Kipanya Katunix Ya leo Inamaanisha Nini ACT kuwa Chama Kikuu cha Upinzani?

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
May 10, 2012
12,025
27,104
FB_IMG_1744947127254.jpg


Naona Zambarau Ikineemesha vizuri kabisa Kijani hapo Juu Baada ya CDM kususia Uchaguzi?
 
View attachment 3308027

Naona Zambarau Ikineemeka vizuri kabisa Baada ya CDM kususia Uchaguzi?

CUF ya Mapanga Shaa tuliambiwa ni chama cha kiislam kwa sababu tuu kiliumgwa mkono na watu wa mikoa ya Pwani na waZanzibar wenye asili ya Oman .Tukaambiwa kamwe hawawezi kuitawala Zanzibar . Ikawa inasemwa wazi na CCM kuwa , CUF wakiingia madarakani kwa vikaratasi basi mapinduzi ni daima . Hatukusikia Mwana CCM yeyote aliyekamatwa kwa uhaini maana walikua wanatishia kufanya mapinduzi endapo Maalim Seif ataingia Madarakani .
Sasa leo Mwarabu na mjukuu wa Sultani na mfalme wa Oman yupo Madarakani Tanganyika wale wale waliokua wanamkataa Salm Ahamed Salm na Maalim Seif wapo Kimya wanaonambikia Kesi ya uhaini Tundu Lisu.


Lakini pia hicho Kibomzo kinaonyesha mto unatoa maji jangwani na kuyapeleka kwenye kijani .
Watakaonufaika na uchaguzi kwa upande wa Tanganyika ni CCM .

Lakini pia Hata sasa chama kikuu cha upinzani bungeni ni ACT kwa sababu kuna wabunge wengi wa kuchaguliwa . Chadema kina mbunge mmoja tu.

Kwa vyovyote CCM ililazimisha Samia aendelee ndio inajiua yenyewe na ACT inaandaa barabara nzuri ya Chandema kuingia madarakani na CCM itapotea kabisa na kuundwa kwa chama kingine kitakachounganika kati ya CCM , NCCR Mageuzi , TADEA , Demokrasia Makini na , TLP ,DP n.k.
Ambapo ACT watashirikiana na Chandema kuachiana majimbo mpaka hapo baadae wataungana na kuunda chama kipya . Hivyo chandema nayo itakua imekufa na kubaki vyama viwili vyenye nguvu ambapo kile Kilichoungana kutokea CCM kitashinda tena kwa miaka 10 na kupotea tena.

Kwa sasa CCM haipo tena kwenye mioyo ya watanzania zaidi ya Rushwa na nguvu ya bunduki kulinda maslahi ya watu wachache waliohujumu hii nchi kwa muda mrefu .
 
Chambua hii cartoon
umeshaeleza kinagaubaga hapo juu gentleman, kulingana na kibonzo chenyewe kwamba kuyeyuka kwa ACT Zanzibar kunaiimarisha na kukirutubisha chama tawala as you can see katika katuni..

Na hiyo ni kutokana na kiongozi wa act mwenye kiburi sana Zanzibar kuonyesha kila dalili kuiengua act kushiriki uchaguzi mkuu kwa upande wa Zanzibar 🐒
 
umeshaeleza kinagaubaga hapo juu gentleman, kulingana na kibonzo chenyewe kwamba kuyeyuka kwa ACT Zanzibar kunaiimarisha na kukirutubisha chama tawala as you can see katika katuni..

Na hiyo ni kutokana na kiongozi wa act mwenye kiburi sana Zanzibar kuonyesha kila dalili kuiengua act kushiriki uchaguzi mkuu kwa upande wa Zanzibar 🐒
Aaaah sawa
 
Halafu Demokrasia Itakuwa Wapi?
Umeona Tamko la Marekani Kuhusu Uchaguzi?
hii marekani yenye matatizo yake ya ndani ya kisiasa chungu nzima pamoja na vita ya kiuchumi karibu na kila taifa ulimwenguni?

Itafanya nini wapi na yenyewe ina matatizo ya kuyatatua?
Au ijifanye nyani haoni kundule?

au marekani ipi unaizungumzia gentleman?🐒
 
Back
Top Bottom