Olumolongez
JF-Expert Member
- Dec 19, 2015
- 818
- 299
kama mtanzania na mwana JF mwenye ubinadam nimeona leo niwakumbushe wenzangu kuhusu hili balaa japo najua mnajua.
wanasema ushuhuda ni moja ya mawaidha.. leo natoa ushuhuda:
1. Mwaka 2001 nikiwa darasa la nne, Dada alikufa kwa UKIMWI. aliacha watoto wawili. Nikasema aaaah, dada nae alikua mcharuko sana, kila mtoto na baba yake!!!!
2. Mwaka 2003 nikiwa darasa la sita, Baba yangu mdogo alikufa kwa UKIMWI. Aliacha mjane na mtoto mmoja. Nikasema tena aaaaaah, huyu nae tatizo machimboni Mwadui kule.. mzembe
3. Mungu si Athuman, mwaka 2009 nikiwa nasubiri selection niende 4m5 BABA YANGU mzazi alifariki kwa UKIMWI. Daaaaah, alituacha mie, mdogo wangu wa kike na mama yetu wa kambo (mama mzazi waliachana miaka 19 iliopita).
Mwaka 2013 (miaka 4 after father passed) mama wa kambo akatuaga nae kwa UKIMWI baada ya kuzembea matumizi ya ARV.
So sad kwa kweli. Ugonjwa nilokua nasema kuupata uzembe ukaja kuni prove wrong ndan ya familia yetu.
NDUGU ZANGU.. UKIMWI UPO NA UNAUA... TUWE MAKINI...
Yaaani wewe jamaa story zako bwanaAsante mkuu umenikumbusha mbali sana. Mwaka 1996 niliomba baba anipeleke Sengerema hospital nikahasiwe (niwe kama ng'ombe maksai) ni baada ya kushuhudia mjomba akifariki nikiwa naishi nae kipindi hicho hata ARV tulikuwa tunazisikia Kenya. Ni zaidi ya wana ukoo 16 wameshaondoka ukiacha mbali marafiki niliosoma nao. Anyway asante kwa kutukumbusha japo ukimwi kwa sasa tunachukulia kama malaria tu.
Kabisa mkuuHapa comments chache ungepost story ya mapenzi ndo ungeona mrejesho...asante kutukumbusha maana watu siku hizi vidudu vinatuwasha balaa
Mkuu pole sana hili janga kwa sasa inaonekana ni kitu cha kawaida sana ila tunashukuru mtoa mada kwa kutukumbushaMwaka 2007 Dada yangu alipima baada ya kuugua mara kwa mara akakutwa kaathirika ila aliwahi kutumia ARVs yupo mpaka sasa, mwaka 2008, baba yangu naye baada ya homa zisizokwisha alipima akakutwa ameathirika mwaka 2009 akafariki, familia ilijawa sana na majonzi kwani tulijua mama naye tayari, alipoenda kupimwa naye akakutwa nao akafariki 2012, mwaka Jana mtoto wa dada naye kaktutwa nao. UKIMWI unaua jamani siye uliovamia kwenye familia zetu ndo tunajua
Sent using Jamii Forums mobile app