Kijana unayejitambua kama una 1.5M fanya hii kitu utakuja kunishukuru

Ninavyofahamu ukiwatumia wataalamu na kufuata ushauri wao unaweza ukapotea.

Mfano pale Kiteto, Manyara, tulikuwa tunalima mahindi ambapo mbegu tunachagua kutoka kwenye mavuno ya shambani hapo hapo na hatukuwa tunatumia mbolea ya kiwandani.

Pia tulikuwa tunapanda mahindi kwa kutumia jembe la trekta la kulimia ile plaugh.

Huu ni aina ya mfumo ambao mtaalam hawezi kukuelewa

Hata mm naukosoa… unaweza kuwa sahihi kama soko pake likiwa todauti na watiotumia mbolea ya kiwandani… kinyume na ivyo unajipunja sana. Naweza kukueleza zaidi ukitaka
 
Mkuu tupe ushuhuda na wewe umetusua??

Wewe pia umelima tena ila katika wnaaotusua naona unatoa mifano ya wengine.
Nilikuwa na mambo mengi nilikaa kambi mwezi 1...then nkarudi chuo,ile kurudi ndo nikaharibu kila kitu
 
Umeshauri vizuri ila kilimo aisee shikamoo kilimo na changamoto zako
Ni probability ,unawekeza 1.5m unakosa mavuno .
Unatoa 200,000/= ndo umepigwa hivo.
Unatoa wapi tena hizo 1.5m ili kuwekeza tena .
Kila kitu ni chepesi kama haujafanya ,ila kiuhalisia ni kupata au kukosa.

Tena hiki kizazi kinachotaka kukaa kwenye lami, wakati mashamba yako porini.
 
Habari zenu wakuu,

Leo nataka niandike maneno kadhaa kwa vijana wenzangu tunaojitambua. Naandika kuhusu vijana wanao jitambua namanisha wale walio na uchu wa mafanikio na wenye ndoto ama malengo makubwa hapo mbeleni panapo majaaliwa.

Hili bandiko ni chugu kwa vijana wa hovyo na wasio jielewa, maana ni hakika watapinga na kuona ni ngumu. Hapa nasema na wanaume haswa wanaojitambua na kupevuka kiakili, sio wale mabishoo uchwara.

Twende kwenye pointi sasa, kijana unae jitambua hii Tanzania yetu ni kubwa sana ni wewe tu kuamua uende wapi. Nita andika kuhusu sekta ya kilimo ambapo bado kuna fursa ila asilimia kubwa ya vijana wameona ni ujinga kuingia huko kumbe sio. Kuna wale vijana huwa wanakuja hapa na mitaji kuanzia 1.5M mpaka 5M na kuuliza wafanye biashara gani, kijana unae jitambua nakushauri ingia kwenye kilimo kwa kumanisha kweli kweli. Vijana mlio kuwa chuo na mpo mtaani tu hamuelewi mfanye nini ingia kwenye kilimo na uache malalamiko ya kukosa ajira, huna connection unataka ajira utasugua sana kwa Tanzania hii. Ni bora huo muda ujikite kwenye kilimo.

Kijana tafuta mikoa yenye uhakika wa mvua nashauri kwa mikoa hii ifuatayo, Katavi, Rukwa, Morogoro na Songea kama kuna mwingine wadau wataongezea. Katika hiyo mikoa tafuta wilaya yenye mashamba ya uhakika kisha jikite kwenye kilimo cha mahindi pekee. Kwanini mahindi, kwasababu kilimo cha mahindi hakina mambo mengi na ni rahisi kwa mtu anayeanza pia ndio zao linalolimwa kwa asilimia kubwa nchini kwetu.

Kijana hamia porini kabisa weka kambi yako huko jipe miezi tano tu, hiyo miezi sio mingi kwa mpambanaji na anae jitambua. Kodi heka tatu kisha piga kilimo cha mahindi, hiyo 1.5M inatosha kila kitu kuhudumia shamba. Yaani hapo kuanzia kukodi, kulima, kupanda, kupalilia, madawa, mbolea mpaka unavuna mazao yako. Hiyo hela ni nyingi sana kwenye kilimo cha mahindi, hiyo hela wewe unakuwepo shamba kuhakikisha kila hatua inakwenda sawia.

Kijana jiandae na msimu ujao wa kilimo cha mahindi kisha fanya hiyo project baada ya miezi mitano utakuja kunishukuru nakwambia. Vijana tumeng'ang'ania tu mjini kwa mambo yasio na msingi wowote ule kwenye maisha yetu na wakati huo muda ukituacha matokeo yake ni kulalama kila uchwao.

Kijana jikite porini huko piga kilimo chako kwa umakini na kwa kumanisha, ingia porini huko kaa miaka mitatu mpaka mitano kisha utaona matunda yake. Kijana ni ukumbuke kuwa maisha hayapo kukusubili na anaekupenda zaidi ni wewe mwenyewe, na huo ndio ukweli mchungu. Wavaa vipensi lazima wapinge!

Mkono wa Papaa Gx
Kuliko kwenda kuichimbia hiyo 1.5 Bora nifanye jambo jingne huk town
 
Good idea but for to be realistic 1.5M kwenda kujichimbia mkoa ambao si mwenyeji kwa miezi mitano ni ndogo sana. Hapo hizo heka tatu kijana ambaye kazaliwa mjini sidhani kama ataweza kuzilima mwenyewe, miezi hiyo mitano atakuwa anakula nn?

So kumsaidia kijana huyu ni bora kupiga hesabu nzima pamoja na estimate ya gharama za kujikimu, vibarua..
Mkuu hapo unatumia akili tu, unafika unanunua kuku wadogi wa elf 5 tano vijogoo kama 50 hivi unabaki na 1.25M hao utakuj kuuza kwa ajili ya palizi.
 
Ni probability ,unawekeza 1.5m unakosa mavuno .
Unatoa 200,000/= ndo umepigwa hivo.
Unatoa wapi tena hizo 1.5m ili kuwekeza tena .
Kila kitu ni chepesi kama haujafanya ,ila kiuhalisia ni kupata au kukosa.

Tena hiki kizazi kinachotaka kukaa kwenye lami, wakati mashamba yako porini.
Mkuu punguza kidogo inauma
 
Back
Top Bottom