Kitkat to Lollipop Updating

JINSI YA KU UPDATE ANDROID KITKAT KWENDA LOLLIPOP

No Computer needed…..

Utangulizi:
Bado Teknologia inakua kila sekunde.. Yapo Maboresho kila Nyanja hasa katika Mawasiliano kwa ujumla. Kompyuta na Simu za Mikononi zimechukua nafasi kubwa katika Nyanja nzima ya Mawasiliano.
Kampuni mbalimbali zakutengeneza simu nazo kila nyakati zinajitahidi kutoa Matoleo mapya na yalioboreshwa. Ipo mifumo (Operating Systems) mitatu inayofanya kazi katika Simu za kisasa zijulikanazo kama ‘Smartphones’. Mifumo ni Android, iOS na Windows phone. Upo ushindani mkubwa kwa Watengenezaji wake hali inayosababisha Uboreshaji kwa kila mfumo.
Binafsi napenda mifumo yote lakini mfumo wa Android ndio unatumika na watu wengi duniani kwa sababu kuu zifuatazo;
(i) Simu zinazotumia mfumo huu zinauzwa kwa Grarama ndogo zikilinganishwa na zinazotumia iOS na Windows phone.
(ii) Kuna zaidi ya Program 1.6 million zinazofanya kazi kwenye mfumo huu amabazo mtumiaji anaweza kuzitumia kwenye simu
Yake kuendana na Mahitaji yake.
(iii) Ni rahisi sana ku root Simu za Android. Rooting ni kitendo cha kukupa uwezo wa kutumia na kuifurahia simu yako kwa
asilimia mia moja. Ukisha root simu yako unakua na uwezo wa ku UPDATE mfumo wa simu yako (Mfano kutoka Kitkat
kwenda Lollipop), kuweka Program zilizozuiwa na Android Developers (Mfano program maalum za Kutunza Chaji, ku ‘boost’
simu yako, kukuongezea RAM, program za kukuwezesha kuipata simu yako hata pale mwizi anapoi flash), kutoa ‘System
applications’ ambazo huna kazi nazo, kuufanya mfumo wa simu UWE KAMA UTAKAVYO wewe, nk…
Kwa waliobahatika kuisoma Makala yangu ya JINSI YA KU ROOT SIMU YAKO YA ANDROID, nafikiri wananielewa zaidi hapa.
Kawa hujaiona Tembelea ukurasa wangu wa Facebook au wasiliana nasi 0757 413 078. Waweza pia kui search google
Kwani iliwekwa kwenye tovuti ya JamiiForums.
(iv) Zipo Program/Applications nyingi na za kisasa ambazo bado watumiaji wa iOS na Windows phone hawajazipata.

Mfumo huu wa Android una Matoleo yafuatayo hadi Makala hii inapoandikwa ambayo ni:
1. Cupcake (1.5)
2. Donut (1.6)
3. Éclair (2.0 – 2.1)
4. Froyo (2.2 – 2.2.3)
5. Gingerread (2.3 – 2.3.7)
6. Honeycomb (3.0 – 3.2.6)
7. Ice Cream Sandwich (4.0 – 4.0.4)
8. Jelly Bean (4.1 – 4.3.1)
9. KitKat (4.4 – 4.4.4)
10. Lollipop (5.0 – 5.1.1)
11. Marshmallow (6.0 --- )
Matoleo haya yanaboreshwa kila yajapo Mapya na Mpaka ninapoandika Makata hii Simu nyingi za Android zinazotumiwa na wengi zinatumia Andriod 4.4 – 4.4.4 (Kitkat). Mfumo wa mwisho (Marshmallow) umewekwa kwenye simu zilizotolewa hivi karibuni kama vile Nexus 6P, Nexus 5X nk... Kujua toleo lako nenda Settings˃About phone˃Android version. Kama upo Kitkat, huu ni Muda sahihi wa kufurahia Lollipop Experience. Binafsi Simu yangu ni Tecno H6 na nilishawishika kutoka KitKat kwenda Lollipop kwa sababu zifuatazo:
(i) Mfumo wa Lollipop uko ‘stable’ na fasta kuliko KitKat
(ii) Unatunza chaji kuliko Kitkat kwani ‘bugs’ nyingi zimekua fixed na pia ‘Power saving feature’ imeboreshwa
(iii) Una mwanga zaidi (More brighter) na pia una Visual effects nzuri na za kuvutia
(iv) Rahisi sana ku root
(v) Una uwezo wa ku manage app nyingi bila ujumbe wa ‘program not responding’ au ‘Unfortunately, program has
stopped’

JINSI YA KU UPDATE KITKAT KWENDA LOLLIPOP;

