Kilichotokea baada ya kuwaweka kuku rangi

View attachment 519149
Nilipoeleza changamoto ninayoipata kuhusu ndege ambaye wadau mmeniambia anaitwa kipanga wengine mlinishauri kuwapaka Rangi kuku, Nimelifanya hilo zoezi na huu ni mrejesho 'feedback'

1. Juzi ilikuwa ni miongoni mwa siku ambazo kama mwehu
nimejikuta nikicheka peke yangu kwani baada ya kuwapaka
ile rangi wa kwanza kuwakimbia alikuwa mama yao, pia kuku
wengine walilazimika kukimbia banda baada ya kuwaona vifaranga
wale wa Rangi rangi kwani nimewapaka rangi za njano, kijani, nyekundu
na bluu.

2. Nimegundua kunguru anawaogopa sana wale kuku, nakusudia
hawa kunguru wenye baka jeupe shingoni.

3. Bado sijapata uthibitisho kama kipanga hatawakamata ingawa kwa
mwewe ambaye leo nimemuona akizungukazunguka hajashuka kuwakamata.

4.Zoezi limesababisha kifo cha kifaranga mmoja, kwani yupo mtetea aliamua
kupambana na vifaranga kwa nguvu kubwa akijua ni maadui, kwa sasa amewazoea
na nmejifunza mara nyingine haitatokea

Ahsanteni wadau kwa ushauri.

dah nimejikuta nacheka mwenyewe we jamaa ni shidaaa
 
subiri wiki ipite hao kunguru watakuwa wameshapata majibu ya maswali yao.. Utaisoma namba!
hahaha!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom