Kikwete Atafanya Mabadiliko Karibuni

ndugu yangu shalom, nimekukosea nini?

nnaona huishi kuniandama? au ndio mapenz tu hayo kwangu? maana maapenzi yana mambo
 
hii sawa na ile

"kuna jamaa alikuwa akimuomba mungu sana ampe mali, lkn kila siku akawa maskini, mwisho akaamua kutukana na kusema wewe mungu gani huna lolote hata huwezi kunipa millions dala huna jeuri hiyo,sasa kuna swahiba yake akamuuliza baada ya maombi yake mbona unakufuru, akajibu nnamchonga ukali mungu anipe".

sasa hii ni sawa na kumchonga ukali Jk abadilishe baraza sawa sie tunaangalia kitachofuata


JK ni binadamu,tena mwenye uwezo mdogo wa kufikiri,usimkuze kiasi hicho,ni Kingwendu tu.
 
Nafikiri hata yeye anajua kwamba mambo hayaendi vizuri sasa anachosubiri ni nani awawajibishe hao walioshindwa kufanya kazi vizuri na hii ndio ilimfanya Nyerere aache kazi ya kuajiriwa ili awatumikie wananchi na sasa kweli wafanyabiasha na uongozi wapi na wapi? watafanya kipi kwanza?
 
Wazee, nionavyo mimi, sikio la kufa halisiki dawa. JK hatafanya mabadiliko, wale ambao wangemwambia mzee hali ni mbaya ndio hao wanaompaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Naogopa kama wana JF watakuwa na fikra kuwa JK atafanya mabadiliko, speed ya kujadili uozo huo yaweza kupungua.Tutaamini tu pale hayo mabadiliko yatakafanyika. 'Aluta continua'
 
Kufanya mabadiliko sio tatizo, je akina nani watakaoziba hizo nafasi...maana ukiangalia bunge letu naona asilimia kubwa ya wabunge ni kama mawaziri waliokuwepo tuu isitoshe wote ni washikaji.(Bird of a feather....)
 
...uzembe na rushwa vinaimaliza Tanzania na uzembe unaanzia kwa Raisi kwa kuachia mambo ya kipuuzi puuzi yaendelee
 
Mh. Rais
naomba kutoa maoni yangu binafsi kuhusu mabadiliko unayotaka kufanya,awali ya yote nakupa pole kwa kusumbuliwa na watu kama msabaha,karamagi,EL na bado unawakumbatia tu,najua unasoma lama za nyakati sababu utakuwa umechoshwa na safari unazopangiwa kila siku ili kuzima mambo.

baada ya kusema hayo mie sitaki mabadiliko ila nataka nataka baraza la mawaziri lipunguzwe.kuna haja gani wizara zingine kuwa na manaibu waziri?kama pale nMiundombinu ambao hakuna jambo la maana linalofanyika..kwa mfano bajeti ya mwaka huu hawana hata project mpya ya ujenzi wa barabara ,wizara nyingine ni wizara ya habari na wizara ya kilimo na chakula..wizara ya kazi na vijana naomba mkuu uiguse.

Mhe. Jk nakusihi sana uwang'oe mtandao maslahi wako mzee kabla wananchi hawajaamua kukung'oa wenyewe hapo 2010 kwa kura.

Mh. naomba kukwambia umaarufu wako umeshuka sana na unachangiwa n uswahiba wako na hawa watu wanopenda kuona watanzania wanataabika.
 
mwache aendelee na jeuri yake wa kumng'oa sasa hivi wanamsubiri tuu 2010 na kiendelea hivi hata wakiiba kura haitawasaidia maana itakuwa ni tsunami!
 
khali ishakuwa mbaya sana,umeona mbeya walivyomzomea EL na kumshabikia Mwandosya,hii ni sababu tosha upepo si mzuri.namshangaa muungwana anaposema hatishwi na watu wanomuita fisadi,hiki kiburi anakitoa wapi???au ho waganga wake ndio wanompa kiburi?? na kwanini JK haendi Mbeya lakini mwanza anaenda kila baada ya miezi mitatu?huko mbeya hakuna shughuli za maendeleo.
 
Ndani ya miaka yote miwili imepita hakuna kitegauchumi chochote alichobuni JK bali ni kuzurula tu kuomba misaada hii ni aibu sana. Namshauri JK akae nyumbani atulie afanye tena ziara za kila wizara aangalie kama aliyowapa wafanye kipindi kile cha kutembelea wizara yamefanyika au la? na sina uhakika aliwaambia wafanye nini ila alikuwa akiwaambia fanyeni!!

Si ajabu baada ya miaka miwili ijayo rushwa ikaisha automatically maana hakutakuwa na na kitu tena cha kula rushwa maana hakutakuwa na pesa, hakuna mradi kama barabara kujengwa ili mtu aonekane kama anakula rushwa ou la.
saccos alianzisha mkapa
TRA mkapa
Mkukuta mkapa
Mkurabita mkapa
Takuru mkapa
TIC mkapa
Tanroad mkapa
Ukaguzi wa madini mkapa
Etc
JK kaanzisha nini hata kimoja? miaka miwili tayari hiyo bado 8.

Wasiwasi ni kwamba pesa itaisha miradi itasimama kama ilivyosimama ya barabara, daraja la kigamboni, ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma, na sasa ujenzi wa shule unaelekea huko huko!
 
