Kinjekitile Ngombale Mwiru: Haiingii akilini kila mwenye tuhuma na kashfa akimbilie upinzani

Mwanaharakati Kinje Ngombare Mwiru, amezungumza mtazamo wake kuhusiana na sakata zima la msanii Wema Sepetu kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo

Amesema kitendo cha CHADEMA kumpokea Wema kinaonyesha dhahiri kwamba Vyama vya Upinzani vimeanza kupoteza mwelekeo kisiasa na vinashindwa kupambana na Chama cha Mapinduzi(CCM) ambacho kinashughulika na mambo mbalimbali yanayowakabili wananchi

"Haiingii akilini kila mwenye tuhuma na kashfa akimbilie upinzani. Huo ni udhaifu mkubwa unaofanywa na viongozi wa vyama hivyo, wameshindwa hoja za msingi kupambana na CCM sasa wanajisifu na kujigamba kwa kuwakaribisha watu watuhumiwa", alisema Kinje

Aliongeza kwa kusema ni jambo la kusikitisha na kushangaza kuona hata alipoingia Edward Lowassa CHADEMA , Chama hicho kilikosa hoja na ndipo kilipoanza kupoteza mwelekeo na matokeo yake yanaonekana katika uchaguzi ambapo CCM ilipata ushindi mkubwa

Kitendo cha CHADEMA , kupokea wanachama wenye tuhuma mbaya ni dhahiri inaonesha chama hicho kimepoteza uelekeo na kukwamisha vyama vya upinzani

Alimaliza kwa kusema wananchi wanapatwa na wasiwasi juu wanasiasa ambao ni watuhumiwa wa dawa za kulevya kuwepo kwao kwenye siasa ni kama maficho ya uharifu.

Chanzo: Dar24



Huyu dogo si ni yule anayedaiwa kuuza unga na kuwasafirisha watanzania wanaokufa South Africa, yaani leo hii kawa msemaji wa chama anachokifadhili kwa madawa anayouza? Hii ni hatari sana.
 
Ndio siasa zetu hizo, kama comedy, eti tunaangalia mtu anawafuasi wangapi kutoka mitandao ya kijamii, haya kuweni makini hata kaoge ana followers na wafuasi kibao kwenye mitandao ya jamii.
Ndugu unaweza kutaja mtu hata mmoja ambaye alishawahi kukataliwa na chama chochote cha siasa duniani kote kisa anatuhumiwa/ amekutwa na makosa kadhaa mbali na usaliti ndani ya chama?
 
Say no to actors, sawa je mtuhumiwa wa ufisadi (walimsakama wenyewe kwa muda wa miaka nane mara wamseme, mchafu hafai kuwa rais, fisadi nk sasa hivi ndiye mgombea rais wa kudumu) , madawa ya kulevya kuhamia chama kingingine kinaondoa tuhuma ? au labda wao wana mamlaka ya kuwasafisha watu? Hebu ni jibu hilo, ila kama ni kweli mnathamini image ya chama si sawa ila ni sawa kama hamthamini image ya chama.Ila kaa ukiijua tabia za wanachama ndizo zina reflect twasira ya chama sehemu yoyote duniani.
 
Aongee mtu mwingine siyo Kinje aliyeshindwa shule kwa kuvuta bange, na madawa ya kulevya. Hana purity wala charisma yoyote ya ku challenge mchakato wa madawa ya kulevya.
 
Back
Top Bottom