Kisu Cha Ngariba
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 22,135
- 48,821
Kawaida yake uyo. Kilazza wa LumumbaDah! Wewe jamaa lazima unaishi maisha magumu sana Tanzania, maana kila ukiandika chochote unakera kwa kauli zako ovyo. Kwanza fahamu hii kauli ya serikali sio kwa nia ya kumfanya kila Mkenya awe mwanariadha wa kutajika, ila ni kuwafanya wanafunzi wetu wawe wakakamavu na sio kama ilivyo Dar kila kijana ameishia kwenye chips mayai na beer.
Mambo ya kuoana au kutooana hayahuasiani na ukakamavu, Waswahili huwa hamkosi vijisababu uchwara. Mnataka kutwa mcheze pool na bao huku mkiwa na vijisababu vya kila aina. Ina maana nchi zote zinazofanya vizuri kwenye riadha wanaoana wao kwa wao. Ukienda Marekani unakuta weusi wenyewe hata hawajui asilia yao, labda hata Msukuma kaoa Myoruba lakini wapo sawa kwenye riadha.
Kidogo uwe unashirikisha ubongo na unachokiandika maana watu wengi wanapitia na wataishia kusoma huo ujinga wote.
Serikali yetu imebuni hii mikakati ya kuhakikisha kila mwanafunzi anachakarika na kuwa mkakamavu. Iwe ndoto yake ni udaktari, urubani wala nini, lakini lazima akimbie. Haya mambo yelikuwepo nikiwa mdogo, sijui yalipungua vipi baadaye. Nakumbuka tulikua tunakimbia wote, tena ilikua ni sharti.
Ni kama tu jinsi Magufuli kwenu ameweka kauli usafi lazima ufanyike kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi, japo mlivyo wavivu mnalalamika hadi kero.