Kikwete siyo safi! - yes I said it!

Umeanza tena! naona hujipendi. Waache wale wala wali wale wali wao!

Bi senti 50, sijui kama ni upeo wangu mdogo ama ni aje, lakini ina maana hapa JF una kazi ya kufuatilia (monitor) anachoandika Mkuu Mwanakijiji, and then ummediately unapost 'kumtahadarisha'? Naomba uniwie radhi (na wanaJF wengine pia) kwa vile ni off topic lakini kwangu sio kitu cha kawaida, aidha una mapenzi mazito dhidi ya maslahi ya Mwanakijiji, aidha...aidha..aidha.....
 
Sijui kwanini tunazungushana na kudai watu wote walioatajwa kwenye orodha ya Ufisadi wanastahili isipokuwa Rais Kikwete! Hata viongozi wanaotambua baadhi ya uzito wa tuhuma zilizotolewa na wanaodai kuwa zitiliwe maanani hujikuta wanajing'ata ng'ata kuhusu Rais Kikwete. Baadhi ya watu wamefikia mahali pa kulaumu kina Dr. Slaa kumuweka Kikwete katika kundi hilo kwani JK ni safi! Hata hivyo ushahidi wote uliopo unaonesha kuwa JK siyo safi na yeye ndiyo awe wa kwanza kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake!

a. Mkataba wa IPTL ulisainiwa yeye akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Hakuna mkataba mbovu kama huo. Kushindwa kwake kutetea maslahi ya nchi akiwa Waziri na kulisababishia Taifa hasara kubwa ilikuwa ni kilele cha kutokuwajibika na kushindwa kuongoza. Akiwa Waziri mwenye dhamana ya nishati Ndg. Kikwete alitakiwa kuhakikisha kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano inaingia kwenye mkataba ambayo inaweza kujitoa pasipo kupata adhabu kubwa. Alishindwa hivyo na hivyo kuoneshe kutokuweza kusimamia maslahi ya nchi.

b. Wakati Rada ya bilioni 50 inanunuliwa, Ndg. Kikwete alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Uhusiano wa Kimataifa na wakati sakata lenyewe linaanza alikuwa ni Waziri wa Fedha. Akiwa Waziri mwenye dhamana hiyo alishindwa kabisa kufuatilia ukweli kuwa kampuni ya BAE siyo mali ya serikali ya Uingereza na ya kuwa rada yenyewe ilikuwa imeongezwa kwa asilimia 24. Kiasi hicho kinakaribiana kabisa na wastani wa asilimia 20 za fedha za umma zinazopotea katika manunuzi ya serikali (public procurement).

Alishindwa kuhakikisha kuwa maslahi ya Taifa letu yanalindwa na alipopata nafasi ya kuonesha busara aling'aka na kusema "kwanini sisi ni idara ya Benki ya Dunia? ni kututukana kudai kuwa tusubiri Benki ya Dunia kutuamulia nini kinatufaa".

Ndio maana leo hii anapokuja na kuzungumza kuwa hawezi kuamini kuwa nchi kama Uingereza inaweza kuacha kampuni "yake" kurusha rada hiyo kwa bei hiyo wengine tunamshangaa kwani alikuwa na nafasi zaidi ya 20 ya kuweza kupinga ununuzi huo lakini alikuwa ni kinara wa kutetea tenda hiyo ya rushwa! Ni kuelewa hilo ndio utaona ni kwanini hakutaka watu wamuulize Rais Mkapa juu ya suala la rada, kwani miongoni mwa wahusika wakubwa ni yeye mwenyewe Kikwete.

c. Kama nilivyoonesha hapo juu kuwa Rais Kikwete aliwahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini. Kwa hivyo nina uhakika kabisa alikuwa anajua kabisa jinsi mikataba inavyoingiwa na alikuwa na kila sababu ya kuhakikisha kuwa mikataba inalinda maslahi ya nchi na kunufaisha nchi wakati inawapatia wawekezaji faida ya kibiashara. Kwa kitendo chake yeye mwenyewe kuwa ukaribu na wafanyabiashara hao hasa swahiba wake ambaye ni mmiliki mkubwa wa ardhi yenye vito na madini Bw. James Sinclair, Rais Kikwete tangu akiwa Waziri wa Nishati na Madini na baadaye Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje amekuwa mtu aliyetiwa upofu na "dhahabu".

