiwa kwa haraka baada ya muda mfupi akapoteza maisha”

“Muda ambao amehudumiwa ni kati ya saa saba (alipofikishwa) hadi saa nane ina maana saa moja haikufika tangu alipofika hadi kufariki, tulishaita Ambulance apewe rufaa kwenda Mwananyamala baada ya kufariki tukawaambia Ambulance wasije tena maana gari la kubebea Wagonjwa halibebi maiti, tukatoa taarifa kwa Askari waliotuletea wakaja wakashuhudia amefariki, tukawaomba Askari tusaidiane kupeleka Mwananyamala, tukashirikiana, tukaandaa mwili, tukatoa hela kama kituo kupeleka mwili Mwananyamala kwa gari binafsi ya kukodi, alienda pamoja na Askari”

“Taarifa tulizopewa ni kwamba alikuwa akiendesha pikipiki halafu kuna lori likatokea, wakagongana, pikipiki ikaumia yote na Mgonjwa palepale akapata majeruhi(ajali imetokea maeneo ya Mandela Road karibu na Gereji na Tabata Relini), baada ya hapo waliitwa Askari ndio wakamchukua na kumleta kituoni, tunaambiwa lori lilikuwa linatoka pembeni linaingia barabara kuu yeye alikuwa barabara kuu, taarifa zaidi za ajali muwasiliane na Polisi ambao walifika eneo la tukio, tulishindwa kujua Ndugu zake kwasababu hatukuona simu yake wala wallet wala document zozote kwenye nguo zake”

Millard Ayo

PIA SOMA
- TANZIA - Mwili wa Ulomi, Mfanyabiashara aliyedaiwa kupotea wakutwa mochwari Mwananyamala

- Katibu wa Afya Hospitali ya Mwanyamala: Ulomi alipata ajali, mwili uliletwa December 11, 2024
 
Yule mzee wa kanda specific alisema alipelekwa na Wasamalia Wema.
 
Vichekesho havitaisha nchi hii; Mwananyamala wanakwambia hv;
Katibu wa Afya Mwandamizi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala, Lydia Nzema, ameiambia Ayo “December 11,2024 jioni tulipokea mwili kutoka Zahanati ya Makuburi, akiwa ameshafariki lakini Polisi kesi, ni kesi ya ajali mwili uliopatikana umepata ajali ameshafariki, ina maana alishapata kama ni matibabu au kama Kituo cha Afya alichopelekwa ilikuwa Zahanati ya Makuburi.

"Mwili ulikuwa Unknown hatukujua ni nani na tumehifadhi kwenye chumba cha maiti, leo December 16,2024 wamekuja Ndugu wameutambua mwili na wamesema ni Ndugu yao huyo Mfanyabiashara (Ulomi), kuhusu taarifa zaidi za alipata ajali gani taarifa zitakuwa mochwari zimeandikwa na taarifa zaidi Polisi wanazo.”
 
Akiongea kwenye mahojiano maalum na Mwandishi wa @AyoTV_, Bakari Chijumba kituoni hapo leo December 17,2024, Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dkt. Alphoncina Mbinda, amesema “Tulimpokea majeruhi (Ulomi) December 12,2024 mchana kama saa 7:30, aliletwa na Askari tukampokea tukamuhudumia, alivunjika mguu na mkono wa kushoto, aliumia kwenye paji la uso, puani, tukamuhudumia, jitihada zilifanyika lakini Mgonjwa akaanza kuwa mweupe dalili kuwa
Hajapangiwa cha kuongea kweli huyo?
 
Back
Top Bottom