Kilimanjaro: Walimu wauza Rasilimali zao kupata pesa za uhamisho

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
9,059
15,737
Walimu zaidi ya 50 kutoka Katika shule za msingi zipatazo 46 katika Tarafa mbalimbali Wilayani Rombo, Mkoani Kilimanjaro wamelazimika kuuza Rasilimali zao kama vile mbuzi, kuku na baadhi ya vitu vya ndani na wengine kuingia kwenye mikopo ili kuweza kupata pesa kwa ajili ya kujihamisha wao pamoja na familia zao baada ya kupata barua za uhamisho na kutakiwa kwenda kuripoti katika vituo vingine vya kazi.

Walimu hao wamedai ya kuwa walipata barua za uhamisho na kutakiwa kuripoti Katika vituo vyao vip ya vya kazi mnamo tarehe 8 mwezi wa pili (2) Mwaka huu lakini baada ya kuripoti kazini waliahidiwa kulipwa stahiki za uhamisho mapema iwezakanavyo lakini Hadi sasa ni miezi Minne (4) imeisha Bila kupata chochote.

Baadhi ya shule hizo ni pamoja na Shule ya Msingi Urauri, Mashima, Kafumbu, Kibaoni, Nanjara na Samanga.

Baadhi ya Walimu hao ambao hawakupenda kutaja majina yao wamedai Kuwa malalamiko yao tayari walikwisha peleka Kwa Afisa Utumishi, Afisa Elimu pamoja na Mkurugenzi.

Lakini Majibu wanayopewa Kila wakati hayaridhishi kwa kuambiwa kuwa mfumo unasumbua ndo maana pesa haijatoka.

Walimu hao wamedai kufanya kazi katika mazingira Magumu kutokana na kuwa madeni mengi.
 
Makonda ni kiongozi wa watu wasio na akili kama wewe.
SEMA MAKONDA BOMAYEEEEEEEE...........RAIS 2030
Screenshot_20231102_120808_Remix.png
 
Kule wilaya ya Kilindi mkoani Tanga kuna walimu watano ambao walihamishwa kwa uhamisho wa dharura kwakuwa shule yao ilihamia Handeni kutokana na badiliko la mipaka tangu November 2023 hawakupewa usafiri wala stahiki zozote na wanatishiwa kufukuzwa kazi wasiporipoti au kugoma laana iwe juu yao wote waliohusika na uonevu huu.
 
Wilaya ya chemba Dodoma

Pia inahilo tatizo walimu toka mwaka Jana 2023 wamehamishwa hawajalipwa stahiki zao..Hela zinapigwa za uhamisho jamn idara sekondari ,,mkurugenz wasaidie walimu wanyonge wanapigwa Hela zao
 
Back
Top Bottom