Kiongozi wa upinzani Rwanda, atangaza serikali mbadala

mimi uzuli nimeishi rwanda kwa miaka kama minne ukweli ni kwamba nchini ukweli ni kwamba kitendo cha mwanasiasa yoyote au mtu yoyote kutangaza nia ya kugombea URAISI
ukiwa Rwanda hiyo inaitwa kesi ya UCHOCHEZI na adhabu yake ni kifo au gerezani

nakumbuka enzi za mwanamama victoria ibugabire huyu mama aliwahi kutangaza nia ya kugombea kiti cha uraisi lakini mwisho wa siku alifugwa gerezani kwa uchochezi na baada ya siku tatu katiba ilibadilishwa ili kumfanya paul kagame aendelee kutawala muhura wa tatu wakati alishamaliza muda wake wa mihula miwili lakini katiba ilibadilishwa.

sio rwanda tuu hata uganda,zimbabwe vitu kama hivo vilifanyika vya kubadili katiba ili waendelee kutawala.

haya mambo kuna nikiyafikilia nashidwa kutofautisha utofauti kati ya utawala wa mtu mweupe na mtu mweusi
 
Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda, ametangaza kuunda serikali sambamba na utawala uliopo Rwanda, lakini itakayokuwa ikifanya kazi nje ya nchi.

Thomas Nahimana ambaye ni kasisi wa zamani anayeishi nchini Ufaransa ametangaza kuunda serikali hiyo itakayofanyia kazi uhamishoni.

Katika mazungumzo na BBC, mwanasiasa huyo anasema lengo la serikali yake ni kuiondoa madarakani serikali ya rais Paul Kagame, anayemlaumu kuvunja sheria na kukandamiza wananchi.

Thomas Nahimana, amekatazwa kuingia Rwanda kujiandikisha kama mgombea wa kiti cha urais, katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Baraza lake la mawaziriView attachment 472650Baadhi ya aliowataja katika baraza lake la mawaziri ni wafungwa wanaotumukia vifungo vya jela nchini Rwanda kwa makosa kama vile kukanusha kuwa mauwaji ya kimbari hayakufanyika nchini Rwanda mwaka 1994.View attachment 472651Bw Nahimana (kushoto) naakiwa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta mwaka jana ambapo alizuiwa kwenda Rwanda
Bw Nahimana, ambaye ni mhutu, amelaumiwa kwa kuandika taarifa kadhaa za kikabila na kumkosoa rais Paul Kagame.

Chama chake cha Ishema, bado hakijaandikishwa nchini Rwanda.

Ufaransa inamtumia kuanzisha vurugu Rwanda, Wazungu hawaoni raha Nchi za Afrika kuwa na Amani ili ziendelee. Rwanda uchumi unakua kwa kasi, vibaraka wanaofugwa kwa wazungu na wale wa ndani ya nchi wanataka tena vurugu zianze. Wazungu mlaaniwe
 
hahahahaha umeongea kwa uchungu
 
Ufaransa inamtumia kuanzisha vurugu Rwanda, Wazungu hawaoni raha Nchi za Afrika kuwa na Amani ili ziendelee. Rwanda uchumi unakua kwa kasi, vibaraka wanaofugwa kwa wazungu na wale wa ndani ya nchi wanataka tena vurugu zianze. Wazungu mlaaniwe
Kwenye nchi ya kidemokrasia iweje kugombea urais iwe ni vurugu?
 
Kwenye nchi ya kidemokrasia iweje kugombea urais iwe ni vurugu?
Swali la kijinga. Rejea uchaguzi wa Tanzania 2015. Chama kimoja kikuwa kikisema kuwa wapinzani wao ni wahuni tu kazi yao ni vurugu. Au una selective memory. SMH
 
Kweli naheshimu mitazamo ya watu..lakini bado waafrika wengi tunamadhara ya ukoloni. Tafakari yangu baada ya comments nyingi nimeona watu wengi wanafikra za uoga ndani the yao na sio watu wenye uwezo waudhubutu, hili linasababisha kila kitu kuonekana hakiwezekani, na ndio fikira za watoto wetu pia, lakini ukijua tu Kagame sio Mungu basi kidogo mtu anaweza kufikiri zaidi...
 
Swali la kijinga. Rejea uchaguzi wa Tanzania 2015. Chama kimoja kikuwa kikisema kuwa wapinzani wao ni wahuni tu kazi yao ni vurugu. Au una selective memory. SMH
Kwa hiyo unavyokumbuka ni mpinzani gani aliyezuiwa kugombea?
 
Back
Top Bottom