Kina baba tubadilike tupunguze ukoloni lasivyo kina mama wataendelea kuzoa points kwa watoto, uzeeni watamjali mama huku wewe uliyepambana unatengwa

gearbox

JF-Expert Member
Apr 20, 2024
563
1,768
point yangu sio kutegemea uje kutunzwa na watoto, ni kwamba ukizeeka muda mwingi watoto wako watakuwa karibu na mama yao kuanzia kumjulia hali, kumsaidia, kumpa faraja na hata kwenye simu unakuta watoto wanampigia sana mama yao, mtoto anakuwa bado anakuheshimu kama baba lakini shida ni kwamba hayupo huru na kujiamini kikamilifu, yote haya sababu hukuweza kubond nao vizuri, wanachokumbuka kwako zaidi ni ukoloni na ukali wako, urafiki kwa watoto ni muhimu sana, sisemi kwamba tusiadhibu watoto wanapolosea bali tusisahau kujenga bond / ukaribu.

naongea kwa experience naiona kwenye familia nyingi, Watoto wakienda kusalimia wazazi mama akiwa peke yake mzee kasafiri wanaweza kukaa hata siku nzima, baba akiwepo watoto watakaa nusu saa tu washapotea, Mama ndie anapewa hela za misaada watoto wanamwambia ampe mzee kiasi anachoona kitamfaa.

wababa wa kiafrika tumekuwa wakoloni sana na hili ndilo linasababisha hata watoto wetu wanakuwa huru zaidi na mama zao kuliko sisi tunaopambana kuwalisha, kuwasomesha, kuwavisha, n.k.

Nani kakwambia kuwa baba lazima uwe mkali mkali tu kugombeza, kutoa kipigo, n.k. hii kitu itawaharibu sana watoto wako kisaikolojia. Wengi wanadhani mtoto akiwa mkubwa anasahau lakini wanakosea sana, kisaikolojia unakuwa umeweka permanent damage. mtoto atakuheshimu ila hana uhuru wala kujiamini kwa asilimia 100 akiwa na wewe.

Tangu mtoto akiwa mdogo jaribu sana aujue upande wako positive anaoweza kuuona kwa macho yake, huko mihangaikoni ni kweli tunapambana kuwajali watoto wale, wavae, wasome, n.k. lakini watoto hawajionei kwa macho yao unavyopambana, mama yao wanaemuona live anavyowajali hata kama anashinda nyumbani muda wote hana kazi. na wewe hakikisha unawajali kwa namna wanayoweza kuona uhusika wako.

Narudia tena usisubiri wawe wakubwa, hilo ni kosa kubwa sana, utakuwa kama mgeni, kumbuka mama yao kaanza kubond nao tangu kichanga, na wewe usiwe nyuma sana jitahidi walau akiwa na miaka miwili muanze kubond.

  • Mawasiliano ni msingi wenu wa ukaribu, jenga mazoea ya kupiga nae story tangu mdogo. sio muda wote kuongea maendeleo ya shule, maelekezo ya kazi, kufatilia adhabu, n.k. wababa wengi wanaruka hii hatua ndio maana hata wakinunulia watoto zawadi, kuwatoa out, n.k. bado haisaidii.
  • Mara nyingine wakipewa adhabu na mama yao jaribu kuwatetea ama wasaidie kisiri kuimaliza.
  • Fundisha kuendesha gari / pikipiki / baiskeli.
  • nenda nao benki unavyolipa ada
  • wakabidhi pesa za mavazi, ada, n.k. uso kwa uso usimpe mke awape (tayari ana mbinu kibao za kubond)
  • waletee vizawadi na hakikisha unawapa wewe
  • cheza nao michezo
  • wanapokosea waelimishe madhara, wakirudia waonye, wakirudia tia viboko / mikanda, usitumie ngumi, kuwarukia mateke, kuwapiga kwa gogo, n.k.

Ni kweli inabidi uwe strict kama baba kwenye future yao lakini usisahau ku enjoy nao present muda mlionao kabla hawajawa wakubwa. kumbuka hata kina mama huwa wanatoa adhabu ila baada ya muda mambo yanajirudi, ni kwasababu ya kujenga mazoea nao.

Kwenye kutoa adhabu hakikisha unamshirikisha mke wako wote mgawane points.

Jiepushe kuwa baba ambae ukisafiri, watoto wanajisikia amani na furaha.
 
Kizazi cha wababa wakoloni bado kipo kweli??? Kama wapo basi wamezeeka ukoloni unaishilia......walikua kina baba na nusu 👍

Kimeingia kwa kasi ya kimbunga kizazi cha watoto wasioishi na baba "zaa nitalea" kizazi cha mama ni mama, mama ni baba....hatari.

Sijui madingi wa baadae watakuaje hata.
 
Nimegundua swala la kukaa karibu na familia hasa watoto mpaka bondi ikubali kama wenzetu wazungu ni tabia ya ndani sana ya kuzaliwa na ucha Mungu ndani yake.

