Kijiji gani ardhi yake ina rutuba, na gharama za kilimo ziko chini?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
32,537
47,549
Sasa ni muda muafaka kwa vijana kuingia kwenye kilimo. Najua vijijini gharama za kilimo huwa chini, unaweza kubahatisha mashamba yenye rutuba na yanakodishwa kwa bei nafuu.

Na pia katika kuimarisha umoja katika maeneo hayo, wanakijiji hao hao wanakuwa vibarua kwenye hayo mashamba, ambapo unaweza kuwalipa Tsh. 2000 kwa siku n.k, na mwisho wa siku ukawa umewapelekea mzunguko wa fedha.

Kupitia uzi huu, tuainishe vijiji vyenye mashamba yenye rutuba pamoja na gharama za ukodishwaji.

Tubadilike sasa, tuwe wawekezaji wa ndani.​
 
Kwa Kilimo cha Mahindi Vijiji vyote vya Wilaya ya Songea na Mpanda Katavi.

Kilimo cha Maharage Kijiji cha Mwesse Wilaya ya Tanganyika. Wenyeji ni Wanyarwanda walipewa Kijiji hicho mwaka 1972 so usiulize sana kwa sasa washapewa Uraia ni Watanzania wenzetu. Wako verry smart na Uaminifu ni 100% ukinunua au kukodi shamba.

Kilimo cha Mpunga Nenda Bonde la Ziwa Rukwa Muzye huko utavuna gunia za kutosha tuu hapa Mjini utaishia kuitwa Muuza Unga au Freemason maaana watakua hawakuoni ukienda kazini bali kutumia tuu.
KILIMO UNAPOKIANZA KITAKUTESA LAKINI BAADA YA MISIMU MIWILI AU MITATU YA KUTAFUTA UZOEFU UNAANZA KUPATA.

Note: unapoanza kilimo msimu wa kwanza au wa pili faida hutoiona au utapata kidogo lkn kadri unavyoendelea utapenda mwenyeeeeee. Tatizo wakulima wapya mnakuja na Matokeo ya kupata mamilioni mara moja tu haiko hivyo.

Karibuni kwenye fani
 
Good
 
Bonge la mwalimu
 
Back
Top Bottom