Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,198
- 2,909
King Mseke (9), mtoto wa msanii wa hip-hop Tanzania Joh Makini, amewasili katika Academy ya Klabu ya Manchester City nchini Uingereza kwa ajili ya mafunzo ya soka ya wiki mbili. Joh Makini amesema mwaliko huo umetokana na juhudi za muda mrefu za kukuza kipaji cha King, kilichoonekana akiwa na umri wa miaka minne.
Mafunzo hayo yataleta tathmini ya kitaalamu kuhusu uwezo wa King na ushauri wa kuboresha kipaji chake, hatua ambayo Joh anaamini itafungua milango zaidi katika safari yake ya soka.
"Ni stori ndefu sana, hivi ni vitu ambavyo tumekuwa tukitafuta wenyewe na kuvifanyia kazi kwa miaka kuhakikisha kipaji cha Mtoto kinaonekana, King alianza mafunzo serious akiwa na miaka minne au mitano baada ya kumuona ana kipaji ilibidi niivalie njuga sikutaka kuchukulia poa kabisa" - Joh Makini.
"King Mseke ambaye ni Mwanafunzi wa darasa la tano, aliondoka Tanzania kwenda Uingereza ljumaa December 13 2024 ambako atakuwa kwenye mafunzo hayo ya Manchester City kwa muda wa wiki mbili "haya mafunzo unapata mwaliko kutokana na juhudi zako na uwezo wa Mtoto".
"Wakishamaliza mafunzo wanaandaa ripoti jinsi walivyomuona Mtoto na pia wanakushauri vitu vya kufanyia kazi, unajua wale wako mbele sana wana vipimo vyao Mtoto anapimwa kila kitu yani wanaweza kukwambia mpaka shuti la huyu Mtoto uzito wake, mikimbio yake kitaalamu n.k, naamini hii safari yake itafungua milango mingi sana kwa huyu Mtoto" Joh Makini.
Chanzo: Ayo TV