Kipi kinafanya Rasimu ya katiba ya warioba ikose uhalali kwa Serikali na CHADEMA na Vyama vingine vya upinzani kuipigia kelele kuhalalishwa?

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
May 10, 2012
10,714
23,507
Kila siku huwa naipitia Rasimu hii nikijiuliza hasa ni kitu gani kinafanya inakosa Uthamani mbele ya Watawala na wapinzani au Ni neno Tanganyika lililosheheni kwenye katiba hiyo?

Au Ni serikali Tatu zilizopo kwenye sura ya Sita na Saba ya katiba hiyo na Ibara ya 60 na kuendelea ya katiba..

Sioni makosa yoyote kila nikisoma Katiba hii iliyofanya mheshimiwa Rais mstaafu JK kikwete ashindwe kuipitisha na hata JP Magufuli ashindwe kuipa nguvu kuwa Katiba halali Ya Muungano..

Kipi kigumu kukimeza Ni hiyo serikali Tatu..
Au ni kipi Ningependa Niambiwe..

Kwa sababu kibaya zaidi CHADEMA wanaikataa lakini kwenye maoni yao Waliyotoa Juzi 85% yametoka kwenye Rasimu hiyo..

Au ni swala la Mgombea Huru asiye na chama?
Au ni Bunge kupewa Nguvu ya maamuzi?

Au ni Idadi ya mawaziri na Naibu waziri ambapo katika imeelekeza wasizidi 15 ," ibara ya 98 ya katiba hiyo".

Au cheo cha Waziri mkuu kuitwa Waziri Mwandamizi badala ya Pride waliyoizoea?

Au ni ile Ruhusa ya Waziri na Naibu waziri Kutohudhuria Bungeni (Kunyimwa Posho 😅 za mahudhurio bungeni mpaka wawe na Shughuli maalumu?) "Ibara ya 103 ya katiba"

Au ni ile sekretarieti ya baraza la mawaziri?

Au ni kupunguzwa kwa Idadi ya wabunge yaani 50 kutoka Tanganyika na 20 kutoka Zanzibar kufanya idadi ya majimbo mchi nzima kuwa 70 (Ibara ya 113 (2a ))

Na kufanya wabunge wa Majimbo kuwa 140 tu..
Na sio 264 kama ilivyo sasa!

Na hiyo Kufanya idadi ya wabunge wote kuwa 150 tu na sio 393 ilivyo hivi sasa?

Au ni Bunge kunyimwa Uwezo wa kufanya marekebisho wa baadhi ya Ibara za katiba endapo itapita?

Au ni Spika wa Bunge kutokuwa Mbunge?

Ni vitu vingi vinanichanganya sana ila naona ni bora niishie hapo nisizidi kuchangamyikiwa..

Lakini kuna mengi yamejificha Juu ya Ugali wa Viongozi kwenye Katiba hii
 

Attachments

  • RASIMU YA KATIBA TOLEO LA PILI.pdf
    1 MB · Views: 3
Back
Top Bottom