Hivi kuna watu bado wan hope na muungwana?? Wananchi waige mfano wa Kenya, jamaa wako serious! Kibaki sasa yuko hoi, kachoka, cheo kinamponyoka. Bongo 2010 utaona SISIEM inashinda kwa kishindo. Mambo ya bongo bwana!!!
 
JK kaanzisha nini hata kimoja? !
kaanzisha vifuatavyo
1.Mradi wake wa kujenga nyumba pale Mwanza eneo la luchelele
2.kaoa mke mwingine mwezi wa pili
3.kaanzisha mikataba ya kutudumaza kama Buzwagi
4.Kaanzisha usanii wa kujibu hoja za watanzania.


kwani unadhani Muungwana ana uwezo wa kuanzisha chochote?wewe tangu lini Ari Mpya ,Kasi Mpya na Nguvu mpya ikawa vision yake?
 
Jamani mwenyezi Mungu anisamehe,hakuna waziri ambaye namchukia kama kapuya,kamuamisha mzee wa watu pale oysterbay kisha kampeleka katika nyumba za jumuia za shirika la bandari,nyumba hiyo ipo oysterbay sehemu inaitwa morogoro stores jirani kabisa na kona ya kuja hospital ya macho ya ccbrt,

Mwana Siasa
Message ya kuhamishwa huyo Mzee imenigusa sana unataka kuniambia ametimuliwa kutoka katika nyumbake kwa mabavu kama ni hivyo hayo ndiyo matumizi mabaya ya madaraka na hao wamekuwa wakifanya hivyo hivyo kwa wanyonge, bila shaka utakumbuka PM aliyepita alipoamua kununua eneo kubwa sana almost 1/3 ya Dar kama sikosei pale Kibaigwa nadhanialikuwa anataka kuwa Kabaila mmoja siku zijazo, lakini nashukuru kelele zetu sasa zimeanza kulipa hata sisi mabubu tunaongea japo kwa jazba mradi meseji iwafikie.
 
khali ishakuwa mbaya sana,umeona mbeya walivyomzomea EL na kumshabikia Mwandosya,hii ni sababu tosha upepo si mzuri.namshangaa muungwana anaposema hatishwi na watu wanomuita fisadi,hiki kiburi anakitoa wapi???au ho waganga wake ndio wanompa kiburi?? na kwanini JK haendi Mbeya lakini mwanza anaenda kila baada ya miezi mitatu?huko mbeya hakuna shughuli za maendeleo.

SIYO MWANZA BRO! HIVI UNAJUA JK NA EL WAMEENDA ARUSHA MARA NGAPI TOKA WAPATE NCHI!? LABDA MGANGA WAO YUKO HUKO! NI ZAIDI YA MARA NANE KILA MMOJA NA JE WAJUA WAKIWA HUKO WANACHANGUISHA CHINI YA SH?

SI CHINI YA MILIONI MIA KILA WAKIENDA HUKO?

JE WAJUA WAKEINDA MIKOA MINGINE WANACHANGI KIASI GANI? JK ALIWAHI TOA MILIONI MOJA TU HUKO KUNA WILAYA MOJA SIITAJI ALIONNYESHWA SHULE LAKINI YEYE ALITOA MILIONI MOJA TU TENA WILYA MASIKINI! LAKINI INA MADINI DHABU KIBAO.
 
bubu msema ovyo,

huyo mzee aliyeamishwa alikuwa anafanya kazi wizara ya michezo na utamaduni enzi hizo kapuya na mudhihiri walikuwa mawaziri(awamu ya tatu),huyu mzee alikuwa ni mhasibu hapo makao makuu ya wizarani ,na amekuwa akiishi hapo oysterbay kwa takribani miaka 10 sasa katika nyumba yake hiyo ya serikali,gafla zile nyumba za serikali zikauzwa,na yule mzee akafanikiwa kuinunua nyumba ile,lakini haikuchukuwa muda mrefu(MIEZI MIWILI)mzee yule akastaafu kazi,so kapuya alichoamua kufanya ni kutumia madaraka yake aliyo nayo kumuhamisha kumpeleka katika maghorofa ya bandari yaliyopo chole road masaki na kisha yeye kuichukua nyumba ile ,hivi sasa kapuya ameporomosha bonge la mjengo hapo ndani,na inasemekana kuwa yule mzee alitaka kuipeleka ishu hii mahakamani ila alichibwa bit la kufa mtu,ikabidi awe mpole kwa kwenda maghorofani kwa shingo upande
 
kaanzisha vifuatavyo
2.kaoa mke mwingine mwezi wa pili
3.Kaanzisha usanii wa kujibu hoja za watanzania.


kwani unadhani Muungwana ana uwezo wa kuanzisha chochote?wewe tangu lini Ari Mpya ,Kasi Mpya na Nguvu mpya ikawa vision yake?

Kama angelikuwa na Professional ya EL (BA Arts specil. Kucheza Ngoma) ningemuelewa kuwa yuko kwenye Mazoezi lakini yeye ni BA econ. Au kuna magnetics inatoka kwa EL kumwendea nini?
 
Nimesikia pia kuwa kuna mabadiliko. habari zinatoka kidogo kidogo. Sijui kama ni za kweli. Kama hizi za Wassira kuwa Waziri Mkuu Mpya on 16th November. Inawezekana ni spinning by some section katika mtandao.
Lakini kwa dalili za sasa mabadiliko yapo
 
Back
Top Bottom