Kim Atangulia Singapore Kumsubiri Trump

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
korea+pic.jpg

Pyongyang, Korea Kaskazini. Kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong Un anatarajiwa kuwasili leo nchini Singapore kwa ajili ya mkutano wa kihistoria kati yake na Rais Donald Trump wa Marekani uliopangwa kufanyika Jumanne, vyombo vya habari vimesema.

Shirika la habari la Reuters lilinukuu chanzo kimoja kikisema kuwa Kim anatarajiwa kusafiri hadi katika uwanja wa ndege wa Changi, Singapore leo Jumapili.

Juhudi za Reuters kutaka kupata uhakika kutoka mamlaka za usafiri wa anga Singapore ziligonga mwamba baada ya kukataa kuzumgumzia safari hiyo ya Kim.

Kim na Trump pamoja na mambo mengine watajadili ajenda ya kuondoa silaha za nyuklia katika Rasi ya Korea na kwamba rais huyo wa Marekani anatarajiwa kumtaka Kim kuachana na uundaji wa silaha hizo.

Wakati Kim akijiandaa kuwasili leo kwa ajili ya mkutano huo wa kihistoria, viongozi wakuu wa nchi zilizoendelea zaidi kiviwanda duniani (G7) Ijumaa walianza mkutano wa siku mbili nchini Canada ambao mada kuu ni biashara duniani na Korea Kaskazini.

Mkutano huo ulifanyika Charlevoix katika jimbo la Quebec lililopo mashariki mwa Canada.

Biashara huru na uchumi wa dunia ilikuwa mada kuu katika siku ya kwanza. Mkutano huo unafuatia hatua ya Rais Donald Trump kuendelea na msimamo wake wa kulinda masoko ya ndani,ushuru wa forodha katika bidhaa za chuma cha pua na alumini uliowekwa na utawala wa Trump umeifanya Marekani kutofautiana na mataifa mengine ya G7.

Katika kikao cha jana Ijumaa, vyanzo vya habari vilisema kuwa Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe aliwaambia viongozi wenzake kuwa majibizano ya vikwazo vya kibiashara ya papo kwa papo yataathiri uchumi wa dunia kwa kiwango kikubwa na hayatamnufaisha mtu yeyote.
MCL
 
Hivi kwa mfano ikatokea kuwa kipindi hiki Kim Jong Un yuko safarini vp Marekani hawawezi kuivamia Pyongyang kwa makombora ya kushtukiza.??
 
Nasubiriaaaaaa kuona kitakachojiri.. Trump aende tu.. tuyaone.. tuwasikilize
 
Kiprotokali hii imekaaje? Dogo lazima atangulie kumsubiria rais. Ingekuwa kinyume chake ingekuwa maajabu. Na Trump ataondoka atamwacha hotelini Singapore. Anyway, Kiduku naye akasafishe macho huko duniani.
 
Walimuomba atangulie ili waamini kama mkkutano upo maana Babu Trump angeweza kutaangulia au kuanda safari dogo amwambie nimesogeza siku mbele!
 
Ni Nani Alieomba Huu Mkutano?Nataka Nijue Nani Mnyonge Na Nani Mbabe
 
Hivi kwa mfano ikatokea kuwa kipindi hiki Kim Jong Un yuko safarini vp Marekani hawawezi kuivamia Pyongyang kwa makombora ya kushtukiza.??

Kwa hiyo Pyongyang yeye ndo analipua mabomu Korea ya kujikinga kwa hiyo atakiwi kusafiri? na kama ni hivyo Marekani naye kama Trum hayupo nani atalipua? akili za Kitanzania ndo hizi jaman!
 
Hivi kwa mfano ikatokea kuwa kipindi hiki Kim Jong Un yuko safarini vp Marekani hawawezi kuivamia Pyongyang kwa makombora ya kushtukiza.??
Kuna mambo ambayo hayawezi kufanyika maana utasababisha nchi zingine kupata uhalali wa kuisaidia North Korea. Nchi kama Russia na China zinaweza kupata uhalali huo.
Hata kuua Rais wa nchi pia ni jambo ambalo haliwezekani kufanywa kwa sababu hizo hizo. Ingekuwa rahisi hivyo basi Assad wa Syria angeshakufa.
 
Kiprotokali hii imekaaje? Dogo lazima atangulie kumsubiria rais. Ingekuwa kinyume chake ingekuwa maajabu. Na Trump ataondoka atamwacha hotelini Singapore. Anyway, Kiduku naye akasafishe macho huko duniani.
Unazungumziaje hatua ya Kim kusitisha mpango wa kukutana uliopangwa hapo awali kabla ya mkutano huu wa keshokutwa? Utampa Mr.Kim jina gani hapo kiprotokali.? Dogo acha mahaba ya kijinga kwenye mambo ya kimsingi.
 
Hayo mazungumzo yao sijui Kama yatapata muafaka
Huyu anataka nyuklia iteketezwe huyu hataki kusikia
 
Back
Top Bottom