Vinavyohitajika;
- Muda
- Simu ya Android iliokua ROOTED tayari (ipo Makala jinsi ya kuroot, kwa atakaehitaji)
- Memory Card isiyo na tatizo ( angalao 8GB)
- Kifurushi cha Internet angalao GB 1 (kwa ajili ya ku download ROM na ku install program zako muhimu baada ya kufanikisha
zoezi zima)
Zoezi hili ni LA HATARI SANA KWA ATAKESHINDWA kufuata hatua zifuatazo kwa MAKINI kwani Simu yako HAITAWAKA tena ukikosea! Kinachotakiwa ni UMAKINI na Uhakika wa USAHIHI kwa kila unachokifanya! Ndio maana nimetangulia kusema andaa MUDA maalum unapoanza—usiwe na kazi nyingine. Binafsi nilisha update SIMU ZAIDI YA 40 sasa bila kuua hata moja!
Kwa kuanza, naamini simu yako tayari umeshai root, na sasa tuanze kupitia hatua moja baada ya nyingine kufanikisha zoezi zima.

1. Hakikisha simu yako ina Chaji ya kutosha. Inashauriwa wakati wa ku update iwe kwenye chaji.

2. Wezesha ‘’Developer Options” kwenye simu yako. Nenda Settings>About phone>Build number. Baadhi ya simu (LG na
HTC) nenda Settings>About phone>Software information>Build number. Ukishafika kwenye Build number gusa hapo
mara saba (tap 7 times)…mpaka uambiwe “You are now a Developer” Sasa nenda Settings>Developer options>USB
debugging. Weka tiki hapo (kama haipo). Hatua hii kwa wengi hua ni tayari kwani hufanywa wakati wa ku root.

3. Nenda settings>Security>Unknown Sources. Weka tiki hapo (Kama haipo).
4. Nenda Playstore install program inayoitwa [ROOT] Rashr – Flash Tool. Usiifungue baada ya kui Install.
5. Hatua hii ni ya Muhimu sana. Kabla hatujaiangalia tunapaswa kujua Mambo machache.
(i) Recovery – Hiki ni kipengele cha Mfumo wa simu au hata Computer ambacho kimetenganishwa na Mfumo wa kawaida
Wa simu. Hiki husaidia tunapo flash/ku update simu.
(ii) Bootloader ni sehemu ya Mfumo wa simu na hata Computer ambacho ndicho huamua Simu au Computer kuwakia
Kwenye Recovery au iwake kawaida. Kwa wale wanao Install Windows OS kwenye Computer zao wananielewa zaidi
hapa. Unapoweka DVD ya Windows files na kuwasha PC yako na Kubonyeza F11 KEY. Hapo ni kwamba unai Instruct PC
yako iwake kwenda kwenye Recovery. Ndicho tunachokifanya tunapo Install Android Lollipop ROM.
(iii) ROM (Operating System Image) – ni Flash files ambazo ndizo huwekwa kwenya Read Only Memory (ROM) ili simu
iweze kuwaka.
(iv) Android Custom Recovery. Watengenezaji wa Simu za Android wame lock Bootloader ili watumiaji wake wasiweze ku
Install ROMs mbalimbali kwenye simu hizo. Wameweka Recovery ambayo hairuhusu kuflash chochote.
Sasa hapa ndipo hatua ya tano ilipo, Ku Unlock Bootloader ili tuweze ku flash ROM yoyote kwenye simu ya
Android. Kufanikisha hatua hii tuna flash Android Custom Recovery nyingine itakayoturuhusu kuflashia ROM
mpya Kwenda kwenya Mfumo wa simu. Zipo Android Custom Recovery mbili (2) ambazo hutumika sana tunapo flash
Android Devices ambazo ni ClockworkMod Recovery (CWM) na Team Win Recovery Project (TWRP). Hapa nashauri twrp
kwani ni rahisi kutumia, inaeleweka zaidi na ina Option nyingi.
Hatua za ku Install twrp;
- Kwa kutumia simu yako au PC, nenda google kisha search tmrp ya Simu yako. Mfano kama unatumia Tecno H6, search
‘twrp image for Tecno H6’ au ‘Team Work Recovery Project image for Tecno H6’ kisha i download.
- Ukishai download iweke kwenye Memory Card ya simu unayotaka kuiflash.
- Fungua Rashr (rejea hatua ya nne hapo juu) kisha gusa ‘Recovery from Storage’. Hapo chagua twrp ulioi download.
Gusa ‘Yes’ utakachoulizwa. Kama itakua imefanikiwa Utaona ‘ Partition flashed. Reboot into Recovery now?’ Gusa ‘NO’
Kisha nenda hatua ya 6.

6. Hatua hii ni ya KU DOWNLOAD Lollipop ROM kwa ajili ya SIMU YAKO. Ziko ROMs nyingi kutoka kwa Developers tofauti.
Binafsi nilishakutana nazo nyingi na asilimia kubwa zilikubali lakini nyingine hua zinakataa!! Nenda Google kisha search ROM
ya Simu yako…Mfano kama unatumia Tecno H6; search ‘Lollipop ROM for Tecno H6’ Nyingi hua ni zaidi ya MB 200.

