Kijana aliyemtusi Rais, Isaac Emily ahukumiwa jela miaka 3 au kulipa faini

Huyu ilibidi apigwe vyote kwa pamoja ili iwe fundisho kuwa Rais si bibi au babu yako!

Mahakama imetenda haki inapaswa kupongezwa.
Kesho itakuwa kwa ndugu yako, you just wait! Time will tell! Hizi ni sheria kandamizi mtu mwenye busara hapashwi kuzitetea. hakuna anayesema kuwa mtu atukane, lakini kuna uhuru wa kujieleza na kusema unaloliona ndio unavyoamini! Kesho itakuwa kwa ndugu yako anayekuhusu, labda kama umekufa roho hutaumia!
 
Always what you cultivate, you will earn the same,
Mkiambiwa acheni matusi, uchochezi, chuki zisizo na maana, na mihemko hamtaki kuelewa kwa kisingizio cha uhuru wa kutoa maoni (freedom of expression ) ona sasa, walio nyuma yake sidhani kama wataingia Atm kutoa pesa ya kulipa hiyo faini zaid ni yy mwenyewe!!
Walio nyuma yake wanatakiwa wamchangie hiyo million saba!

Lakini mchuma janga hula na wakwao...sasa hivi ndugu zake ndio wana hangaika kutafuta hiyo hela!
 
Kamwe ndugu zangu hawawezi kukosa heshima kiasi hicho hadi kumtukana Rais!
Wangapi wamemtukana baba yako/mama yako/shangazi/ mjomba wako etc na hujawafanya lolote? Hujawasemea kama unavyomsemea rais! Nani wa heshima zaidi, Baba yako au Rais? Najua kwa nyinyi nshomile BK watu vijijini wanatukanana sana. Huwezi sema hao niliowataja hawajawahi tukanwa! I have lived there over 20 yrs!
 
Akomeee tuu na heshima aishike..nkimuangalia namuona mtu mwenye maisha magumu sana lakini mdomo wake mchafu
 
Mkapa alitukana hadharani sijui sheria ilikuwa haijatungwa?

Au wakubwa wao watahukumiwa na Mungu siku ya kiama?
 
Kesho itakuwa kwa ndugu yako, you just wait! Time will tell! Hizi ni sheria kandamizi mtu mwenye busara hapashwi kuzitetea. hakuna anayesema kuwa mtu atukane, lakini kuna uhuru wa kujieleza na kusema unaloliona ndio unavyoamini! Kesho itakuwa kwa ndugu yako anayekuhusu, labda kama umekufa roho hutaumia!
Uhuru wa kujieleza ndo kutukana??
 
Wangapi wamemtukana baba yako/mama yako/shangazi/ mjomba wako etc na hujawafanya lolote? Hujawasemea kama unavyomsemea rais! Nani wa heshima zaidi, Baba yako au Rais? Najua kwa nyinyi nshomile BK watu vijijini wanatukanana sana. Huwezi sema hao niliowataja hawajawahi tukanwa! I have lived there over 20 yrs!
Wewe endelea....
 
rais wa nchi anatakiwa kuheshimiwa huyu si rais wa FM academia au rais wa TFF tunatakiwa ku restore nidhamu ya vijana wetu si ukiwa na kisimu au kilaptop unweza kuandika chochote tu leo vijana wanamuogopa mwanajeshi kuruta lakini rais wa nchi wanamuona kama vile sanamu wanatakiwa kujua hata ukijificha nyuma ya keyboard ya simu au laptop yako nyumbani kwako mgagala majimatitu watu wakiamua kukutafuta utapatikana tu sasa huyo mu R chuga akauze nyumba ya urithi apate hyo 7 mil au aende akapumzike jela
 
Endeleeni tu kudadisi, tatizo lenu mnafikiri hadhi ya rais ni sawa na mwananchi wa kawaida tu!! Baadhi ya watu hufikiri wana nafasi sawa na mkuu wa nchi kwa kujilinganisha kila alisemalo au kulitenda, ieleweke tu kuwa kiongozi wa taifa ni bora umuogope kama hutaki kumheshim ili ujipunguzie matatizo!! Hautavumiliwa kutoa lugha chafu kwa mkuu wa nchi kama vile unawasiliana na mtani wako/mshikaji,
Hekima na utulivu wa mawazo unasaidia sana kuondoa adha kama hizi!!
Ni kweli, lakini isiwe kitisho kikuu cha Uhuru wako.
 
Walio nyuma yake wanatakiwa wamchangie hiyo million saba!

Lakini mchuma janga hula na wakwao...sasa hivi ndugu zake ndio wana hangaika kutafuta hiyo hela!
Ndo hvyo kujifanya unajua harakati ni tatzo tu, hizo 7mills ni fedha nyingi ambayo angeiokoa kwa hekima na uwasilishaji wa hoja zake pasipo kuruhusu mihemko!!
 
Back
Top Bottom