Wakati Rais Mkapa na Yona wanajipatia tenda ya Kiwira, Rais Kikwete na Msabaha walikuwa wanajisogeza karibu na Kampuni ya Tanzania Royalty Exploration ambapo kuna madai (yanayothibitishwa na taarifa za SEC na EDGAR) kuwa Msabaha na Kikwete walikuwa na "hisa" za kiasi fulani. Kampuni hiyo ya TRE iliingia mkataba na Barrick Gold kuwa inapovumbua madini katika ardhi inayomiliki basi Barrick wanakuwa wanunuaji wa kwanza.

Ni wao TRE waliouzia Buzwagi kwa Barrick na maeneo mengine kadhaa kwa makampuni mengine. TRE inaponufaika kwa mikataba mibovu ambayo serikali inaingia na makampuni ya uchimbaji kuna watanzania wawili ambao nao wananufaika (ni wazi wapo wengine na wengine ni vigogo wengine) na dili hizo.

Ni kwanini Barrick walikuwa wa kwanza kukubali mabadiliko ya vipengele vya mikataba yao? jibu ni ushawishi wa James Sinclair na Kikwete ili kutetea kilicho chao. Kwa yale makampuni ambayo hayana ukaribu wa James Sinclair na Kikwete (JK alimualika JS kwenye kuapishwa kwake na mara nyingi amekuwa mgeni wake akija US, na binti ya JS aliyeko Tanzania ni rafiki wa karibu...) basi imekuwa vigumu kuwashawishi kubadili vipengele hivyo.

Ndio maana hadi leo hii si kweli kuwa kupitia vipengele na kuzungumza na "wakubwa" hao kuhusu mikataba kumekoma kama alivyodai mjasiriamali mwingine Nazir Karamagi alipokuwa akijaribu kupangua hoja za Zitto. Ukweli ni kwamba kamba waliitundika wenyewe serikali na ni wenyewe walioziweka shingo zao humo! wawekezaji wanatishia kuondoa kigoda!! Serikali inabembeleza!!

Anapozungumzia matatizo ya mikataba Rais Kikwete anazungumzia kana kwamba tatizo ni kipengele kimoja tu! Hajachukua muda kufuatilia uzito wa hoja hizo kwani kwake ni kelele!

d. Kikwete si Safi kwani amewalinda watu wachafu! Waswahili walisema ukiwa na urafiki na wezi, usishangae watu wakakuhisi na wewe mwizi! Rais Mkapa anapomlinda mjasiriamali Mkapa, aliposhindwa kumsimamisha kazi mara moja Ditto na kuamua kumuacha ajiuzulu huku akiendelea kupata mafao yake alionesha udhaifu mkubwa wa uongozi!

Rais Kikwete amekuwa mtetezi wa wabadhirifu akikesha kutoa vitisho hewa akijaribu kutetemesha mabua na kuangusha vichuguu huku milima ikiendelea kuganda theluji! Ukimya wake kama ule wa Mkapa ni ishara wazi kuwa walifeli darasa la Mwalimu!

Anapoona kuwa madai ya ubadhirifu Benki Kuu, matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu, n.k kuwa "kelele za upinzani" na kuwa "ndiyo demokrasia" anaonesha udhaifu mkubwa usiomstahili kiongozi wa nchi. Haiwezekani upotevu wa mabilioni ya fedha, matumizi mabaya ya madaraka kuwa viwe ni "kelele" tu!

Rais ni lazima we mtu ambaye hapuuzii masuala mazito na hayafanyi kuwa ni ya kijinga. Kwa mtu kuwa mpinzani hakuifanyi hoja yake kuwa "kelele". Leo hii wana CCM wenzake wanazungumza wazi kuhusu tuhuma hizi na kudai kuwa wanaotuhumiwa (akiwemo yeye mwenyewe) wajibu siyo suala la kupuuzia!

e. Rais Kikwete ameonesha na anaendelea kuonesha udhaifu mkubwa wa maamuzi hasa kwa kuwa mtu wa kusita sita na ambaye yuko tayari kutumia uwezo wake wote kutofanya lolote. Hivi hadi nini kitokee ndipo Rais Kikwete atajua kuwa mambo haya si ya kupuuzia? Wakati Lowassa ameenda kukutana na Karamagi kule London na mkataba wa Buzwagi ukasainiwa je Rais Kikwete alifahamu ujio wa Waziri wake Mkuu? Je walikutana? Kama Rais hakujulishwa kutiwa saini kwa mkataba mkubwa namna hiyo na Waziri Mkuu anakutana na Waziri mwingine pasipo ujuzi wa Rais je haoni ni ukosefu mkubwa wa kiutawala!? Lowassa alifuata nini London na kukutana na Karamagi badala ya kukutana na Rais?

Leo hii watu wakihoji mazingira ya kusainiwa mkataba huo kwanini hiyo iitwe kelele!

Tanzania imefanya kosa kubwa kumchagua Kikwete. Kosa hilo vizazi vijavyo vitasimulia kama hadithi, kuwa "hapo zamani za kale kulikuwa na mwana CCM mmoja ambaye aliwapo watu matumaini sana kabla ya uchaguzi. Watu wengi waliamini kuwa mwanaCCM huyo ndiye atakuwa mkombozi na kiongozi wa kuwaonesha njia ya kufikia nchi ile ya ahadi. Walipomchagua kwa asilimia 80 ya wapiga kura, Watanzania walijawa na matumaini... Miaka miwili baadaye watanzania walishika vichwa vyao kujuta, kwani waliyemdhania ndiye kumbe siye... !! "....

Kama Rais Kikwete hatabadili mwelekeo wa uongozi wake, na kama ataendelea kufanya kazi kana kwamba madai na hoja zinazojengwa ni "kelele" tu na hivyo kuendelea kufumba macho ufisadi unaoendelea nchini (na hapa simaanishi rushwa ya kutoa na kupokea tu, namaanisha matumizi mabaya ya madaraka, n.k) basi ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha kuwa Rais Kikwete hapati nafasi ya pili ya kutoitumikia Tanzania. Endapo atagundua upotofu wa uongozi wake na kusahihisha mapema ndani ya miezi sita ijayo yawezekana akajiokoa na kuukoa urais wake. Vinginevyo, Rais Kikwete atakuwa ni Rais wa kwanza kutawala kwa mhula mmoja!!

Rafiki zake wezi sasa wewe ulitegemea nini?
 
Mkuu MMJ,

Heshima mbele mkuu, binafsi bado sijafikia kumuweka rais wa sasa Muungwana, kwenye listi ya wafisadi au wezi, na viongozi wabovu wa taifa letu,

Urais ni kazi nzito sana, inayohitaji kutumia busara kabla ya kufanya maamuzi muhimu ya taifa, ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza kwa makini washauri wake wa kuitawala na kisiasa, pamoja na kisheria, mambo ya kukurupuka yalituponza taifa tukawalipa mamillioni lukuki watu fulani wa benki kuu, enzi zile za Mkapa, tumewalipa mamillioni lukuki ndugu wa Kombe, kutokana na kurupu kurupu,

Mkataba wa IPTL, tuliletewa na Lowassa, akishirikiana na Kolimba, Radar tuliletewa na Mramba, kwa kushinikizwa na marafiki wa Mkapa, kuwa na hisa kwenye kampuni tumekubaliana hapa forum kuwa sio tatizo, tatizo ni kama walizipata hisa hizo kwa haki, na wanaendelea kuzimiliki kwa haki na kufuata sheria zote zetu za nchi kuhusiana na hizo hisa,

Tuhuma zilizotolewa ni nzito, hilo halina ubishi, rais amesema serikali inachunguza mdai hayo, pia tumeambiwa na Spika kuwa yeye binafsi ameyafikisha malalamiko ya kina Slaa kwa mwanasheria mkuu, naye anasubiri majibu, recentlty tumeambiwa na waliotuhumiwa kuwa, wanajitayarisha kwenda mahakamani, na sasa hivi tunawasikia viongozi wengi wa CCM, hata Kingunge, wakijitokeza kuwa majibu yanatakiwa,

Kumbuka hii ni mara ya kwanza Tanzania kama taifa tumejikuta na ishu nzito kama hii, so far ni vyema kuwa na subira, binafsi siamini bado kuwa Muungwana, ni mchafu au si safi kama ulivyosema, ninaamini kuwa kinachomsumbua ni lack of experience na urais, na siasa za taifa kwa ujumla, he was good kwenye kampeni, lakini kwenye urais bado kunamtatiza kidogo,

Lakini kwamba yeye ni mchafu, hapana hilo labda kuwepo na ushaidi zaidi ya uliokwishatolewa tayari, Muuungwana hana mali za kutisha, hana majumba, wala mahekalu, hana magari wala mashamba, I mean mnyonge mnyongeni the man is poor kwa standards za marais wengine wa Afrika, au hata mstaafu wetu,

Binafsi bado niko radhi kusubiri, na sijafikia hatua ya kuamini kuwa Muungwana ni mchafu, just because hasikilizi mob justice, hapana urais una maadili yake na miiko yake, na busara zake tofauti kabisa na busara za kuwa upinzani kwenye siasa za taifa, au hii forum,

Mkuu sawa ni haki yetu wananchi kuonyesha outrage zetu kuhusiana na tuhuma za mafisadi, lakini bado ninampa benefit of the doubt rais Muungwana, maana hii hukumu na charges ulizozitoa ni nzito mno kwa mkuu wa nchi na kisiaa pia, ambaye amekuwa madarakani for only 23 months.

Aahsante Mkuu, na Wakuuu Wote Waliochangia Hiii Topic!
 
mzee mwenzangu, kanuni kadhaa za uchafu zinasema hivi:

a. Mwenye kuchezea uchafu, naye huchafuka
b. Kuupaka uchafu rangi na kuunyunyiza marashi, hakubadili ukweli kuwa bado ni uchafu.
c. Aliyechafuka mikono, na aliyechafuka shati, na yule ambaye ni viatu tu vimechafuka kwenye uchafu ule ule wote ni wachafu, hawachekani.
4. Ni vigumu kumwambia mtu mchafu asafishe wachafu wenzake!
 
Mie nasubiri hiyo j5, nione hiyo makala gazetini ya muheshimiwa saana al maarufu Mkjj kabla sijatoa comments zangu.
Msee ES, kazi ya Urais sio kama ufundi bomba, uselemara au kazi nyingine ambazo unaweza ku-learn on the job!!!. Urais ni kazi inayotaka vision kabla hujaingia kazi.........mie na kila sababu ya kutaka kuwa mshabiki wa muungwana, lakini huyu bwana ni hapendeki ni vigumu kuona hayo mazuri alofanya!!. Miezi 23 ni more than extended honeymoon, ni muda tosha kabisa wa kuwa na visible results.....tusubiri miaka 5 itaisha na atasema kwamba muda haukutosha.
Mengine yalojiri over the weekend bwana ES ni kuwa Redsox wameingia kwenye world series against rockies, game one wed @fenway park. lingine ni Louisiana imejagua Governor wa kwanza asiye mweupe since reconstruction naye ni Bobby Jindal (Republican), age 36. American born Indian, parents immigrated to USA from New Delhi,India.
 
ila alichosema mzee mwenzangu FMES kimenifanya nibadili mambo mawili matatu kwenye makala ya Jumatano
 
mzee mwenzangu, kanuni kadhaa za uchafu zinasema hivi:

a. Mwenye kuchezea uchafu, naye huchafuka
b. Kuupaka uchafu rangi na kuunyunyiza marashi, hakubadili ukweli kuwa bado ni uchafu.
c. Aliyechafuka mikono, na aliyechafuka shati, na yule ambaye ni viatu tu vimechafuka kwenye uchafu ule ule wote ni wachafu, hawachekani.
4. Ni vigumu kumwambia mtu mchafu asafishe wachafu wenzake!

Mkuu ninakusikia sana, lakini pia subira huvuta heri ndugu yangu, ukweli ni kwamba viongozi wetu wamepigwa na butwaa kama sisi wananchi,

Nafikiri Mkuu Zitto, atanisaidia kwenye hili, jinsi wabunge walivyopigwa na butwaa kule bungeni, siku alipomwaga vitu kuhusu Karamagi, yanayotokea sasa hivi ni mabadiliko ya kisiasa, ambayo mwana-adam siku zote hapendi kubadilika, kwa hiyo wakuu ndio ni lazima tupinge kelele, lakini pia tuwape nafasi pia viongozi wetu kuitafakari situation!

Mkuu YRSMN,

2.
Urais ni kazi inayotaka vision kabla hujaingia kazi.........mie na kila sababu ya kutaka kuwa mshabiki wa muungwana, lakini huyu bwana ni hapendeki ni vigumu kuona hayo mazuri alofanya!!. Miezi 23 ni more than extended honeymoon, ni muda tosha kabisa wa kuwa na visible results.....tusubiri miaka 5 itaisha na atasema kwamba muda haukutosha.

I know, lakini pole pole tu rais wetu atafikia tu, nafikri umeona hotuba moja ya Mwalimu, ambapo anasema kuwa yeye alifanya makosa makubwa tena mengi kwenye kipindi chake cha urais cha miaka 23, kwa sababu hawakuwa na experience, kama alivyosema Kada kuwa tusubiri kidogo, subira yavuta heri!

Mkuu hii kitu ya Red Sox, nimeizimia, hao wanaonekana watachukua hiyo ubingwa, maana Big Papi, Manny na huyo mkongwe Shillingi, hao ni hatari sana, na huyo Mjapan Igawa kweli Rockies wataweza hao, naona this time ni moja kwa moja, au?
 
Mkuu FMES,

Ninakubaliana na hoja zako na ufafanuzi wako kuhusiana na JK. Tatizo langu kwa JK ni moja, kama yuko serious na hayo anayotuambia kwamba yanafanyiwa uchunguzi kwanini amekuwa anatoa kauli zinazopingana kila kukicha?

Akiwa nje ya Tanzania anasema tuhuma zinafanyiwa uchunguzi na kwamba report ikishakuwa tayari na ikagundulika kwamba tuhuma ni za kweli basi wahusika watachukuliwa hatua zinazopaswa (rejea majibu ya swali la BoT alipoulizwa na Condy Rice na pia hotuba yake kwa mapadri walio Vatican). Akiwa ndani ya nchi the very same person na baadhi ya wapambe wake wanasema tuhuma hizo siyo za kweli ni kelele za wapinzani wanaotaka madaraka kwa njia za kuleta vurugu (rejea hotuba yake ya sherehe za kuzima mwenge majuzi pale jijini Arusha, yaani tofauti ya chini ya wiki tayari mtu anasema kitu kingine kabisa). Kama anadai kwamba tuhuma hizo siyo za kweli ama ni uzushi, je, wamechunguza lini na kugundua kwamba tuhuma hizo siyo za kweli? Kama ni PCCB or whoever anafanyia kazi uchunguzi huo halafu mtu kama JK au EL akatoa statement hiyo huoni kama anaweza kuwa ana influence findings za tuhuma hizo? Kauli ya Rais au Waziri Mkuu ni nzito sana, na ndiyo maana kwenye katiba mambo yako wazi kwamba swala likiwa mahakamani serikali au Bunge halitakiwi kuliongelea. Ndiyo kuna baadhi ya cases mawakili huwa wanaomba mahakama itoe amri kwamba vyombo vya habari visiwe vinaongelea ili kupunguza uwezekano wa ku-influence hukumu ya case. Sasa wao wenye dola wakisema kwamba tuhuma hazina ukweli unategemea PCCB watakuwa na nguvu ya kuzinguza wakati Boss wao kasema hakuna kitu?

Tatizo langu kwa Mkuu wa Kaya (JK) ninaona kama vile hayuko serious. Ni vyema akawa na msimamo mmoja wa aidha kusema uchunguzi unafanywa na kuwaambia wananchi wasubiri matokeo. Au aseme hizo ni kelele za wapinzani na kwamba anazipuuza, halafu tujue moja kwamba Rais wetu hataki kupambana na ufisadi kwa vitendo bali kwa maneno ya kisiasa majukwaani.