Tahadhari; Kabla ya ku download ROM utakayoiona soma kwanza COMMENTS za walioitumia ili uweze kujua kama ilikubali
kwao. Baadhi ya ROMs hua zilishakua infected na Virus na ukizi Install hua zinakataa!! Na zikikataa hua nia HATARI
kubwa kwani simu haitawaka tena!
Baada ya kui download iweke kwenye Memory Card ya Simu unayotaka kui flash/update.

7. Hatua hii ndio kiini cha Zoezi zima! Nunua kikombe cha Kahawa weka pembeni, mwombe Mungu kisha ENDELEA….
Fungua tena Rashr kisha gusa ‘Reboot Recovery’. Sasa simu yako itawakia kwenye Recovery ( Team Win Recovery Project)
kama inavyoonekana pichani.

Kama tulivyokwishaona, zoezi la Kuflash linaweza ku fail..na ikitokea SIMU HAITAWAKA TENA!
Ni mpaka Computer na USB vitumike KUFUFUA simu hio! Sasa kuepuka hili, hua tunahifadhi mfumo uliopo ili likitokea tatizo
tuurudishe simu iwake.. Ili kuuhifadhi mfumo uliopo, gusa ‘Backup’ , weka alama kwenye Boot, Unboot, nvram, System,
na Cache,,, gusa Storage na uweke alama kwenye sd card kisha ‘Swipe to Back Up’
Ikishamaliza ku back up rudi nyuma kisha gusa ‘wipe’ ˃ ‘Advanced wipe’ kisha weka alama kwenye Dalvic Cache,
System, Cache na Data kisha ‘Swipe to Wipe’ Kumbuka ku format System ndicho kinachofanya Simu isiwake tena kwani OS
haipo tena mpaka hatua hii. Kwa hio hakikisha Backing Up Process ilikamilika kabla ya ku format/wipe Simu.

8. Baada ya ku back up na ku wipe, rudi nyuma, gusha ‘Install’, chagua ile ROM ya Simu yako uliokwishai download kisha
‘Swipe to Confirm Flash’. Ni ndani ya Dakika zisizozidi 10, utakua tayari una Android Lollipop experience kwenye simu yako!!!
Gusa Reboot ˃ System
Angalizo; Kuna baadhi ya Lollipop ROMs ambazo System apps hazijawa included. Uwe makini hapo, kama hio ROM haina apps, lazima kuna maelekezo ya ziada ulipoipatia hio ROM.

9. (Hatua hii ni endapo Flashing process ili fail…) Gusa Restore, chagua Package yenye tarehe sahihi kisha Swipe to Restore.
Hapo ule Mfumo uliopo utarudishwa na simu yako ITAWAKA kama kawaida. Kama bado utakua na nia Tafuta ROM nyingine tofauti kisha jaribu tena.

Hitimisho:

Mwandishi wa Makala hii hatahusika kwa Uharibifu wowote utakaofanywa na baadhi ya Watu watakaokosa Umakini wakati wa Kuflash Simu zao. Hatua zote zilizoelezewa hapa ni SAHIHI na alieziandika hua anazitumia na kufanikiwa.
Waweza pata Msaada kutoka kwa Mwandishi wa Makala hii kama vile;
- Kupata ROM sahihi kwa ajili ya simu yako (ndani ya saa 24). Hua nina ROM za simu ambazo ni popular na zilikubali kwenye Simu hizo. Ukihitaji utatumiwa ‘download link’ ili ui download kwenye simu yako.
- Kua na mawasiliano ya moja kwa moja na Mtaalam pale unapoanza zoezi hili… hapa utakua unatoa taarifa kwa kila hatua ambayo utakua huelewi au kama kuna tatizo.
- Kuuliza swali lolote kuhusu Makala hii.

Nikutakie kila la Kheri wewe utakaeamua kuchukua hatua za kufurahia Maisha MAPYA na Android Lollipop Experience…

Mawasiliano;

Phone Number: 0757 413 078

E-Mail adress: chriss.ath2@gmail.com

VICTORY SERVICES

Mwandaaji & Mwandishi: Athanas Chriss

Regards…..
Ahsante sana mkuu kwa darasa,
Ningependa kufahamu kama baada ya kuflash ikashindwa kuwaka na inaishia kwenye TECNO BOOT LOGO, nifanyeje kuirudisha mwanzo kabisa?
 
Kuna wadau wananambia kwamba kuroot simu unapoteza usalama wa simu,,ni kwel au
 
Ahsante sana mkuu! Hatimae nimefanikiwa ku upgrade. Ila jana niliweka avg anti virus pro ika-detect malware which is cynagogen nikaidelete. Nika reboot matokeo yake simu ina pop up tu hai boot mpka leo. Nikijarbu ku hold volume up and power button hataki msaada plz!
 
Pole sana kwa tatizo hilo.
Chukua namba ya mawasiliano iliyokwenye makala uwasiliane moja kwa moja na muandaaji kwa msaada zaidi.

Sent from my TECNO-Y3 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom