tibwilitibwili
Senior Member
- Sep 12, 2006
- 184
- 10
Hatimaye Kikwete Afanya Kweli
Na Mwandishi Wetu
Rais Jakaya Kikwete ameanza mchakato wa kuhakikisha nyumba za serikali zilizouzwa kwa watumishi wake wakati wa uongozi wa Awamu ya Tatu, zirejeshwa serikalini.
Habari za uhakika kutoka baadhi ya maofisa waandamizi serikalini zinasema Rais Kikwete ameamua kuzirejesha nyumba hizo katika mikono ya serikali kwa kuzinunua upya kutoka kwa watumishi waliokwisha kuzinunua.
Kwa mujibu wa habari hizo Rais Kikwete ameiamuru Wizara ya Miundombinu kufanya tathmini ya kina ya ununuzi wa nyumba hizo kubaini ni kiasi gani kinastahili kurejeshwa kwa wote walionunua nyumba hizo ili hatimaye zirejeshwe Serikalini.
Inaelezwa ya kuwa kitakachotathmiwa ni kiasi gani cha fedha kilichokwisha lipwa na kila aliyenunua, ikizingatiwa ya kuwa si wote ambao wamekwisha kumaliza kuzilipia nyumba hizo.
Habari ndani ya Wizara ya Miundombinu zinaeleza ya kuwa waliozinunua watatakiwa kuzirejesha na kulipwa kiasi ambacho kila mmoja alikuwa amekwishalipa kwa mujibu ya mikataba waliyopewa.
Inaelezwa kwamba Rais Kikwete ameamua kuzirejesha nyumba hizo Serikalini kwa vile hivi sasa Serikali inakabiliwa na uhaba mkubwa wa nyumba kwa watumishi wake wanaoteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali na wanaohamishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Kwa sababu hiyo serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuwapangisha katika hoteli wafanyakazi wengi wapya wanaokosa nyumba katika maeneo wanayopangiwa kufanya kazi, kimesema chanzo chetu cha habari.
Sababu nyingine ni kwamba Serikali imeona kwamba nyumba hizo bado zinatakiwa kuendelea kubakia katika mikono ya serikali kwa sababu ziko katika maeneo yaliyotengwa na maalumu kwa ajili ya viongozi na watumishi wa Serikali.
Chanzo chetu cha habari kilisema kwamba tathmini ya nyumba hizo imeanza kufanywa na Wizara ya Miundombinu ambayo itawasilisha ripoti yake kwa Rais Kikwete kwa ajili ya utekelezaji.
Waziri wa Miundombinu, Basil Mramba hakuweza kupatikana kwa njia ya simu kwa vile anafuatana na Waziri Mkuu Edward Lowassa katika ziara Mkoani Kigoma.
Naibu Waziri wa Miundombinu Dk Makongoro Mahanga alipoulizwa hakukataa wala kukubali kuhusiana na suala hilo.
Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa nyumba za serikali zilizouzwa nchi nzima tangu mwaka 2002 ni 6,000.
Mauzo ya nyumba hizo yalikuwa yakifanywa kwa awamu na Wakala wa Nyumba za Serikali chini ya Ofisa Mkuu Mtendaji wake, Togolai Kimweri.
Serikali ya awamu ya Tatu ilisema wakati huo ya kuwa fedha zilizopatikana zingetumika kujengea nyumba nyingine kwa ajili ya watumishi wa serikali katika maeneo mbali mbali kama Dar es Salaaam, Arusha, Dodoma na Mwanza.
Baadhi ya nyumba hizo zimekwisha kujengwa Dar es Salaam kwa ajili ya maofisa waandamazi wa Serikali wakiwamo Mawaziri.
Uchunguzi unaonyesha ya kuwa wakati Kikwete akidhamiria kuzirejesha nyumba hizo Serikalini, baadhi ya watumishi wa Serikali waliozinunua wamezifanyia ukarabati.
Wengine wamejenga nyuma nyingine ndani ya viwanja vya nyumba hizo ambavyo ni vikubwa, yaani ‘low density'
Vivyo vivyo wengine wamepangisha kwa makampuni binafsi na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs) na nyingine zimejengwa maduka ya biashara na ofisi kwenye uzio wa nyumba hizo, hususan zilizopo karibu na barabara.
Uuzaji wa nyumba hizo za Serikali ulioanza mwaka 2002 ulisababisha malumbano na mzozo mkubwa miongoni mwa watanzania, wakiwamo viongozi wa vyama vya siasa, baadhi wakipinga kuuzwa kwake.
Baadhi ya wananchi na viongozi wa vyama vya siasa walionyesha masikitiko yao kwa hatua ya kuuzwa nyumba hizo, hasa kwa bei ndogo, wakisema haikulingana na thamani na tathmini ya nyumba na viwanja vya nyumba hizo, kwa pamoja.
Wananchi pia walitaka uwepo uwazi wa majina ya watumishi waliouziwa nyumba hizo na bei waliyonunulia, jambo ambalo Serikali ilikataa kulitekeleza.
Serikali ya Awamu ya Tatu ilisisitiza kuziuza nyumba hizo, ikisema itakuwa ikijenga nyingine kutokana na malipo ya ununuzi wa nyumba hizo.
Miongoni mwa walionunua nyumba hizo ni mawaziri wengi, kama si wote, wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu, hasa katika Mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma, kwa kuwa walikuwa wakiishi katika nyumba hizo.
Chanzo: Mtanzania Jumapili Toleo Namba 3784
- Aagiza Nyumba za Serikali Zilizouzwa Zirejeshwe