Kipindi cha Uangalizi kwa Mama aliyejifungua Mtoto Njiti sio likizo ya Uzazi

Wild Flower

JF-Expert Member
Jul 20, 2023
351
721
Your browser is not able to display this video.

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango, akiwa katika Sherehe za Kilele cha Mei Mosi Kitaifa, zilizofanyika jijini Arusha alitangaza kuongezeka kwa Siku za likizo kwa Wanawake wanaojifungua Watoto Njiti (Kabla ya Wiki 36 za Ujauzito)

Kuanzia sasa iwapo Mfanyakazi atajifungua Mtoto Njiti, kipindi cha uangalizi maalumu hakitahesabika kama likizo ya uzazi. Likizo ya uzazi itaanza tu baada ya kumalizika kwa kipindi cha uangalizi, kadiri madaktari watakavyothibitisha

Vilevile, Mfanyakazi huyo ataruhusiwa kutoka Kazini Saa 7:30 mchana kila Siku kwa muda wa Miezi sita baada ya kumalizika kwa likizo ya Uzazi, ili kumpa fursa ya kwenda kunyonyesha.
 
Kwahiyo hizo siku za uangalizi huyo mzazi atakuwa kazini? .....UPUUZI MTUPU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…