Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,805
- 1,293
KIKAO CHA MBUNGE WA JIMBO NA WAKUU WA SHULE (HEADMASTERS) ZA MUSOMA VIJIJINI
Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 lina jumla ya Sekondari 27 ambazo:
- Shule za Sekondari 25 ni za Kata/Serikali
- Shule za Sekondari 2 ni za Madhehebu ya Dini (SDA & Katoliki)
Mbunge wa Jimbo ataitisha KIKAO cha kutathmini matokeo ya mitihani ya:
- Kidato cha Pili (Form II)
- Kidato cha Nne (Form IV)
LENGO KUU
- Kutathmini matokeo ya mitihani ya vidato hivyo viwili kwa Wanafunzi wa Musoma Vijijini
- Kutoa mapendekezo ya kuboresha mbinu za kujifunza (uelewa) na kufundisha
Mahali pa kufanyika Kikao:
Busambara Sekondari
Tarehe ya Kikao:
Itategemea upatikanaji wa Matokeo ya Mitihani ya Form IV (2022).
Usafiri & Chakula:
Mbunge wa Jimbo atagharamia
Miaka kadhaa ya nyuma, Mbunge huyo alishirikiana na Serikali ya Mkoa wa Mara kufadhili Kongamano la kuboresha Elimu Mkoani mwetu (Mara).
Walimu Wakuu (Headmasters) wa Sekondari zote 27, wanaombwa kujitayarisha.
Usisahau kutembelea Tovuti ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumatano, 11.1.2023