Kikwete kosa kubwa ni kumpa Magufuli chama, utanikumbuka

Hii nchi imefikia hapa tulipo kwa sababu ya Ufisadi, tukifanikiwa kuuzika ufisadi nakwambia lazima nchi ipige hatua, na kama Magufuli anaweza kupambana na ufisadi basi anatufaa shida yetu ndani ya miaka hii kumi ni kupambana na ufisadi kweli kweli ili kila mtu ajue wizi haulipi kiasi ya kwamba kizazi kijacho kiishi kwenye misingi ya kuogopa wizi

Mwenzetu sijui unatumia Shisha iliyotengenezwa na nini. Hivi, nani amekwambia Magufuli ataongoza kwa miaka 10? Kana kwamba hakuna uchaguzi? Kakwambia atagombea 2020? Acheni mazoea someni katiba.
 
Hii nchi imefikia hapa tulipo kwa sababu ya Ufisadi, tukifanikiwa kuuzika ufisadi nakwambia lazima nchi ipige hatua, na kama Magufuli anaweza kupambana na ufisadi basi anatufaa shida yetu ndani ya miaka hii kumi ni kupambana na ufisadi kweli kweli ili kila mtu ajue wizi haulipi kiasi ya kwamba kizazi kijacho kiishi kwenye misingi ya kuogopa wizi
Hivi kweli Mwisenge1993, tatizo kubwa la nchi hii ni ufisadi?
Ina maana tukiweza kuondoa ufisadi tu maisha yatakuwa mazuri?
 
Na bado ni kuogopa kutumbuliwa tu kunawasumbua wengi, hakuna lingine.

Apewe anyooshe, mazoea yafeeee sababu na pesa za umma wengi wanatumbua tu ovyo
 
Kwa kuwa hakuna chuo kinachofundisha uenyekiti wa chama, apewe tu atajua la kufanya mwenyewe.
 
HAWA hapa makatibu wakuu wa CCM;Horace Kolimba,Laurence Gama,Philip Mangula,Yusuph Makamba,Wilson Mukama na Abdulrahman Kinana.Ina maana hata hii historia fupi asiijue?
 
mkuu kajina kako kanafanania kile ulichoandika. mzaliwa wa kwanza wa ccm lazima amalizie safari yake misri, hawezi vuka bahari ya shamu. majira mapya na mambo mapya
 
Bado nafikiria tu, kwa akili ya kawaida Jakaya Kikwete anamkabidhi vipi Joseph Pombe Magufuli chama? Yaani sababu kubwa ni kwamba eti ni utaratibu toka mwanzo?Pamoja na jinsi JPM anaongoza nchi kwa utaratibu huu bado Jakaya Kikwete haoni tu?

Tunampa vipi mtu chama wakati hata jukumu la nchi tulilompa bado ni shida? Yaani kila siku yeye anajifunza tu. Chama ni zaidi ya serikali, chama ni mama, Serikali ni mtoto wa chama, na Serikali huongoza kupitia chama.

Bado naendelea kuvuta picha, yaani haingii akilini kabisa kumpa mtu chama ambaye hujui hata historia yake. Nina hakika ukimwuliza Magufuli akutajie makatibu wakuu wa 5 wa chama waliopita hatoweza, hata taratibu nyingi cha chama hazijui.

Please JK just be serious, dont make a mistake. Be strong, lead the party until you find its the right time for Magufuli
Wakati mwingine watu waondokane na ndoto za mchana Magufuli ni: (1) Rais wa nchi, (2) Amirijeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, (3) Kiongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (4) Mwenyekiti wa baraza la mawaziri. Na dunia yote inamtambua hivyo.

Haiingii akilkini kwamba mtu aliyeaminiwa na Watanzania wanaokaribia milioni hamsini ati atashindwa kuongoza CCM chama chenye wanachama wasiozidi milioni mbili. Serikali inaweza ikawepo na kuendelea na utendaji wake hata kama CCM haitakuwepo, lakini kamwe CCM haiwezi kuwepo kama serikali haipo. Tumeshuhudia CCM katika uhai wake ikibadirisha viongozi na watendaji wake. Wakati mwingine wametuletea watendaji hadi tunajiuliza kuhusu weredi wao, lakini pamoja na mapungufu hayo yote hatukuona chama kushindwa katika chaguzi mbalimbali.

Kubali usikubali CCM imeimarika zaidi baada ya Magufuli kuingia madarakani, tulishafika mahali watendaji wa chama wakaishutumu serikali kwamba baadhi ya mawaziri iliyowaweka ni mizigo na bado pamoja na kuwa na baadhi ya mawaziri mizigo bado chama kimeshinda katika uchaguzi. Mwenyekiti aliyepo amebakiza si zaidi ya miaka miwili ya kuwepo madarakani kulingana na utaratibu wao, ikifika mda huo watafanyaje kama wanadhani Magufuli hawezi kuongoza chama. Kiongozi mmoja mwandamizi wa chama kishasema kuwa ndani ya CCM kuna majipu, nadhani alikuwa anambip Magufuli ajiandae kuyatumbua, na hiyo hakika ndiyo shughuli yake ya kwanza anayokwenda kuanza nayo mara baada ya kukabidhiwa rungu.

Habari ya Magufuli kukabidhiwa uongozi wa juu wa chama ni mshituko mkubwa kwa wale waliozoea kutafuna fedha za chama. Mara kwa mara tunamsikia Rais akisema nchi hii ni tajiri na haipashwi kuwa omba omba. Sasa tunangoja kusikia Mwenyekiti akisema chama hiki ni tajiri na hakipashwi kutegemea kwa asilimia kubwa ruzuku kutoka serikalini. Ushauri wangu kwa wale wote ndani ya chama wenye mtizamo kama wa huyo jamaa hapo basi ni sharti WAJIANDAE KISAIKOLOJIA maana ni hakika Magufuli is just around the corner.
 
Mbona mmeanza kugeukana nyie kulikoni...kila zama na.........wake jamani msisahau
 
Mkuu nchi inamatatizo zaidi ya ufisadi.
Kuondoa ufisadi ni swala moja lakini kujua dira ya kuwaletea watu maendeleo na unafuu wa maisha ni suala jinginee.

Utaletaje maendeleo na unafuu wakati kila kitu kinachotwa na mafisadi? Hao waliotangulia mbona hawakuleta hayo maendeleo? Unakula ugali bila kunawa mikono..
 
Dhambi nyingi ulizotenda ndiyo zimekufanya uwaze haya tena koma kabisa tuache na jpm wetu endeleeni na Lowasa lenu,
 
Watanzania wengi mmezoea chai chai sasa ngoja mfundishwe jinsi ya kuishi kudadekiiiii
Thikamoo JPM
Nilipokua sipo Tz nilikua nafatilia kweny mitandao sasa naona laivu laivu watu wazembe saaana yani
Nchi zilizoendelea hawajahi kuwa hv na kusubr maendeleo
No pain No gain
Hakuna lisiloshindikana ila hakuna kitu kinachopatikana kirahis
Ndo maisha
 
Hahahaahha huu mtifuano ni wa Magamba wenyewe kwa wenyewe!! Kazi ipo, Vita vya panzi hivi....
 
Karibu mwaka sasa hajamaliza kuunda serikali yake
Mpeni chama apoteze miaka mingine miwili,tena ampe Bulembo ukatibu mkuu atufunze kutukana badala ya siasa,wanaendana

Mkuu umeongea point kubwa sana ambayo nimesahau kuiandika
 
Back
Top Bottom