Kuna broo mmoja yeye kila siku anarud home watoto washalala na siku akiwatoa ni anawapeleka kama swimming anawabwaga na kulaza mshale kurudi anawaitia pikipiki ....imeisha hiyo
 
Hiki ndiyo kizazi hatari sana kitakachomaliza kabisa upendo kwa wanaume kutoka kwa watoto wao
 
naongea kwa experience naiona kwenye familia nyingi, Watoto wakienda kusalimia wazazi mama akiwa peke yake mzee kasafiri wanaweza kukaa hata siku nzima, baba akiwepo watoto watakaa nusu saa tu washapotea, Mama ndie anapewa hela za misaada watoto wanamwambia ampe mzee kiasi anachoona kitamfaa.

Wazazi wa kiafrika tumekuwa wakoloni sana na hili ndilo linasababisha hata watoto wetu wakiwa wakubwa wanakuwa huru zaidi ya mama zao, kumsaidia mama, kumpa pesa mama, n.k. kuzidi wewe uliepambana kuwalisha, kuwasomesha, kuwavisha, n.k.

Nani kakwambia kuwa baba lazima uwe mkali mkali tu kugombeza, kutoa kipigo, n.k. hii kitu itawaharibu sana watoto wako kisaikolojia.

Wengi wanadhani mtoto akiwa mkubwa anasahau lakini wanakosea sana, kisaikolojia unakuwa umeweka permanent damage.

Tangu mtoto akiwa mdogo jaribu sana aujue upande wako positive anaoweza kuuona kwa macho yake, huko mihangaikoni ni kweli tunapambana lakini hawawezi kuona wala kujua jinsi unavyotafuta pesa. ni kazi bure na hutaweza kuchukua points mbele ya mama yao wanaemuona live anavyowajali hata kama anashinda nyumbani muda wote hana kazi.

Usisubiri wawe wakubwa, hilo ni kosa kubwa, utakuwa kama mgeni, kumbuka mama yao kaanza kubond nao tangu kichanga, na wewe usiwe nyuma sana jitahidi walau akiwa na miaka miwili muanze kubond.

watoe out
Fundisha kuendesha gari
waletee vizawadi
cheza nao games, n.k.

Ni kweli inabidi uwe strict kwenye future yao lakini usisahau ku enjoy nao present muda mlionao kabla hawajawa wakubwa.

Kwenye kutoa adhabu hakikisha unamshirikisha mke wako wote mgawane points.

Jiepushe kuwa baba ambae ukisafiri, watoto wanajisikia amani na furaha.
JIDANGANYE.
 
Mnakoelekea na huo mnaoita uzungu hakuna tofauti ya mama na baba ndani ya nyumba, huo ni uzwazwa..... matunda yake sio matamu wala halisi.
 
Kizazi cha wababa wakoloni bado kipo kweli??? Kama wapo basi wamezeeka ukoloni unaishilia......walikua kina baba na nusu 👍

Kimeingia kwa kasi ya kimbunga kizazi cha watoto wasioishi na baba "zaa nitalea" kizazi cha mama ni mama, mama ni baba....hatari.

Sijui madingi wa baadae watakuaje hata.
Let’s wait and see😂
 
Attachments

  • Screen_Recording_20240510-054145_Facebook.mp4
    23.4 MB
Nimegundua swala la kukaa karibu na familia hasa watoto mpaka bondi ikubali kama wenzetu wazungu ni tabia ya ndani sana ya kuzaliwa na ucha Mungu ndani yake.

Kuna broo mmoja yeye kila siku anarud home watoto washalala na siku akiwatoa ni anawapeleka kama swimming anawabwaga na kulaza mshale kurudi anawaitia pikipiki ....imeisha hiyo
Duuhh, kwamba yuko busy au hawapendi wanao?
 
Hao watoto wamefika hapo kwasababu ya hao Baba zao- Sasa kama mtoto hautotambua umuhimu wa Baba yako kwenye maisha yako huo utakuwa ni upunguani wako Mwenyewe especially kama na wewe Sasa umeshakuwa Baba na una mke.

Lastly wanaume tuandae uzee wetu-hii kutegemea mke na watoto ndiyo wakutunze uzeeni naona imekaa kimtego sana.
Mwanaume usiamini kama mkeo/mwanamke wako atakuja kukuthamini ukishazeeka-sahau huo ndiyo muda wao wa kukukomesha kwa chuki zote.
 
Ujamuelewa mtoa mada....point yake sio kutunzwa na mtoto point ni ukizeeka muda mwingi watoto wako watakuwa karibu na mama na hata simu ikipigwa akiongea na mama ataongea nae muda mwingi kuliko ww baba ingawaje mtoto anakuwa anakuheshimu kama kawaida...sasa hili ttzo lazima liwe linakutesa kwa kuona watoto wako hawakupendi kumbe ni ule unonko wako na ukali wako wakati wapo watoto ndio umesababisha....urafiki kwa watoto ni muhimu.
 
asante kwa kufafanua vizuri mkuu,
 
Nadhani wewe ndiyo hujanielewa.
 
Back
Top Bottom