Kikuu vs AliExpress

Sory naomba kujua AliExpress na Alibaba ni kitu kimoja au tofauti?
Kikuu na Jumia yupi ni bora katika kuhakikisha bidhaa unaipata haraka
alibaba ni baba wa aliexpress, pia uagizaji wa mizigo alibaba ni tofauti kidogo na wameweka ka kwambi ni mizogo mikubwa ama mingi zaidi ila aliexpress unaweza nunua hata sindano moja tuu

kikuu wanata china na nahisi wanafanya drop shipping aliexpress ila jumia nao hawanatofauti sana na kikuu wao wanachukua mizigo yao kwenye store za watu mbalimbali hasa hapo kariakoo kulingana na mahitaji ya wateja wao, wao hawana store zao useme wanatoa kwenye godown lao.
 
Jumia tz ni ya humu humu Ila kikuu inachukua na vitu kutoka nje au Ina order bidhaa China ,,pia Alibaba hao nu B2B yaan wanawauzia wateja wa jumla jumla Ila AliExpress hao ni B2C platform wanawauzia consumer moja kwa moja kaks
Sory naomba kujua AliExpress na Alibaba ni kitu kimoja au tofauti?
Kikuu na Jumia yupi ni bora katika kuhakikisha bidhaa unaipata haraka
 
Ahsante kwa ufafanuzi sijawahi kununua bidhaa mitandaoni juzi nikajaribu kuingia ALIBABA kununua bidhaa cha kushangaza bei ya bidhaa ni USD 11 shipping cost ni USD 117 mpaka Sasa hivi sijaelewa inakuwaje shipping ni gharama kiasi hicho
mkuu kunavitu vingi yafaa uvijua katika biashara ya mtandaoni na ndo maana unaweza kuta kitu kinauzwa bei nzuri ila kikawa hakiji tanzania. ila katika shipping agent ndo pakuangalia maana ukikuta msafirishaji ni DHL ujue bei ni juu ila mzigo haumalizi hata wiki unakuwa umefika
 
Vipi mzigo ukifika posta hakuna makato mengine kama kodi..?
kodi ipo kwa baadhi ya mizogo hasa simu na vifaavingine vya umeme ni swala la kufuatilia pale posta uweze kujua ni vipi vinapigwa kodi na vipi havipigwi ili ukiwa unanunua uwe unafahamu ,
 
kamati yamaamuzi magumuu

KiKuu ni wapuuzi sana unaagiza kiatu size 43 wao wanakuletea 39 halafu wanabandika namba 43 pumbavu ha.ufikishwaji wa bidhaa hovyo, huduma kwa wateja mbovu....unaweza pick sandals za ngozi halafu wao wakakuletea yeboyebo(slipper) sina hamu nao

nishafutaga App yao kitambo......ila bidhaa zao ni affordable
 
dropshing kwa aliexpress.
Sasa mchango wenu kati ya Kikuu na AliExpress yupi bora.
Aliexpress ni bora
- Sababu kikuu anachukua bidhaa aliexpress na web zingine za china na kuweka kwenye site yake.

Hitimisho.
- Kama unafahamu kufanya manunuzi online ni vyema ukaagiza mwenyewe toka aliexpress/ banggood/ gearbest na site zingine nilizo orodhesha hapa www.bit.ly/101buy4me kwenye post ya pili.
- Faida utakayoipata kwa kuagiza direct bila kupitia kikuu ni kuwa utaweza kuchagua shipping Agent utakayehitaji kulingana na muda ambao unataka bidhaa ikufikie.
- Hivyo sio sawa kulinganisha KIKUU na ALIEXPRESS
 
Mzigo unafika posta ata kama sina sanduku la posta?
- Inashauriwa uwe na sanduku la posta ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza au kupoteza mzigo wako.
- Wapo waliopokea mzigo kwa kuweka tu namba ya simu/ jina la wilaya yake/ mkoa - Ila sio njia ya sahihi na aishauriwi kabisa LBDA kama unatumia huduma ya EMS hapo ondoa shaka.
- Pia iwapo utatumia njia za haraka za usafirishaji kama DHL hapo sanduku la posta halihitajiki, ni physical address yako na namba ya simu inatosha.
 
Mkuu niko.zenji vipi na hapa zenji naweza agiza vitu nje mkuu kupitia posta ama..?
 
Mi natumia posta mwaka wa 3 sasa na sijawahi poteza mzigo wangu.....
Hawezi pewa mtu mzigo wako maana ukienda kuchukua parcel yako lazima utoe kitambulisho cha NIDA ndo unapewa na kuhusu kodi ya bidhaa imeongezeka kutoka 1500 mpk 3000 ukiwa una parcel ndg ila kuna baadhi ya store ukinunua wanalipia mpk kodi ya mzigo wako we ukifika unachukua tu
 
Mkuu niko.zenji vipi na hapa zenji naweza agiza vitu nje mkuu kupitia posta ama..?
Ndio unaweza cha msingi ujaze detail zako zote na utaweka option ya kutumiwa posta au kwa sandk lako laposta na utaweka zip code, namba ya simu, kitambulisho cha NIDA na vingne vyote ....
Muhimu Zip code, namba ya simu na eneo unalokaa ..ukiwa mkoani kama vile shinyanga, singida na kwngne hutafaidi izi application coz inachukua mda mrefu kukufikia bidhaa ako na utalipia additional charges
 
Mi natumia posta mwaka wa 3 sasa na sijawahi poteza mzigo wangu.....
Hawezi pewa mtu mzigo wako maana ukienda kuchukua parcel yako lazima utoe kitambulisho cha NIDA ndo unapewa na kuhusu kodi ya bidhaa imeongezeka kutoka 1500 mpk 3000 ukiwa una parcel ndg ila kuna baadhi ya store ukinunua wanalipia mpk kodi ya mzigo wako we ukifika unachukua tu
Mkuu unachukulia posta wapi..?

Mimi sina uzoefu kabisa nasijui hata nianzie wapi..
 
Back
Top Bottom