Tukirudi kwenye kasheshe ya Spika wa Bunge, hivi tangu lini Mwanasheria Mkuu wa Serikali anafanya kazi ya kuchunguza documents ambazo zinakuwa submitted Bungeni. Mwanasheria Mkuu wa ni Mbunge (nadhani ni ex-off.), ndiyo anapewa hizo documents azipitie ili iweje? Ana ujuzi wa kuchunguza kama hizo documents zina utata au la? Jamani mbona haya mambo tunayapeleka kisiasa sana? Sitta mwanzoni alisema angepeleka hizo documents polisi, baadaye Bwana Foka akasema atazipitia hizo documents na then atamshauri Spika ziende wapi. Finally, wakasema zitaenda kwa mwanasheria mkuu wa serikali, sasa sijui anachunguza nini? Maana claim ya Sitta ilikuwa kwamba documents hizo zilikuwa zimegushiwa, na hivyo alitaka polisi wachunguze kama ni documents halisi, hapo ndipo palipo na mkorogo. Sasa Bwana Mwanyika anafanya huo uchunguzi au anaangalia namna ya kupangua hoja na evidence za Slaa kisheria ili kuisafisha serikali yake ambayo yeye ndo mtetezi wake kisheria?
 
ila alichosema mzee mwenzangu FMES kimenifanya nibadili mambo mawili matatu kwenye makala ya Jumatano

Gazetini weka yenye mabadiliko, hapa mie naomba utuletee original isiyo na mabadiliko. Ameen

Msee ES,
Nimesoma pongezi zako kwa Chissano kule kwa thread nyingine, umesifia mambo yanayotokea Mozambique toka enzi za Samora(RIP), Chissano na aliyepo sasa...........makosa alofanya Nyerere yalikuwa yanatosha, baada ya hapo ilibidi TZ iwe mwendo mdundo kiuchumi, elimu, afya na kadhalika na sio watu wanakuja with the same ol' excuse ya kutokuwa na experience ya kutosha. I really think hiyo excuse ni nzee kama kinguge na ni joke kwa politicians wetu hasa raisi kuendelea kuhitumia.

Mjepu anaitwa Daisuke Matsuzaka also known as Dice-K, he is good but alikuwa yupo hyped. Anayefanya sana mavituz ni Josh Beckett, I hope they don't win kwani wakishinda itakuwa chaotic hapa kijijini.!!! just kidding.
 
Mkuu ninakusikia sana, lakini pia subira huvuta heri ndugu yangu, ukweli ni kwamba viongozi wetu wamepigwa na butwaa kama sisi wananchi

Hiyo BOLD partly inaweza kujibu hoja kwamba kwanini JK anajikanyaga kanyaga na baadhi ya viongozi wetu wamekuwa wakitoa majibu yanayopingana. Nadhani la msingi alitakiwa akae kimya kabla ya kuanza kusema hiki na kile, na hivyo kutupatia picha tofauti sisi wananchi. Tunashindwa kumwelewa kwamba yuko wapi!
 
Mzee Mwanakijiji,
samahani kidogo kuhusu JK nimekuja dakia katikati hapa bila kupitia maelezo ya wengi walionitangulia.
Ikiwa JK alikuwa na scandal zote zile na zilifahamika kabla hata hajaupata Urais imekuwaje nyioe waandishi na wanasiasa wengine nyote mlikaa kimya na kutuweka kizani hali mkifahamu JK sio msafi hata kidogo!.
Kama utakumbuka sisi wengine tulisema hatumfahamu JK kwa kiasi hicho zaidi ya kugongana naye sehemu sehemu. Na sikuthubutu kutoa comment zozote zaidi ya kutaja chaguo langu ambalo lilikuwa Salim ama Warioba kwani hawa niliwafahamu zaidi ktk Uongozi na pia nilifahamu ni watu wenye msimamo, mtazamo upi.
Zaidi ya hapo mjomba mbona unatuongezea machungu zaidi!...
Je, hii sio dalili tosha ya kuwa viongozi wetu ni reflection yetu wenyewe!
 
Hata hivyo ushahidi wote uliopo unaonesha kuwa JK siyo safi na yeye ndiyo awe wa kwanza kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake!

kaka hapa jiandae kutoa ushahidi wa uchafu wa mkuu, maana hii sasa siyo allegetion tena bali ni aina fulan ya comfirmation ya uchafu wenyewe. angalia wasije wakakutoa kafara mkuu,ukawa wewe ndo wa kwanza kufikishwa huko kwa wanaogawa haki, ili utetee haki yako ya kuendelea kuwa mtu huru

Tanzania imefanya kosa kubwa kumchagua Kikwete

Hii itaonekana kama unadhamiria kumu "undermine" mkuu nashauri utumie kile tunachokiita TAFSIDA , yaani kupunguza ukali wa maneno bila kuharibu ujumbe,

Anyway ni makala nzuri ila jaribu approach ya kiuungwana , kusema jk, hajui kuongoza, kucomfirm moja kwa moja kuwa ni fisadi, bila kumpa advantage of doubt (kutokana na ukubwa wa cheo chake), mimi nadhani sometimes soft power na hard power inabidi itumike kumtoa nyoka pangoni
 
"Tanzania imefanya kosa kubwa kumchagua Kikwete"

Ingekua vizuri kama kosa hili lisingekuja kurudiwa.
 
Umeanza tena! naona hujipendi. Waache wale wala wali wale wali wao!

Hivi kama huna cha kuandika kwanini hunyamazi kama mimi?
Lazima mtu uchangie tuu hataka kama huna la kuchangia jamani!?

Mweh! Watanzania kweli hatutaendelea.
 
Hata hivyo ushahidi wote uliopo unaonesha kuwa JK siyo safi na yeye ndiyo awe wa kwanza kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake!

kaka hapa jiandae kutoa ushahidi wa uchafu wa mkuu, maana hii sasa siyo allegetion tena bali ni aina fulan ya comfirmation ya uchafu wenyewe. angalia wasije wakakutoa kafara mkuu,ukawa wewe ndo wa kwanza kufikishwa huko kwa wanaogawa haki, ili utetee haki yako ya kuendelea kuwa mtu huru

Tanzania imefanya kosa kubwa kumchagua Kikwete

Hii itaonekana kama unadhamiria kumu "undermine" mkuu nashauri utumie kile tunachokiita TAFSIDA , yaani kupunguza ukali wa maneno bila kuharibu ujumbe,

Anyway ni makala nzuri ila jaribu approach ya kiuungwana , kusema jk, hajui kuongoza, kucomfirm moja kwa moja kuwa ni fisadi, bila kumpa advantage of doubt (kutokana na ukubwa wa cheo chake), mimi nadhani sometimes soft power na hard power inabidi itumike kumtoa nyoka pangoni


Kwenye makala ya J'tano nimefanyia mabadiliko kidogo unajua ninapoandika mara ya kwanza huwa naandika vinavyonijia wakati huo ila ninapokaa na kuanza kutafakari zaidi najikuta nabadilisha kidogo hata mwisho wa makala utakuwa tofauti na mwisho wa mawazo ya hapa JF...
 
Mzee Mwanakijiji,
samahani kidogo kuhusu JK nimekuja dakia katikati hapa bila kupitia maelezo ya wengi walionitangulia.
Ikiwa JK alikuwa na scandal zote zile na zilifahamika kabla hata hajaupata Urais imekuwaje nyioe waandishi na wanasiasa wengine nyote mlikaa kimya na kutuweka kizani hali mkifahamu JK sio msafi hata kidogo!.
Kama utakumbuka sisi wengine tulisema hatumfahamu JK kwa kiasi hicho zaidi ya kugongana naye sehemu sehemu. Na sikuthubutu kutoa comment zozote zaidi ya kutaja chaguo langu ambalo lilikuwa Salim ama Warioba kwani hawa niliwafahamu zaidi ktk Uongozi na pia nilifahamu ni watu wenye msimamo, mtazamo upi.
Zaidi ya hapo mjomba mbona unatuongezea machungu zaidi!...
Je, hii sio dalili tosha ya kuwa viongozi wetu ni reflection yetu wenyewe!

tatizo la waandishi wengi nikiwamo mimi ni kutotofautisha majukumu yetu (kufanya uchunguzi na kuripoti) na badala yake kupigwa na mwanga wa ujiko wa Kikwete kiasi cha kwamba watu walikuwa wanafuatilia mwitikio wa wananchi kwa Kikwete badala ya kujaribu kuonesha alikuwa ni mtu wa namna gani. La pili ni kuwa vyombo ambavyo vilikuwa vikali kiuchunguzi tayari vilikuwa mikononi mwao na wakati ule hakukuwa na watu ambao walithubutu kuandika vikali. Nikiwaonesha makala yangu ya kupongeza ushindi wa CCM mnaweza kunisikitia...!!
 
Back
Top Bottom