Kilichomlazimisha Rostam kula matapishi yake ni hiki

Wanajamvi:

Nimekuwa najiuliza ilikuwaje Rostam kutinga Igunga katika kampeni za CCM na huku alishasema hataki tena 'siasa uchwara' za CCM? lakini baada ya kutafakari sana inakuwaje mtu huyu mwenye jeuri kubwa sana ya pesa (alizotuibia) kula matapishi yake mwishowe nikajikuta nina jibu: huenda ni kwa sababu alitishwa na vyombo vya dola vinavyomilikiwa na serikali ya CCM, vyombo ambavyo mara kadha vimekuwa vikitumika ili kuwaweka viongozi mstarini.

Navyoona mimi Rostam alitishwa kwamba akishikilia kukipa mgongo chama hicho basi huenda vyombo vya sheria vikaanza kumshughulikia kwa dhati kutokana na ufisadi na wizi wake. Akajikuta hana namna isipokuwa kupiga magoti na kula matapishi yake.

Mtindo huu CCM wanautumia sana katika kujiweka mstarini.
Hawa jamaa wanafikiri wanaongoza maiti kama kipindi cha Tanu. safari hii ataumbuka mtu,tusubiri matokeo.
 
Wanajamvi:
Nimekuwa najiuliza ilikuwaje Rostam kutinga Igunga katika kampeni za CCM na huku alishasema hataki tena 'siasa uchwara' za CCM? lakini baada ya kutafakari sana inakuwaje mtu huyu mwenye jeuri kubwa sana ya pesa (alizotuibia) kula matapishi yake mwishowe nikajikuta nina jibu: huenda ni kwa sababu alitishwa na vyombo vya dola vinavyomilikiwa na serikali ya CCM, vyombo ambavyo mara kadha vimekuwa vikitumika ili kuwaweka viongozi mstarini.

Navyoona mimi Rostam alitishwa kwamba akishikilia kukipa mgongo chama hicho basi huenda vyombo vya sheria vikaanza kumshughulikia kwa dhati kutokana na ufisadi na wizi wake. Akajikuta hana namna isipokuwa kupiga magoti na kula matapishi yake.

Mtindo huu CCM wanautumia sana katika kujiweka mstarini.

Hapana Mkuu, hapa umekosea tena sana, waliolazimika kula matapishi yao ni CCM. Ni CCM waliompigia magoti Rostamu awaokoe baada ya kuonja ladha ya joto la uchaguzi Igunga. Kama kawaida Rostamu alitoa masharti kadhaa na CCM licha ya awali kudai imemtema imewabidi wammeze Rostamu mzima mzima na naamini huko ndiko kula matapishi.

  1. Sharti moja kubwa alilolitoa Rostamu ni pamoja na jina lake kusafishwa mbele ya wapiga kura wa Igunga na mtu wa kufanya hiyo kazi awe ni katibu wa Uenezi, Nape Nnauye aliyekuwa kinara wa kumchafua.
  2. Sharti la pili ni kuwa atahudhuria uzinduzi wa kampeni Igunga kama atakuwapo kigogo moja wa juu kabisa wa CCM na mtu huyo mtu awe Raisi mwenyewe, Jakaya Mrisho kikwete au mwakilishi wake.
  3. Sharti la tatu kubwa ni kuwa serikali ya CCM imhakikishie atafaidika vipi kimaslahi kama atakubali kuwapakata huku wakiwa wameshamnyea.
Hatua zilizochukuliwa na CCM:
  1. Sharti la kwanza lilitimizwa kwa Nape Mnauye aliyekuwa kwenye kifungo cha kutokukanyaga Igunga haraka haraka alifunguliwa na kutumwa awahi huko kusafisha jina lake Rostamu na kweli alifanya hivyo.
  2. Sharti la pili lilileta tafrani kidogo lakini baadaye iliamuliwa kuwa Kikwete asiende Igunga ila awakilishwe na si mwingine bali Raisi Mstaafu Benjamin William Mkapa na Rostamu, kwa shingo upande, aliridhia.
  3. Sharti la tatu limetekelezeka pia na tetesi zipo kuwa haraka haraka fedha zilitafutwa (mabilioni !) na kampuni ya Caspian ya Rostamu imefaidika kwa namna moja au nyingine.
CCM na Rostamu ni kama pete na kidole na pete lenyewe limeganda kidoleni kiasi kwamba kulivua itabidi kukata kidole kizima. Rostamu ni kama tawi walilokalia CCM na kulikata ni sawa na kuanguka kwa CCM. Rostamu ni kama hewa ya oxygen anayopewa mgonjwa mahututi (CCM) ambaye yuko ICU na kumwondoa ni sawa na kuitoa uhai CCM.
 
Ccm na viongozi wake wana akili kama za kuku zinafikiria hapo zilipo tu hazijui kesho kwani walimpiga vita na leo ndo wanamtumia kwenye kampeni na wanaigunga hawajaliona hili bado wanakusanyika na kuwasikiliza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom