Kipi kimemkuta Godfrey Tumaini (Dudu Baya/Konki Master)?

Habarini wanajukwaa.

Ni muda mrefu sasa umepita tangu watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa IG kumuona KONKI3MASTER akitoa maoni yake yenye lugha ya 'matusi' dhidi ya 'wanyonyaji' wa wasaniii.

Na mara ya mwisho alionekana amejirekodi videos akimvurumishia 'mvua' ya matusi mkurugenzi mkuu wa Benchmark Production waendeshaji wa shindano la BSS Bi. Madam Rita. Baada ya hapo akaitwa kwa barua Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

Nataka kujua, kipi kilitokea baada ya huo wito maana naona kimya? Kipi kimemkuta Dudu Baya? Mbona hata haposti kitu chochote kwenye page yake, vipi alifungiwa na TCRA kutumia IG baada ya zile 'MVUA' za matusi? Mwenye taarifa zake please mana akaunti yake ni mda sasa haipositiwi kitu na habari zake zisisikii kabisa.
itakuwa hana smart phone
 
Mkuu huyo jamaa mara ya kwanza alifungiwa baada ya kuanza kuchafua watu mtandao wa Instagram,alikuwa anataja list ya watangazaji wasio na marinda na kuwatukana watangazani wa clouds fm , Ruge alipofariki alimtukana sana .

Baada ya kufungiwa na basata akaomba msamaha ,haijapita mwezi akaanza tena kuwatusi watu kitu ambacho yeye anaita mapunduzi ya mziki lakini harakati zake ilikuwa ya udhalilishaji watu ,ndipo BASATA ikamfungia tena wakishirikiana na TCRA ,na amefungiwa na hakuna msamaha tena ,basata walisema hata asihangaike tena kuomba msamaha washafuta leseni yake na hata akiomba msamaha hatasikilizwa.
Sasa itabidi arudi hapa Mwanza maeneo ya Mhandu Machinjioni ili ashirikiane na kakaake kuuza mabaki ya nyama hapa kwenye solo la Machinjioni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom