Wananchi wa kijiji cha Toraja, huko Sulawesi ya Kusini, nchini Indonesia, kila baada ya miaka mitatu, hufukua na kusafisha maiti ya ndugu zao.
Ieleweke kuwa hawafukui maiti hiyo hiyo kila miaka mitatu ila kila maiti inapozikwa, kwa wale wanafuata utamaduni huu, hufukuliwa mara moja na kusafishwa na kuzikwa tena. Na sherehe hiyo inafanywa kila miaka mitatu katika mwezi wa Nane.
Sherehe hiyo inaitwa Ma'nene na wananchi wa kijiji hicho wanaamini kuwa kufanya hivyo inawaletea baraka kwa kuwakumbuka marehemu na kuwasafisha na kuwavalisha nguo ili wapendeze na kuwabariki.
Haijulikani imeanza lini hii sherehe na serikali haiingilii zoezi hili kulinda utamaduni wa watu wa kijiji hiki.
Kweli ustaarabu ni suala la tafsiri tu wala sio kuvaa suti na tai. Huku Afrika tukiabudu miti, Magharibi wanatuita washenzi. Wao wakioana midume tupu sie twawaita wana laana. Wengine hawa wanafukua maiti. Malimwengu haya!
Kufufua maana yake ni kurudisha uzima katika mwili ambao ulikuwa umetoka. Kufukua ni kutoa kitu kilichokuwa kimezama ndani ya tifutifu. Sasa awa wanarejesha uhai?