Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,941
- 32,044
KITABU CHA MAISHA YA JAKAYA MRISHO KIKWETE
Rafiki yangu kanipigia simu kutoka duka la vitabu la Mkuki na Nyota, Samora Avenue ananitaarifu kuwa kipo kitabu cha maisha ya Jakaya Mrisho Kikwete.
Nimeshtuka tena sana kwani kitabu hiki nimekisubiri kwa hamu kwa miaka toka niliposikia kuwa kinaandikwa kitabu cha maisha yake.
Kitabu hiki kimeandikwa na Julius E. Nyang’oro.
Haraka nimekifungua na kutazama yaliyomo mwanzo wa kitabu kisha nimeruka hadi mwisho wa kitabu kuangalia faharasha.
Nimeangalia mwanzo wa kitabu na kukuta Sura ya Nne inayoeleza alivyogombea Urais wa Tanzania mwaka wa 1995.
Haukupita muda nikawa nimemaliza sura hii lakini sura imeniacha na maswali mengi kupita kiasi.
Naendelea kusoma sura za mbele.
Imekuwaje?
Najiuliza.
Nikarejea tena kwenye faharasha nasoma majina ya wote ambao mwandishi kawataja katika kitabu cha JK.
Nashangaa.
Mbona sioni jina la Rostam Aziz wala la Prof. Kighoma Ali Malima?
Kwa yale ambayo mimi nayajua hata bila utafiti wa kuandika kitabu hawa ni watu muhimu katika maisha ya JK.
Kwa wafatiliaji wa siasa za Tanzania miaka ile ya utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 1995 watatambua kuwa siasa zilikuwa moto sana nchi nzima.
JK hakupita Dodoma na hii ni historia ya peke yake.
JK aliporejea Dodoma 2005 kugombea urais alikuwa na timu kali sana ya vijana maarufu kwa jina la ‘’Wanamtandao.’’
Hawa hawakujitokeza hadharani lakini wakifahamika kwa uwezo wao wa fikra na halikadhalika kwa uwezo wao wa fedha.
Kuwajua hawa ilibidi lazima mtu uwe na sikio lako ardhini, ‘’An ear to the ground.’’
Bila hivi utabakia na jina la ‘’Wanamtandao,’’ peke yake.
Inasemekana Wanamtandao walitanda nchi nzima na wote walikuwa na simu za mkononi kwa mawasiliano ya haraka na ya uhakika.
Mwandishi hajawataja hawa na kwa kukosa kuwataja hawa na vishindo vyao mwandishi katoa ladha katika kitabu cha maisha ya JK.
Kitabu hiki hakijamtaja Rostam Aziz wala Prof. Malima.
Uchaguzi wa 1995 ulikuwa na mambo makubwa yaliyowagusa JK na Prof. Malima ambayo kwa hakika si ya kuachwa kuelezwa katika kitabu hiki.
Kipindi cha wagombea urais wa CCM walipokuwa wanajitayarisha kwenda Dodoma kuchukua fomu magazeti yaliandika kuwa Waislam wanafanya kampeni ya kuchagua Rais Muislam katika Uchaguzi wa 1995.
Kitabu kingenoga sana endapo mwandishi angepita huko na kueleza haya na kutufunulia ni nani walikuwa wahusika wakuu wa propaganda hii na nini ilikuwa nia yao?
Mawaziri Waislam katika Baraza la Mawaziri la Rais Ali Hassan Mwinyi walijikuta katika hali ngumu sana.
Ndani ya Bunge propaganda hii ilishika kasi kiasi wale mawaziri Waislam ambao magazeti yaliwataja kuwa wanaweza kuwa wagombea urais ilibidi wasimame ndani ya Bunge kudai kuwa wao hawana nia ya kugombea urais.
Hapa ndipo anapoingia Prof. Malima.
Prof. Malima alikataa kuorodhesha jina lake.
Jina lake halikuwa katika orodha ya mawaziri Waislam waliosema kuwa hawana nia ya kugombea urais halikadhalika saini yake haikuwako.
JK jina na saini yake vilikuwako.
Yako mengi katika uchaguzi huu ambao endapo mwandishi angeyaandika kitabu hiki cha maisha ya JK kingetia fora.
Lakini juu haya kitabu hiki ni kizuri na si cha kukosa mtu kukisoma.
Msomaji atakifaidi kitabu hiki endapo atahangaisha bongo lake kuangalia siasa za Tanzania zilivyokuwa huko nyuma na kufananisha na hali ilivyo hivi sasa.
Je, kuna kitu viongozi wetu katika ngazi za juu wamejifunza kuwafanya wawe viongozi bora na makini zaidi katika kuuendea Urais wa Tanzania?
Hitimisho
Nilidhani hiki ni kitabu cha JK ambacho nilichokuwa nakisubiri kwa muda mrefu.
Msomaji mmoja kaniandikia kuniambia hiki sicho.
Nakipekua nakuta kitabu kimechapwa 2011.
Kinachonishangaza ni kuwa imekuwaje kitabu hiki sikupata kukisikia miaka yote hadi hii leo?