Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 351
- 721
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango, akiwa katika Sherehe za Kilele cha Mei Mosi Kitaifa, zilizofanyika jijini Arusha alitangaza kuongezeka kwa Siku za likizo kwa Wanawake wanaojifungua Watoto Njiti (Kabla ya Wiki 36 za Ujauzito)
Kuanzia sasa iwapo Mfanyakazi atajifungua Mtoto Njiti, kipindi cha uangalizi maalumu hakitahesabika kama likizo ya uzazi. Likizo ya uzazi itaanza tu baada ya kumalizika kwa kipindi cha uangalizi, kadiri madaktari watakavyothibitisha
Vilevile, Mfanyakazi huyo ataruhusiwa kutoka Kazini Saa 7:30 mchana kila Siku kwa muda wa Miezi sita baada ya kumalizika kwa likizo ya Uzazi, ili kumpa fursa ya kwenda kunyonyesha.