Ni kweli kabisa mkuu, tumekuwa tunalima kwa mazoea sana. Yaani kila mmoja mahindi au mbaazi. Mimi kuanzia msimu ujao nitaanza kufocus na kilimo cha high valuable crops kama maharage, vitunguu na nyanya. Najua yana changamoto nyingi sana lakini nitapambanazo.
Nyanya Lima off season hapo unapiga pesa
 
Wadau kama kichwa cha topic kinavyosema, shauku kubwa la mim kuja hapa ni kutaka kupeana uzoefu wa kilimo cha vitunguu maji kw misimu ya hiv karbun kutokana na nyuz zlzomo jukwaani kuwa za miaka mingi iliyopta mfn 2010! Mambo yamebadlika Sana kipind kile unakuta mtu anazungumzia kuuza gunia kwa elfu 60;
Karibuni kwa michango
1. Aina ya mbegu inayotoa vitunguu vizur vya saiz ya Kati
2. Gharama ya mbegu za kutosha hekari moja
3.Gharama ya uendeshaji
4.Changamoto.
5.Makadrio ya mapato yazingatie misimu ya mauzo ya wastan tustamanishane kwa kutajiana Bei kubwa kumbe uhalisia haupo vile.
N:B Niko sehemu inamito isyokauka na mashamba na miliki mwenyewe ispokuwa wenyeji wamebweteka hakuna aliyeiona hii fursa! Kusini kumenoga.
Karibuni kwa mawazo.
Nipo hapa
 
Ah ah apo kwenye kulinda unakuwa na bati au dumi akiwa anakuja kwenye shamba unapiga maana Tembo apendi kelele lkn inabidi muwe kuanzia watu watutu na kuendelea maana ukiwa mmoja unakuwa mfu mtalajiwa
Tembo wa kule wameshindikana mpaka wanatumia askari kwenda kuwafukuza Kwa bunduki. Hapo ndio una fika unatamani bwana AK arudie tu kufanya kazi yake 😂😂 ili wapungue
 
1. Mbegu nzuri: red bombay

2. Gharama ya mbegu heka 1: 300k

3. Gharama ya uendeshaji kwa heka: 1.5
million ikiwa shamba la kukodi, kulima,
mbolea, madawa kumwagilia, kuotesha
n.k)

4. Changamoto
●Wadudu,
●ukungu,
●uhaba wa mvua (kwa wanaotegemea mvua)
●Magonjwa
●Sio kila eneo unaweza kusitawisha
vitunguu ukapata mazao mazuri

5. Wastani wa bei kwa gunia la debe 6: 70k mpaka 400k (inategemea na msimu
mfano mwaka huu e gunia hadi
400k)

Heka 1 inaweza kutoa hadi magunia 100 ikitunzwa vizuri
Nimependa Kuna. Rafiki yangu alilima hekaa 4 alitumia 12mil kaja kuvuna 60mil
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom